Snowden asema lengo lake limekamilika

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,280
2,000
Mfanyakazi wa zamani wa muda katika Shirika la Usalama la Marekani, NSA, Edward Snowden, ambaye alifichua kuwepo kwa mipango ya Marekani kufuatilia taarifa za mawasiliano ya watu, amesema amefaniskisha lengo lake.
"Kwa kuridhika binafsi, mpango wangu tayari umefanikiwa," ameliambia gazeti la Washington Post.
Taarifa zinazohusiana
Marekani, Latest
"Tayari nimeshinda," amesema Bwana Snowden, ambaye ufichuaji wake mkubwa umesababisha Marekani kuangalia upya sera yake ya ufuatiliaji wa taarifa za siri za watu na mashirika.
Snowden mwenye umri wa miaka 30, alifanya mahojiano na gazeti hilo nchini Urusi, ambako alipewa hifadhi ya ukimbizi wa muda tarehe Mosi Agosti.
Bwana Snowden aliondoka Marekani mwishoni mwa mwezi Mei, akichukua kiasi kikubwa cha nyaraka za siri kuhusu mpango wa udukuzi wa Marekani.
Anakabiliwa na mashitaka ya ujasusi nchini Marekani.
NSA iligundulika kuhusika katika udukuzi wa data za simu. Taarifa za kina za watu na taasisi zilizolengwa na udukuzi wa mashirika ya ujasusi ya Uingereza na Marekani zilichapishwa wiki iliyopita na magazeti ya The Guardian, The New York Times na Der Spiegel.
Magazeti hayo yamesema orodha ya watu na taasisi zipatazo 1,000 zilizolengwa ni pamoja na Kamishna wa Umoja wa Ulaya, mashirika ya kibinadamu na maafisa wa Israel akiwemo waziri mkuu.
Makampuni makubwa ya teknolojia ya mawasiliano nchini Marekani ya Google, Microsoft na Yahoo yanachukua hatua ya kuzuia ukusanyaji wa data unaofanywa na serikali yao.
Mwezi Oktoba, habari ziliposambaa kuwa NSA lilikuwa limedukua mazungumzo ya simu ya kiongozi wa Ujerumani Chansela Angela Merkel, kulisababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya Ujerumani na Marekani.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff naye pia alikasirishwa na taarifa kwamba shirika la ujasusi la Marekani, NSA, liliingilia mtandao wa kompyuta wa kampuni ya mafuta ya serikali ya Brazil, Petrobras ili kukusanya taarifa na mawasiliano ya barua pepe na simu.
 
time theory

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
767
1,000
Ngoma ya wakubwa hiyo,tuwaache wacheze wenyewe.kama kuna ya kujifunza tuchukue hakuna tubaki watazamaji.
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,496
2,000
Wewe mwache adunde dunde kama Kitenesi mwishoni kitatulia tuu. Amuulize mwenzake Robert Phillip Hansen,jina la Kijasusi Bob Hansen yupo wapi sasa hivi ambae alikuwa Agent wa F.B.I huku akiwa double Agent wa K.G.B kwa miaka 20.
 
kaka km

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
1,309
2,000
mwisho wa siku wale jamaa watamuufosaro,wabaya sana,wako tayari kumuua hata rais wao kama ataenda kinyume na maslah ya nch yao sembuse bwana snowden,sion future yake.
 
mwahaja

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
387
225
Jamaa yupo juu sn kwa teknolojia huyu,but awe makini sn mbna hawa wajomba.
 
Morinyo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
2,782
2,000
Wewe mwache adunde dunde kama Kitenesi mwishoni kitatulia tuu. Amuulize mwenzake Robert Phillip Hansen,jina la Kijasusi Bob Hansen yupo wapi sasa hivi ambae alikuwa Agent wa F.B.I huku akiwa double Agent wa K.G.B kwa miaka 20.

Baba wa Taifa kipindi kile Mrema anabebwa alisema hivi " Kama anapenda kubebwa bebwa kama maiti muacheni tu, itafikia wakati wanaobeba watachoka na anaebebwa nae atachoka"
 
2013

JF-Expert Member
Jan 1, 2013
11,331
2,000
snowden ni psychopath asiye na vision kabisa, kwakuwa amejikuta anaondoa uzalendo kwa taifa lake la marekani, huyu ni gaidi tu.
laiti angekuwa sio mmarekani nisingemlaumu kabisa lakini ni raia wa taifa hilo kubwa duniani na leo amekuwa mkimbizi kama yaliyomkuta Osama kwa taifa lake la saudia arabia alipoligeuka. hivi najiuliza shida yake ilikuwa ninini mpaka akaona atoe siri ambazo zingeweza kuliingiza taifa lake kwenye vita kubwa duniani? hii ni aibu kwa raia waliokosa uzalendo kwa mataifa yao.
 
Ngapulila

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
766
1,000
Hii ni mbinu mpya ya USA kuuhadaa ulimwengu kwa kutangaza kuwa Snowden katoroka na taarifa japokuwa ni kweli.Lengo la USA ni kufanya ujasusi kwa kila nchi Snowden amepita.Their primary goal has been achieved.Jiulize swali hili "Ni kweli kuwa USA walshindwa kumpata Swonden mapema alipotoroka ?
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,473
2,000
Mfanyakazi wa zamani wa muda katika Shirika la Usalama la Marekani, NSA, Edward Snowden, ambaye alifichua kuwepo kwa mipango ya Marekani kufuatilia taarifa za mawasiliano ya watu, amesema amefaniskisha lengo lake.
"Kwa kuridhika binafsi, mpango wangu tayari umefanikiwa," ameliambia gazeti la Washington Post.
Taarifa zinazohusiana
Marekani, Latest
"Tayari nimeshinda," amesema Bwana Snowden, ambaye ufichuaji wake mkubwa umesababisha Marekani kuangalia upya sera yake ya ufuatiliaji wa taarifa za siri za watu na mashirika.
Snowden mwenye umri wa miaka 30, alifanya mahojiano na gazeti hilo nchini Urusi, ambako alipewa hifadhi ya ukimbizi wa muda tarehe Mosi Agosti.
Bwana Snowden aliondoka Marekani mwishoni mwa mwezi Mei, akichukua kiasi kikubwa cha nyaraka za siri kuhusu mpango wa udukuzi wa Marekani.
Anakabiliwa na mashitaka ya ujasusi nchini Marekani.
NSA iligundulika kuhusika katika udukuzi wa data za simu. Taarifa za kina za watu na taasisi zilizolengwa na udukuzi wa mashirika ya ujasusi ya Uingereza na Marekani zilichapishwa wiki iliyopita na magazeti ya The Guardian, The New York Times na Der Spiegel.
Magazeti hayo yamesema orodha ya watu na taasisi zipatazo 1,000 zilizolengwa ni pamoja na Kamishna wa Umoja wa Ulaya, mashirika ya kibinadamu na maafisa wa Israel akiwemo waziri mkuu.
Makampuni makubwa ya teknolojia ya mawasiliano nchini Marekani ya Google, Microsoft na Yahoo yanachukua hatua ya kuzuia ukusanyaji wa data unaofanywa na serikali yao.
Mwezi Oktoba, habari ziliposambaa kuwa NSA lilikuwa limedukua mazungumzo ya simu ya kiongozi wa Ujerumani Chansela Angela Merkel, kulisababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya Ujerumani na Marekani.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff naye pia alikasirishwa na taarifa kwamba shirika la ujasusi la Marekani, NSA, liliingilia mtandao wa kompyuta wa kampuni ya mafuta ya serikali ya Brazil, Petrobras ili kukusanya taarifa na mawasiliano ya barua pepe na simu.
Hakuna alichopata nani wa Kumchukia Mmarekani? Obama alikuja Tanzania akaachiwa Idara zote za Usalama aziendeshe mwenyewe.... huo ujinga wa Kiongozi wa Ujerumani anasikilizwa simu zake haileti mantiki yeyote hapo ujerumani haitaweza kujiondosha kwa mmarekani kisa kiongozi wao Dunia ya Sasa cha maana ni Maslai.... ukipoteza maslai uchumi wako utadoda na wananchi watakukataa.... kansela hatoweza kujiondoa kwa Mmarekani Snowden kafanya kazi ya bure.... Watizame Brazil mafuriko yale lazima wapige hodi marekani... si ulimuona Raisi wa Brazil alipokuwa anambusu Obama kwenye Msiba wa Mandela?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom