Sofia Simba azua mtafaruku mwingine UWT, amkataa katibu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sofia Simba azua mtafaruku mwingine UWT, amkataa katibu wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Nov 21, 2009.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba ambaye alilipua mabomu yaliyochafua hali ya hewa kwenye kikao cha Kamati ya Mwinyi na wabunge, sasa amehamishia makombora hayo ndani ya jumuiya yake.

  Mama Simba sasa hamtaki katibu mkuu wake wa UWT ambaye ndio kwanza ameanza kazi, Mwananchi imebaini.

  Taarifa ambazo Mwananchi umezikusanya kwa wiki nzima zinasema kuwa Mama Simba haelewani na katibu wake, Husna Mwilima ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo katikati ya mwaka huu akitokea Hai mkoani Kilimanjaro ambako alikuwa mkuu wa wilaya.

  UWT, ambayo uchaguzi wake ulitanguliwa na mtafaruku mkubwa baina ya Simba na mpinzani wake kwenye nafasi ya mwenyekiti, Janneth Kahama, ilianza mkutano wa baraza kuu la wanawake tangu jana na habari zinasema hali ya kutokuelewana kwa viongozi hao wawili ndiyo iliyotawala maandalizi na kusababisha baadhi ya viongozi wa CCM kuingilie kati.

  Hali hiyo ya msuguano ilithibitika jana wakati mpasuko ulipojionyesha na kusababisha wengi wa wajumbe kuonyesha tofauti kubwa na viongozi hao.

  Baada ya kuanza kwa kikao hicho cha baraza ambacho kilikwenda sambamba na mafunzo kwa viongozi hao, kulizuka hali ya kutokuelewana baina Simba na Mwilima, ambaye baadaye alipatwa na shinikizo la damu na hivyo kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

  Alipoulizwa kuhusu ugonjwa wa katibu huyo wa UWT, mganga mkuu wa mkoa, Godfrey Mtey alisema kuwa hayupo mkoani Dodoma na akataka mwandishi awasiliane na kaimu wake, Jacob Chembele.

  Hata hivyo, katibu huyo ambaye wauguzi waliiambia Mwananchi kuwa alilazwa wodi 18, aliruhusiwa kutoka hospitalini.

  Husna Mwilima aliteuliwa hivi karibuni na vikao vya juu vya CCM kwa ajili ya kushika nafasi hiyo akitokea wilaya ya Hai.

  Vyanzo kutoka ndani ya mkutano huo viliidokeza Mwananchi kuwa Simba na Mwilima wamekuwa na mgogoro wa chini chini na hadi sasa wameifanya jumuiya hiyo kumeguka vipande viwili kutokana na baadhi kumuunga mkono Mwilima na wengine wakiwa upande wa Simba.

  "Sisi tumekuwa tukiwashangaa sana viongozi wetu, yaani huyu Mwilima kaingia juzi tu katika jumuiya na Simba naye bado ni mgeni katika nafasi aliyonayo, lakini wameanza kutupiana lawama kwa madai kuwa mmoja wao amefuja pesa za jumuiya, jamani hii ni aibu kubwa," alisema mmoja wa wajumbe kutoka moja ya mikoa ya Kaskazini.

  Mjumbe huyo alisema kuwa tatizo linaloikabili jumuiya hiyo ni hali ya mitazamo ya viongozi wa juu katika jumuiya hiyo na akasema hivi sasa kumekuwa na matabaka ndani ya uongozi.

  Kwa upande wake mmoja wa wabunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya Magharibi alilidokeza Mwananchi kuwa si kweli kwamba Mwilima alikuwa amefuja pesa za chama, bali kilichofanyika ni kuwa mwenyekiti amekuwa hampendi tangu mwanzo kutokana na misimamo yake.

  "Unajua tufike wakati lazima tuseme ukweli... huyu binti wa watu hana makuu kabisa, lakini tatizo limekuwa ni sisi maana akivaa vizuri, tunasema kuwa anajipenda, akibadili nguo tunasema kuwa anaiba hela... ah, ili mradi kumtwisha maneno mtoto wa watu bila hata sababu za msingi," alisema.

  Habari zinasema katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba na mwanansiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru waliingilia kati ili kunusuru balaa hilo na kufuta aibu ya jumuiya hiyo ambayo ni tegemeo kwa CCM.

  Hata hivyo, pamoja na kasoro hizo, UWT ilipitisha katiba yake.

  Simba amekuwa akitamba kwenye vyombo vya habari tangu alipotofautiana na Kahama katika kikao cha wanawake cha mkoa wa Dar es salaam.

  Lakini, katika siku za karibuni amekuwa akiandikwa zaidi baada ya kutoa maneno makali kwenye kikao cha Kamati ya Mwinyi na wabunge baada ya kuripotiwa akimtetea waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa ni mwanamume wa shoka ambaye alijipatia utajiri zamani na kueleza kuwa tuhuma za kashfa ya Richmond dhidi yake ni za uongo.

  Pia alimsafisha mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge dhidi ya kashfa ya ununuzi wa rada.

  Kama haitoshi, Simba, ambaye anaongoza wizara inayohusika na utawala bora, alimrushia kombora mwenyekiti na waziri mkuu wa zamani, John Malecela kuwa alipewa hela za kifisadi wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

  Alimrushia pia kombora Malecela na mkewe, Anne Killango kuwa harusi yao ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel, huku akiwaelezea wabunge wanaojinadi kuwa wanapambana na ufisadi kuwa wanasumbuliwa na njaa.

  Wote hawakujibu tuhuma zake, na badala yake Malecela alisema waziri huyo ni mgonjwa wa akili na akamshauri apitie hospitali ya wagonjwa wa akili ya Mirembe kabla ya kurudi jijini Dar es salaam.

  Kama ni kweli, aliyemloga huyu mama ni kichaa
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,598
  Trophy Points: 280
  Hilo ni zao la mafisadi.....na matunda ya kubebwa.....mbumbumbu limbukeni kapewa mpini....tutakoma....ila ajiandae kushitakiwa muda wao ukipita.....makamba,el,ra,jk,chenge,nchimbi.....jiandaeni muda waja...
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Malechela anasema kwamba huyo mama apitie Dodoma Milembe kwenye wagonjwa wa akili, ili wakamcheki kama yupo poa upstair kweli ni kaazi CCM
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  washtakiwe kwa kosa gani?unadhani watu wanastakiwa kwa maneno matupu ya hapa JF..forget about it
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa mtaji huu, hakuna atakayewachukua sirias.

  Amandla........
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  masikini wee Sofia Simba!!!!! unalipeleka wapi taifa na Chama chako.


  Hebu wajameni naomba CV ya huyu mama labda inawezekana kiatu alichopewa ni kikubwa kuliko mguu wake.
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  CV haisaidii kitu. Busara hauwezi kuitambua kwenye CV.

  Amandla.......
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  lazima atamsumbua sana Jk huyu, maana haaminiki, havumiliki, wala hachanganyiki na watu, kwani CV yake ni ipi, maana namashaka kidogo na uelewa wake, siku zote huyu mwanamama amekua chanzo cha matatizo, mimi nadhani hana hadhi hata yakuongoza kata sembuse ubunge na uwaziri, Kikwete anawatoa wapi hawa mawaziri wake, anateua kama wanakamati wa kuongoza vikao vya maandalizi ya harusi, mimi sielewi kabisa.
  ila lawama zote anabeba Jk maana yeye ndie aliempa kichwa kwa kutomkemea tangu wakati ule anajipakazia kua ktumwa na Rais kugombea UWT.
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Neno "educated fools" halikutungwa bila sababu. Kutegemea mno CV kumechangia sana kutufikisha hapa tulipo.

  Amandla......
   
 10. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani wa kumsumbua JK???!!!! JK hasumbuki na lolote wala yeyote,mtu asiye serious katika mambo ya muhimu atashughulishwa vipi na mcharuko wa Sofia Simba?
  Hapa hakuna raisi wala wateule wake ambaye anaitakia mema nchi hii.Huu ujasiri wa kifisadi wa kumtetea Lowassa na Chenge hauji hivihivi bali kuna nguvu kubwa nje ya taratibu za kiuongozi zinazomtia kiburi huyu mama,
  si ajabu ni fundi mzuri sana wa kukata viuno haswa pale anapoona kuna faida ya binafsi kwa kufanya hivyo
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  i can agree with you, no comment.
   
 12. b

  ba mdogo Member

  #12
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua huwa kuna kipindi nashindwa hata kuamini kama haya ayatendayo huwa anakuwa mzima au ni ilevi wa madaraka? Nasikia ni mwanasheria ila sijui alisomea wapi sheria. Na kama kweli ni mwana sheria mbona ayafanyayo hayaendani na taaluma hiyo ambayo mimi naiheshimu sana? yawezekana hata katika vyeti vyake kuna utata. ila hebu tusu biri vumbi la uchaguzi mwakani maana zipo taarifa kuwa anatia timu katika jimbo la kisarawe. Ee Mungu tusaidie maana tunapita katika kipindi kigumu.
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Shitaki shitaki tunayoiona ni maendelezo ya usanii tu. Labda kipindi cha CHADEMA kuongoza Serikali na Dr. Slaa akiwa Rais ndipo tutaona hiyo orodha uliyoitaja ikifikishwa mahakamani na si katika kipindi hiki cha JK.
   
Loading...