Soko la kimataifa nafaka kutumia bil. 11/-

Soko la kimataifa nafaka kutumia bil. 11/-

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1109602


MCHAKATO wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa soko la kimataifa la nafaka ambalo uwekezaji wake utagharimu Sh. bilioni 11 katika eneo la Kwa Sadala, Wilaya ya Hai, umepewa jina la ‘The Magufuli International Complex Centre’ (MICCHai).

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amesema mchakato huo umeiva na kwamba soko hilo litajengwa karibu na kiwanda cha Arsho au karibu na njia panda ya kwenda Masama. Ole Sabaya alikuwa akizungumza mwishoni mwa wiki na watumishi wa halmashauri wa wilaya hiyo, madiwani, viongozi wa dini, taasisi za fedha na wadau wa maendeleo ambao wamekubali kutoa fedha hizo.

“Soko hili litakuwa na kazi ya kuongeza thamani ya mazao, kuchochea pato la mkulima na kuingizia serikali kodi, litakuwa na eneo maalum la viwanda vya usindikaji, eneo la utalii zikiwamo hoteli, kituo cha habari za utalii, migahawa ya kisasa na maeneo ya huduma za kibenki, bima, kumbi za kisasa za mikutano na maduka makubwa.

Muda ambao mradi huu utatekelezwa ni miaka miwili na utagawanyika katika awamu tatu,” alieleza. Kwa mujibu wa Ole Sabaya, mradi huo unafadhiliwa na serikali ya Tanzania, Halmashauri ya Wilaya ya Hai na wabia wa maendeleo yakiwamo mashirika binafsi na kampuni binafsi. Karibu asilimia 70 ya wakulima wadogo katika wilaya hiyo, wanajishughulisha na kilimo cha ndizi na kilimo cha mbogamboga kwa mwaka mzima.

Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa kimkakati, utakaotumia miezi 12 kufanya vipimo, michoro, kuandaa eneo la kuweka vifaa vya ujenzi wa mradi na kufanya mapitio ya kiasi cha uhitaji wa mitambo.
Ujenzi wa soko la kimataifa litakalokuwa na viwanda vya usindikaji wa nyanya, ndizi, kahawa, matunda na mboga, utatumia kiasi cha Sh. bilioni 8, wakati ujenzi wa kituo cha habari za utalii na maeneo ya huduma mbalimbali za kijamii, utagharimu Sh.bilioni 2 na manunuzi, usimikaji na majaribio ya mitambo na uendeshaji wa viwanda utaigharimu Sh. bilioni 1.
 
‘The Magufuli International Complex Centre’ (MICCHai). ,🙄🙄🙄🙄
 
Back
Top Bottom