IMEELEZWA kuwa, tani 200,000 za korosho zinazotarajiwa kupatikana msimu wa mwaka huu, zinaweza kulika nchini na kuleta faida kwa mwekezaji, tafsiri hiyo inaondoa hofukwa mwekezaji kama tarajio lake lasoko la korosho halitategemea sokola nje kama ilivyohofiwa na wafanya biashara.
Pamoja na soko la nje kushuka,pendekezo la serikali la wakulima kulipwa si chini ya shilingi 3,000 limeitikiwa na wafanya biashara mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakisema korosho za Tanzania kwa soko la China zina bei isiyo na ushindani.
“Japo wafanyabiashara hatuna ushirikiano wa masoko, soko la korosho sio la kubembeleza,” alisema Mkulima Mwekezaji, Dkt. Alex Macha wa Agrofarm International, Bagamoyo, mkoani Pwani. Dkt. Macha alisema mazao asili kama pamba, chai, korosho na mengineyo yamekuwa na masoko nje ya nchi lakini bado tunahitaji kuwa na ushirikianowa mawazo, nguvu ya ushirikiano ili kutosheleza mahitaji ya wanunuzi wa nje.
“Unakuta soko linahitaji tani nyingi kila mwezi lakini anayepewa soko hilo anafanya siri wakati uwezo wa kulitosheleza soko hana,” alisisitiza.
Maduka makubwa ya bidhaa (super market) yaliyotembelewa jana ili kujua mwelekeo wa mauzo ya korosho katika maduka yao, baadhi yao walisema korosho zipo na zina walaji nchini lakini zimepungua hasa mwezi huu, wakala wanaowaletea kutoka Mtwara na Lindi wamepungua.
Maduka yaliyotembelewa na Idara ya Habari-Maelezo, bei zao zinapishana na ile ya sokoni, kwenye maduka makubwa zinapishana kidogo, korosho zilizokaangwa na kufungwa zenye chumvi, pilipili au zisizo na kiungo kwa kilo ni sh. 35,000 hadi sh. 37, 000, nusu kilo sh. 15,000 hadi 19,500 na robo kilo ni sh. 10,500.
Kadhalika, katika soko la Kisutu ambalo huuza mazao ya chakula, wachuuzi wanauza korosho zilizobanguliwa na kukaangwa sh. 22,000 kwa kilo, wakati za kuchemsha zinauzwa Sh. 20,000 kwa kilo. “Kwa mahitaji mengi kama tani zaidi ya mbili lazima mtu atuandae na kusubiri ili zifuatwe Lindi,” alisema mchuuzi Zuberi Muswafa wa soko la Kisutu.
Akizungumza Ikulu kupitia vyombo vya habari, mapema wiki hii, Rais Dkt. John Pombe, alisema wafanyabiashara wanapotaka kununua korosho za wakulima sh. 1500 kwa kilo nikuwahujumu wakulima na kuhujumu uchumi wa nchi.
Pia alionya kuwa sekta binafsi inapaswa kuweka uzalendo wa Taifa mbele, serikali ilipendekeza sh. 3.000 kwa kilo moja.
Mvutano kati ya wakulima wa korosho nchini na wanunuzi wakubwa, umedumu zaidi ya mwezi ambapo Rais alikaa na wanunuzi hao, kuafikiana pendekezo la kuwalipa wakulima bei isiyopungua sh. 3,000 kwa kilo ya korosho, baadhi ya wanunuzi waliendelea kuwarubuni wakulima kwa bei ndogo chini ya makubaliano.
Wiki iliyopita Serikali iliamua kuchukua hatua za dharura ili kununua korosho za wakulima zinazokadiriwa kufikia tani 200,000,
ambapo wanajeshi wanafanya kazi ya usombaji na usimamizi, wakati Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwa ushirikiano wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko na Vyama Vikuu vya Korosho watawalipa wakulima.