soka la bongo bwana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

soka la bongo bwana!

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Mar 3, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Papic raia wa Serbia hajalipwa mishahara ya miezi miwili hadi mitatu na mara kadhaa amewaambia rafiki zake wa karibu kuwa ataondoka na kurejea kwao Ulaya baada ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Eloi Lupopo iliyochezwa Jumamosi iliyopita mjini Lubumbashi.

  Jana, Championi Jumatano lilimsaka na kufanya naye mahojiano maalum naye alisema hivi, “Kweli kwa sasa sina tena sababu ya kuficha, sina raha tena hapa Yanga. Ninastahili kuondoka na kuangalia sehemu nyingine.”

  “Unatambua kuwa mambo mengi sana yaliyo katika mkataba wangu na Yanga yamevunjwa. Lakini sikuona sababu ya kuanza kuanika kila kitu mapema kwa kuwa tulikuwa na jukumu kubwa mbele yetu la kuing’oa Lupopo, bahati mbaya hatukuweza,” alisema Papic baba wa watoto wawili, Todor na Natas na kuongeza.

  “Kweli sielewi wananichukulia vipi, siwezi kuishi hapa nikifanya kazi halafu fedha ya kuendesha maisha natumiwa kutoka Ulaya. Lakini pia suala la fedha kwangu si kubwa sana hata kama nafanya kazi ili nizipate. Ile hali ya heshima tu, mimi ninaamini wananidharau na kuninyanyasa, wangenilipa ili kuonyesha tu wanajali.

  “Kila mwezi hadithi ni zile zile, hakuna mabadiliko na ndiyo maana nimewaambia kesho lazima tukutane na uongozi na kulijadili hili. Kama hawatataka kufanya hivyo, sitakuwa na kinyongo, nitabeba mizigo yangu na kuondoka. Ni nguo mbili zilizo nje ya begi langu hadi sasa,” alisema Papic akionyesha kuwa na hasira.

  “Nasema imetosha! Imetosha! Dharau hii siwezi kuivumilia, mkataba wangu umevurugwa, mshahara silipwi na hakuna anayeonyesha kushtuka,” alisema kocha huyo aliyeleta mabadiliko makubwa Yanga katika kipindi kifupi ambaye pia amewasilisha maombi ya kuinoa Taifa Stars.

  Mkutano huo wa uongozi wa Yanga na kocha huo ndiyo pekee unaoweza kubadili mambo ingawa, hali halisi inaonyesha Papic hatakuwa na muda mrefu ndani ya Yanga kwa madai ya kukasirishwa na hali ya kuonyesha kumdharau.

  Papic aliyewahi kuzinoa klabu kubwa kama Enyimba, Lobi Stars (Nigeria), Kaizer Chiefs, Orlando Pirates (Afrika Kusini) alichukua nafasi ya Dusan Kondic raia wa Serbia pia ambaye pia alilazimika kushitaki Yanga TFF ili kulipwa fedha za mshahara wake. Kondic alisema alilipwa dola 18,000 badala ya zaidi ya dola 30,000 alizokuwa akidai.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,934
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  Kocha halipwi mshahara, halafu mnategemea makubwa, utumbo mtupu
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 17,554
  Likes Received: 5,121
  Trophy Points: 280
  Wenzio twalia ndizi................:rolleyes:
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,835
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  Manji wao yu wapi?
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Tatizo la Yanga nilionavyo mimi ni ile Tabia yakumtegemea Manji nje ya Mkataba, sasa Bwana Manji akiona hajalambwa miguu unaona anaondoa Pesa yake kwenye Mishahara ya wachezaji, akilambwa miguu na vile vizee kina Mlimba sijui anatamka kua ataendelea, huyu anawayumbisha, huyu aliingia Yanga kutafuta kuungwa mkono na UMMA, ili Umma ukapate kumuhurunia.
  hakuingia kuifadhili YANGA kwa mapenzi yake, ila kwa AGENDA ya kificho .
   
 6. bona

  bona JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,794
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  kwa wale msiojua uyo manji aliingia ktk michezo gafla baada ya makashfa ya ufisadi, wizi na dhuruma (quality group mauziano na nssf, kuuziwa open space kwa kuimega kibasila etc) kumuandama sasa akaona njia ya kuficha aya ni kukimbilia kwenye kitu kinachogusa watu wengi nao ni mpira na kujifanya kuidhamini yanga ili asiandamwe hata jinsi alivyokua akitoa ela utaona kua alikua anazimwaga kama kaziokota!
  maendeleo ya mpira yanaletwa tu kwa club kua kampuni sasa uongozi wa yanga wa sasa umerudisha yaleyale ya kutembeza bakuli, kina george mpondella walileta mabadiliko ya kweli lkn sasa tumerudi nyuma!
  uyu kocha ni makini nashauri tumpe taifa stars atatufikisha mbali!
   
 7. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hii janga na nyenzake jote ni jingajinga tuu,hata hiyo Papic yao pia jingajinga,meona menzake ule kondic bado nalipwa pesa jake,yeye nazidi ng'ang'ania janga,janga-janga,janga,janga kitu gani banaaa,joo huku fudisha sisi kricket napate pesa jingi jingi,achana na hiyo janga yako!!
   
 8. K

  Konaball JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 2,124
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  mie siwezi kumlaumu Manji ila nitaulaumu uongozi wa Yanga, miaka 3 waliyofadhiliwa na Manji wao wamejibweteka tu hawakuwa na mpango wowote wa kujitegemea!! Natoa mifano hii

  1-Viongozi wa Yanga waeleeze mapato yote ya miaka 3 wakiwa chini ya Manji?

  2-Viongozi waeleze usajili wa msimu huu wametumia kiasi gani na wamesajili wachezaji gani?

  3-Waweke wazi mktaba wao na Quality Plaza na wa TBL unainufaisha vipi CLUB?
   
 9. M

  Magehema JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 449
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili si tatizo la Yanga ni tatizo la kitaifa, tunaishi kwa kutegemea wafadhili kwa kila kitu hata kuwaza tumewaachia hao wawaze kwa niaba yetu!!!!!!
   
 10. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 930
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 45
  tatizo kubwa hapa ni vilabu vyetu kuendeshwa kienyeji, mambo ya kutegemea kila kitu, wahusika wamejiachia tu hawataki hata kuumiza kichwa na kuweka mipango mbalimbali ya maendeleo. Hata hii timu ya taifa, wakijitoa wadhamini tu utaona jinsi hao TFF watakavyohaha coz bado hawajaweka mikakati imara ya kujitegemea.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...