Soko la mahindi tatizo kwa wakulima

Soko la mahindi tatizo kwa wakulima

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Habari wana JF.

Mimi ni mwal. kwa taaluma yangu na nimeanza kazi mwaka jana wilayani mbinga, kutokana na ukweli kwamba swala la mishahara midogo katika kada yetu imekuwa ni kilio cha muda mrefu, kijana na kataaluma kangu nikaamua nisibweteke ngoja nichangamkie fursa na fursa yenyewe kwa mazingira yangu ni kilimo, kijana nikajitahidi kujibanabana kutoka kwenye kamshahara kangu nikaingia shambani kwenye kilimo cha mahindi.

Basi ikawa mimi na kilimo kilimo na mimi na kwa kuwa ni mfanyakazi inanilazimu kazi nyingi kutumia vibarua ili kazi yangu kubwa ikiwa ni kukagua na kusimamia siku za weekend, gharama za mbolea, vibarua nk nilifanikisha kuzikabiri na mungu amenisaidia nimevuna zaidi ya gunia 80.

SOKO LA MAHINDI 2014/15
Ndugu zangu hapa ndo nimechanganyikiwa kwani kinachofanyika mwaka huu katika soko la mahindi ni kizunguzungu tu kwa mkulima, kama tunafuatilia mambo haya ni kwamba serikali mwaka huu mbali na kwamba imepanga kununua tani chache sana za mahindi kwa msimu huu pia serikali kupitia NFRA imeamua kununua mahindi hayo kupitia kwa mawakala.

Kinachotokea kwa mawakala hao ni kuwa wamepangiwa tani za kununua lakini waliowengi ni wafanyabiashara wakubwa ambao kiasi kikubwa cha tani hitajika kinatokana na mzigo walio nao hivyo kusababisha mkulima wa chini kukosa nafasi ya kuuza mahindi yake, na mawakala hao wanatumia pia mwanya huo kuununua mahinndi kwa bei ya chini (Tshs. 18000 -21000) kutoka kwa wakulima waliokosa soko na wao kuyapeleka NFRA. Kero ni nyingi wala nisiwachoshe ndungu zangu.

Binafsi pamoja na wakulima wengine wengi tu hadi leo tumekosa soko la kupeleka bidhaa zetu tumerundika mahindi sehemu fulani ambapo tuliambiwa mnunuzi fulani angekuja kununua hadi leo hii haonekani na kuna tani takribani 4500. hadi sasa hatuelewi nini cha kufanya, zaidi tu nashindwa kuelewa vijana wanapolalamika hakuna ajira watu wengi tumekuwa tukiwabeza na kuwaambia wajiajiri lakini tumekuwa tukisahau mfumo wetu na sera zetu zisivyovutia sana kumwinua kijana huyo mwenye mtaji mdongo.

Mwisho; naomba sana kwani JF ni jukwaa linalojumuisha watu mbalimbali, kama kunamdau anahitaji mahindi kwa ajili ya kupack unga, kuuza nk. naomba tuwasiliane ili kuweza kuokoa jahazi kwani msimu wa kulima ndo unakaribia na pesa hakuna. Shukrani kwenu wadau!
 
Mie nilishajiondoa kwenye haya mambo ya kulima maana kuna kilio
 
vijana weng hampendi kujiajir ndo kauli za magamba hzo
kwa mazngira gan?
RUUUMA kwa ujumla soko la mahndi ni tatzo kubwa
 
rushwa imetawala wakulima wadogo wanaumia
kwan uthaman wao haupo kwa sasa mpaka uchaguzi wapewe kofia na kanga 4 gud lfe
 
Njoo uuze Arusha bei inalipa saiv 35000 kwa gunia lkn mwez wa 10 inapanda mpaka 50000 Kwa gunia, kaz ni kwako!
 
vijana weng hampendi kujiajir ndo kauli za magamba hzo
kwa mazngira gan?
RUUUMA kwa ujumla soko la mahndi ni tatzo kubwa

huko Ruvuma mnapenda kuchagua Magamba yakisha pata viti vya ubunge yanahamia Dar. Dawa ni kupiga chini magamba yote ili tuje tupate serikali itakayo wajali wanyonge
 
Back
Top Bottom