let the caged bird sings
JF-Expert Member
- Sep 19, 2020
- 4,179
- 9,750
Japan:-unajua moja ya sababu ya Mwalimu kuaingia vita na Amini ni kwasababu kuna Mwehu mmoja ndani ya jeshi la Amini aliingia ndani ya Ardhi ya Tanzania akanywa Gongo then akaanza fyatua risasi hovyo ndani ya Ardhi ya Tanzania na tukio hilo likachukukiwa kama uchokozi mkubwa.yaan kufyatua risasi tu ikawa ni moja ya sababu ya Tanzania kuingia vitani.Japan walipokwa haki yao kwa kurushiwa mabomu ya nyuklia,
Kuna Afghanistan, iraq, iran, libya.
Cuba walipokwa haki kwa kuwekewa vikwazo kisa mabomu ya nyuklia.
Hata Us kuwanyima wengine kumiliki nyuklia ilhali nae anayo na ndio kinara ni kupoka uhuru wa nchi huru zenye kujipangia mambo yake mengine
Sasa 7 Dec 1941 unprovoked Japan ikaingiza jeshi lake ndani ya Marekani na kufanya uharibifu mkubwa na watu 2,403 wakafa... Sasa kufyatua risasi tu kuliingiza Tanzania vitani, mfyataji hakuua wala kujeruhi mtu ila vita ikatokea ila kwa US unaashilia kusema haikupaswa kujibu chochote dhidi ya Japan ilhali watu 2,403 wamekufa?.
Sikubalini na jibu zito la US, ila naunga mkono kujibu kwake.
tunaishi katika dunia ambayo hupaswi kumuacha Mungu kila kitu.
AFGHANISTAN:- Baada ya Osama kuwazidi Ujanja US akakimbilia Afghanistan, Bush akawaomba Taleban kwa amani wamkabidhi Osama kama alivyo.. Taleban hawakukataa kuwa Osama hayupo ndani ya Ardhi yao bali walikataa kwa dharau tu kumkabidhi Osama kwa Bush.
Unajua Sep 11 Osama aliondoa Roho za watu wa ngapi? Unajua ni hasara kiasi gani Osama aliyoitia US?.
watu 2,753 walikufa na majeruhi ni karibia namba ya wafu.. Yaan Mtu aje kwako aue watoto wake na akimbilie ndani ya nyumba ya jirani yako then umuombe huyo jirani yako kwamba:, Khamis kaja nyumbani kwangu, kaua watoto wangu na kuvunja madirisha ya nyumba yangu then akakimbilia ndani mwako.
Then jiran yako akujibu:, ni kweli khamis yupo ndani kwangu lakini siwezi nikamkabidhi mikononi mwako.. what would you do?.
Cuba:- uko sahihi, marekani aliiwekea vikwazo tu ila hakujaribu hata kidogo kufanya kama inachofanya Urusi I wish Putin nae angalifanya kama alichofanya US dhidi ya Cuba.
Nyuklia:- US wanaweza wasiwe sahihi katika ila fikiria dunia ambayo nyuklia inapatikana kama Ugoro Sokoni.. leo Boko haramu wana miliki nyuklia.
Alshababu wanamiliki nyuklia..
ISIS na wana nyukilia...ikiwa wanamiliki Ak47 tu moto wao haushikiki ni vipi wawe na nyuklia?.
Kuwa na nyuklia si tatizo, tatizo ni, unaaminika kuwa na hayo madude?.
Unajua hatari ya hayo madude yakiingia kwenye mikono hisiyo sahihi?.