Soka: MOTOMOTO za Usajili Ulaya!

Soka: MOTOMOTO za Usajili Ulaya!

kichwat

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Posts
1,819
Reaction score
593
- Edinson Cavani (26) anakamilisha mipango ya kutua ManCity. Chelsea na Real Madrid nao wamo kwenye mawindo. Lakini klabu imempa ofa nono ya mkataba wa £6m kwa msimu ili abaki.
- Kiungo mchezeshaji Eden Hazard (22) anawindwa na Monaco kwa dau la £40m.
- Gareth Bale (23) sasa anawindwa na Real Madrid kwa dau la ukweli la £85m (rekodi ya dunia). Tottenham wanasisitiza HAUZWI, watampa mkataba mpya wa mshahara wa £130,000 kwa wiki. Kumbuka Christiano Ronaldo alisajiliwa na Real Madrid kwa dau la £80m.
- Luis Suarez (26) HAUZWI. Lakini mtu akija na tita la kuanzia £50m atafikiriwa. Real Madrid wamemwaga ofa ya mkataba wa miaka 4 wa £140,000 kwa wiki.
- Christian Benteke (22) sasa ameanza mipango ya kwenda Arsenal au Tottenham. Anawindwa na Atletico Madrid kwa dau la £15m.
- Marouane Fellaini (25) huenda akabaki Everton kwa mpango wa kocha Martinez. Anawindwa na Juventus na ManUtd kwa dau la £24m.
- Kocha Roberto Martinez (39) huenda akatua Everton.
- David Villa (31) anakamilisha mipango ya kutua Tottenham kwa dau la £10m.
- Cesc Fabregas (26) ataamua wiki ijayo kama atabaki Barcelonaau kurudi Arsenal. Hana mpango wa kwenda ManUtd.
- Kipa mzoefu Julio Cesar (33) wa QPR anawaniwa na Arsenal katika mkakati wa kuimarisha safu ya ulinzi.
- Romelu Lukaku (20) sasa anawindwa na Liverpool kuchukua nafasi ya Suarez endapo deal la kwenda Real Madrid litakubali.
- mkoba wa Porto Eliaquim Mangala (22) yupo njiani kuelekea Chelsea, ikiwa ni mpango wa Mourinho kuimarisha safu ya ulinzi.
- Cristiano Ronaldo (28) HAONDOKI Madrid, hata ManUtd wakija na dau la £800m.
- Mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski (27) anawindwa na Borussia Dortmund na Atletico Madrid.
- Winga anayetisha Hispania Jesus Navas (27) anayeondoka Sevilla huenda akatua ManCity.

DONE DEALS:
- Radamel Falcao (27) ametua Monaco kwa dau la £50m, mkataba miaka 5. Monaco sasa inamilikiwa na bilionea mwingine wa Kirusi - Dmity Rybolovlev, na inafundishwa na kocha Claudio Ranieri.
- Kocha Jose Mourinho (50) amerudi Chelsea kwa mkataba wa miaka 4 kwa dau la £8.5m kwa mwaka. Atakuwa kocha ghali zaidi kuliko wote katika historia ya EPL.
- Winga kinda machachari Wilfred Zaha (20) amerudi ManUtd kutokea Crystal palace alikokuwa anachezea kwa mkopo na kufanikisha kuipandisha daraja.
- Kocha Rafael Benitez (53) ametua Napoli, kazi yake ya kwanza ni kukamilisha dili la Cavani kwenda Chelsea.
- Neymar da Silva (21) ametua Barcelona kwa mkataba wa miaka 5 kwa dau linalokairiwa kufikia €28m.
- Kocha Mark Hughes (49) ametua Stoke City
- Kocha Manuel Pellegrini (59) ndiye kocha mteule wa ManCity. Mkataba kusainiwa ndani ya wiki 2 zijazo.
- Beki Kolo Toure (32) ametua Liverpool kuimarisha safu ya ulinzi baada ya Jamie Carragher kustaafu.

Vyanzo: goal.com; skysports.com, BBC.com, caughtoffside.com na ESPN.3
 
Wilfred Zaha, winga kinda machachari anayerudi ManUtd huenda akawa tishio EPL msimu ujao.
 
Gareth Bale (23) sasa anawindwa na Real Madrid kwa dau la ukweli la £85m (rekodi ya dunia). Tottenham wanasisitiza HAUZWI, watampa mkataba mpya wa mshahara wa £130,000 kwa wiki. Kumbuka Christiano Ronaldo alisajiliwa na Real Madrid kwa dau la £80m.
 
Chifu, kuna threads zenye vichwa 'transfer news update 2013/2014' na 'football transfer centre 2013', ndani ya jukwaa la michezo.
Unaweza omba moderators waunganishe hii thread na mojawapo ya hizo threads.
 
No need. Hii thread iko neat na ame outline vizuri sana. Halafu si kila thread zinazoelekeana zinapaswa kuungwa.
 
No need. Hii thread iko neat na ame outline vizuri sana. Halafu si kila thread zinazoelekeana zinapaswa kuungwa.

Umezisoma threads nilizomwonyesha? Threads hizo zimebeba ujumbe kama wa hii thread. Tena mbaya zaidi kuna ile thread ya 'transfer window update...." ina ujumbe kama huu huu uliopo kwenye post ya kwanza ya kichwat

Ebu angalia hizi threads, halafu useme kama kuna haja ya kuwa na thread nyingine:

https://www.jamiiforums.com/sports/...er-centre-2013-transfer-news-and-rumours.html

https://www.jamiiforums.com/sports/444910-transfer-window-updates-2013-2014-season-europe.html tena hii imeanzishwa na kichwat mwenyewe!!!
 
Agreed.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom