Soda Ash...a curse or blessing?

justice-lover

Member
Jan 11, 2008
15
2
Naomba kuuliza wataalamu wa uchumi, wanieleze faida zitakazo toka kwenye kiwanda cha magadi kinachopendekezwa eneo la Ziwa Natron. Mkataba utakuwa kati ya kampuni ya Tata Chemicals ya India na Lake Natron Resources (TZ) Limited.

Baada ya wataalamu wetu "halafu cha ajabu walikuwa ni wazungu watupu sasa sijui...anyway..." walioanguka na helikopta ya jeshi wanaosadikiwa kuwa walikwenda kusurvey hilo eneo. Hawa watu wameona wamemaliza sehemu zote za madini wakaona waende kwenye mali asili chache tulizobakiwa nazo? Hayo madini yote tunayochimba yametusaidia nini? Ni watanzania wangapi wamenufaika na Tanzanite mpaka hivi sasa? Acha watu wachache waliodraft mikataba kwa mamilioni ya fedha na kupata ajira. ni wachache sana.

Mi ningeomba tujaribu kutunza japo sehemu ndogo tu ya maliasili zetu kwa ajili yetu na vizazi vijavyo.

Ndege "flamingos" wanaozaliana hapo wanatuletea watalii wengi kiasi cha kutuingizia fedha za kigeni. Sasa mkishaharibu mazalia yao hao ndege wataangamia na kwa kweli watalii hawaji kote huku kuangalia ziwa tupu. Wataalamu wanatuambia kuwa wale ndege wakipata disturbance hata kidogo tu wanaacha mayai yao na kuyatelekeze na hivyo kizazi chote kitaangamia. Ikimbukwe pia hawa ndege waliwahi kukumbwa na ugonjwa kiasi cha kupotea kwa wingi ni sasa tu ambapo idadi yao inaanza kutengemaa.

Tujaribu kutumia akili saa nyingine. Na hao LEAT (Lawyers' Enviromental Action Team) wanafanya kazi gani?[/FONT]
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom