Sofia Simba amtosa Hasna Mwilima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sofia Simba amtosa Hasna Mwilima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Marigwe, Feb 22, 2010.

 1. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kuna minon'gono nimeisikia lakini sijaithibitisha kuwa Mwenyekiti wa UWT Mheshimiwa Sophia Simba kamtosa HASNA MWILIMA na si Katibu Mkuu tena wa UWT. Mwenye kujua atujuze.
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  hongera sophia simba kwa ujasiri. katibu mkuu akilegalega aondoke, hakuna haja ya kusubiri sijui hadi uchaguzi mwingine. huyu simba ni mama wa shoka, ni mwepesi wa kuchukua hatua. nimempenda sana kwa ujasiri wake huu kama habari hizi ni za kweli.

  kulindana ndio kumetufikisha hapa. hii ni salamu maalum kwa JK asiendeleee kumkumbatia makamba wakati chama kinasambaratika. hongera simba,umedhihirisha kuwa wewe ni simba halisi. nakuombea udumu hapa na baada ya JK ulambe fomu ya magogoni...................... big up mamamaaaaaaaaaaa.........
   
 3. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ndugu AKILI KICHWANI. Yamekuwa hayo tena!!!!!!!Nilitaka uthibitishe kuondolewa kwa Mwilima. Siyo kumsifia Simba. Jamani aaa
   
 4. b

  ba mdogo Member

  #4
  Feb 23, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua hata mimi nilitegemea atujuze. mara naona big up kwa sana. naungana na wewe hebu mwenye taarifa za ukahikika atujuze tunene tuliyo nayo
   
 5. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Akili Kichwani ndiyo Sofia Simba mwenyewe ....Hapa akili ndog sana inatakiwa kujua argument za mtu..
   
 6. K

  Konaball JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 2,128
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  kwani Katibu uondolewa na Mwanyekiti au na nani jamani mtujuze basi
   
 7. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu ni katibu wa kuchaguliwa au kuteuliwa? Je, kulikuwa na mkataba wa kazi? Nauliza kwa kuwa naona mambo yamefanyika kienyeji kama kweli tukio hili limetokea.
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Tetesi : Si kweli Katibu wa UWT-CCM hawezi kuondolewa kazini/kufukuzwa/kuachishwa kazi na Mwenyekiti wa UWT-CCM!

  Ni kweli ndani ya UWT-CCM mambo sio shwari - na hii ni tangia baada ya uchaguzi - Mama Kahama ana kambi yake na Sophia ana kambi yake - Husna yupo kambi ya Mama K and Co na The great Anna Abdallah yupo upande wa Sophia and Co. Tatizo kubwa ni la maslahi binafsi - Ikumbukwe kwamba pale penye mjengo wa Celtel aka Zain aka YYY tel ni eneo la UWT-CCM na kuna mambo mengi yameenda underground kuhusu hiyo project!

  Survival ya Husna ni ndogo, lakini will need a lot of courage kumwondosha pale UWT-CCM kikatiba.


  Mzee Sinde Warioba we need you badly on these trying times!
   
 9. M

  Mkufu Member

  #9
  Feb 23, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndio katoswa, si katibu mkuu tena wa U.W.T wajameni si mnakumbuka Baraza Kuu la U.W.T la Novemba lilimkataa? Hicho ndio kikao cha Mwisho chenye Mamlaka ya Ajira yake na anawajibika kwa Baraza Kuu.

  Hivyo Sophia anatekeleza maamuzi ya vikao, someni katiba ya U.W.T. inashangaza magazeti yaliandika eti hasna ameteuliwa na rais, hakuna kitu kama hicho,

  Huyu Hasna ana madudu mengi kayafanya pale U.W.T wala sio kwamba eti yupo kambi ya Mama Kahama ni KILAZA TU NA KAFISADI KADOGO
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nimesikia toka kwa Mbunge fulani..Hoja hapa ni je SS ana mamlaka ya kumfukuza uonmgozi Hasna kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji UWT-CCM?
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Feb 23, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 13,572
  Likes Received: 6,705
  Trophy Points: 280
  ..Sophia Simba pia alitoa mapendekezo kwamba Wabunge wa viti maalum wa CCM wasichaguliwe zaidi ya vipindi viwili.

  ..sasa CCM-NEC wamekubaliana na hoja hiyo lakini ili kuepusha shari wameagiza utekelezaji wake uanze mwaka 2015.
   
 12. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  simba ni bonge la kichwa sijapata uona................ big up mama.....................
  unaona vichwa maji wanachelewesha utekelezaji wa mawazo ya mama mpambanaji ss, sasa utekelezaji hadi 2015 wanaogopa nini??? mbona kumpiga chini husna mwilima hakusubiri 2015. nakwambia nchi hii ikipata akina ss 10 hivi, kufumba na kufumbua tutaipota japan kimaendeleo nawaapia.............................

  uharaka wa kuchukua hatua muhiu sana, sio usubiri mambo yaharibike ndo uanze kutoa visisngizio wakati ulikuwa na mamlaka ya kutosha!!!!!!!!!!!!!!!

  kila mtu leo anamlaumu JK kwa kuchelewa kuchukua hatua, sasa kwa nini tusimpongeze ss?????????????? acheni wivu, big up mamaaaaaaaaaaaaa........... 2015 nakuchukulia fomu za kuingia magogonu kwa hela zangu...................
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kutoka Tanzania Daima

  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba, amemsimamisha kazi Katibu wa jumuiya hiyo, Hasna Mwilima katika mazingira ya kutatanisha kwa madai kuwa ni maagizo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

  Waziri Simba ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa na mahusiano mabaya na katibu wake huyo, alifikia uamuzi huo mwishoni mwa wiki katika kikao cha Kamati ya Utekelezeaji ya UWT taifa, iliyokutana kwa dharura jijini Dar es Salaam.

  Katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kikao hicho kupitisha uamuzi wa kumsimamisha, wajumbe wanne walitumwa nyumbani kwa Hasna kupeleka barua wakati akiwa kitandani akijiuguza kutokana na homa iliyokuwa ikimsumbua.

  Mbali ya Waziri Simba, wajumbe wengine waliohudhuria kikao hicho na kuridhia uamuzi huo ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa UWT, Asha Bakari.

  Wengine ni Shamsa Mwangunga, Hawa Ghasia, Zainabu Mwamwindi, Furahia Abdallah, Fatuma Tawafiq, Lucy Mayenga, Lediana Mng’ong’o, Subira Mohamed na Zainabu Shomari.

  Habari kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa kikao hicho zilisema wakati wa kikao hicho, Hasna hakuhudhuria kwani alikuwa mgonjwa.

  “Kweli kikao kilifanyika na kuamua kumfukuza kazi Hasna na mwenyekiti alisema lilikuwa ni agizo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa CCM taifa,” alisema mmoja wa wajumbe hao.

  Kwa mujibu wa habari hizo, barua ya kusimamishwa kazi kwa Hasna ilipelekwa nyumbani kwake na wajumbe wanne ambao ni Asha Bakari, Zainabu Mwamwindi, Furahia Abdallah na Subira Mohammed.

  “Hata hivyo walipofika pale, Hasna alikataa kuisaini kwa madai kuwa kikao kilichokaa hakina mamlaka kisheria kumsimamisha kazi,” kilisema chanzo chetu cha habari.

  Habari zaidi zinasema kuwa mbali ya kumsimamisha kazi, kikao hicho pia kiliamua kumnyang’anya gari.

  Hata hivyo, Sofia Simba jana hakuwa tayari kupokea simu kila alipopigiwa na gazeti hili, badala yake simu hiyo kwa zaidi ya mara sita ilikuwa ikipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake na kudai kwamba yuko mbali na waziri huyo.

  Mzozo kati ya Waziri Simba na katibu wake uliongezeka wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la UWT ambapo aliwaambia wajumbe hao hamtaki katibu huyo ambaye hajafikisha hata mwaka mmoja tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo akitokea wilayani Hai, alikokuwa mkuu wa wilaya. Hali hiyo ilisababisha Hasna apate shinikizo la damu na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, huku wajumbe wakigawanyika.
   
 14. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  safi sana SS,...................................... uuuuuuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii........................... nipe raha mama................... huo ndio uongozi......................SS for presidency 2015!!!!!!
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Feb 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  hii ni post yangu ya 1000.
  ni hivi Sophia Simba anacho kiburi apatacho kutoka kwa Rais, ama alijuana na Rais nje ya mfumo wa utawala ama anajua na rais kifamilia ama kuna mahusiano fulani nje ya kazi yanamtia kiburi huyu mama.
  Maana sikudhani mpaka leo angekua sehemu ya chama ama serikali kimamlaka.
  akiwa mteule wa ofisi ya Rais na mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa CCM Tanzania, amefanya mambo mengi ya kihuni kuliko ilivyowahi kutokea tangu Uhuru.
  kweli binafsi huyu mama ananikera, ananiboa, bahati nzuri mimi si mwana CCM , lakini kwasababu akili yake haijatulia nashangaa kuachwa kwenye mamlaka ya Taifa hili hadi leo.
  halafu anapenda sana kutumia neno la Raisi kanituma, Rais ameniagiza, hili lina baraka.....sikupendi Sofia.
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  uhuni gani kafanya na wewe????????????// hebu acha maneno maneno maneno.................... tena ya vijiweni................watendaji wakiboronga mnakuwa wa kwanza kutaka wawajibishwe, wakiwajibishwa manakuwa wa kwanza kuwalilia!!!!!!!!!! tuwaeleweje waTZ!!!!!!!!!!!!!!!

  kuna mfano mwingine wa uongozi tunaotaka zaidi ya huu......................... you are not serious men.........................

  mi namzimikia huyu mama kinoma.......................
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Feb 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  haa kumbe unamzimia, kipenda roho.
  huyu mcheza taarab huwezi kuona madhaifu yake kwa sababu ya huba lako juu yake, huyu mama ni mama mipasho tu, uongozi sifuri,
   
 18. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Heeeee! yeye kaboronga mara ngapi lakini hajatimuliwa? Kiboko yake Kilango.
   
 19. K

  Kristin Member

  #19
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  naomba nifahamishe huyu Husna Mwilima kaboronga kitu gani mpaka atimuliwe.
   
 20. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,670
  Likes Received: 858
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu kwa husna kwa kuwa ana elimu asing'ang'anie kwenye vyeo vya kisiasa kwani anaweza kuishia kuugua magonjwa yasiyoendana na umri wake kama hizo presha n.k. Aingie kwenye asasi za kiraia
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...