Soko la mibono (jatropha)

Gajungi

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
257
83
Habari zenu wanajamvi.

Nilipenda kuulizia mwenye ujuzi na biashara ya Jatropha. Mimi nina namna ya kupata jatropha kwa wingi sana kwa hiyo anayejua soko la Jatropha anijulishe.

ASANTENI

1624963608619.png
 
Habari wakuu,

Kuna mdau mwenzetu humu kanishauri dawa flani ya kiasili ya kutibu tatizo la Ulcers ambayo kwa bahati mbaya haipatikani mkoa nilipo.

Dawa yenyewe ni mmea uitwao Jatropha. Kwa ambae anaweza nisaidia kunifikishia hapa Mwanza Itapendeza sana kwani nimeteseka muno muno hasa tatizo la gesi tumboni iliyoletwa na hii ulcers.

Msaada tafadhali.
 
Niliwah kuishi kilwa maeneo ya nangurukuru na mavuji mimea hii n mingi maeneo hayo Kwan kulikuwa na kiwanda cha mibono maeneo hayo
 
Kuna mama jirani yangu aliombwa mizizi yake kwamba ni dawa ya figo, anadai hakupewa maelzo jinsi kutayarisha hiyo mizizi Ila alipelekwa duka la karibu akanunuliwa mahitaji muhimu ya ndani ya kutosha jamaa akaondoka na mizizi.

Mjuzi wa hii dawa atujuze tafadhali
 
Hahaa hii kitu ilivuma sana miaka ya 2009 hadi na 10 na huko.Kulikuwa hadi na NGO's wanadili na hii kitu.

Hizi zilikuwa kupigwa vita sana kwa sababu ya mambo ya kimazingira make zinaharibu sana mazingira.

Arusha kulikuwa na Taaasisi wanadili nazo.

Mafuta yake yalikuwa yanaendesha mitambo ya Desel engene. Na pia mafuta yake yalikuwa yanatengeneza sabuni na vitu vingine vingi.

Shida kuu ni kwamba yalipigwa sana vita kwa sababu pia yalikuwa yanaweza sababisha njaa,Kuna watu walianza kulima.in lager scale lakini nazani walisha acha.

Wale Jamaa walio pewa yale Mashamba ya Mpunga ya Kapinga kule Mbeya nao walikuwa na mchakato wa kuacha kulima Mpunga walime haya mavitu sijui iliisha vipi.

Ili uyauze au ufanye viashara zake inahitaji Production kubwa sana kitu ambacho hakipo kwa sasa Tanzania.

Hii inatakiwa kuwe na plantantion za haya mavitu.

Ukitaka Detail zaidi naweza kukuunganisha na mtu alie kuwa kwenye hio NGO akuambie ilisha isha vipi na hata detail zingine za haya mavitu.
 
Mbegu zake zina mafuta sana, unaweza test mwenyewe ukakausha zeni ukazimenya ukaziwasha zinawaka balaa, kulikuwa hadi na Aina fulani ya majiko yanatumia hizo mbegu za mibono nayo sijui yaliishia wapi,

Inaelezwa hii mibono ilitumiwa sana na watu wa kale enzi hizo kuwasha moto
 
Mbegu zake zina mafuta sana, unaweza test mwenyewe ukakausha zeni ukazimenya ukaziwasha zinawaka balaa, kulikuwa hadi na Aina fulani ya majiko yanatumia hizo mbegu za mibono nayo sijui yaliishia wapi,

Inaelezwa hii mibono ilitumiwa sana na watu wa kale enzi hizo kuwasha moto
Aisee hilo jiko ninalo mpaka leo,walipo kuwa wana promote walikuwa wanakupa na kichupa cha hayo mafuta ya mbegu za mimbono yakiisha nanma ya kuyapata ndiyo ilikawa ngumu.
 
Back
Top Bottom