SMZ yaifunga mdomo UAMSHO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ yaifunga mdomo UAMSHO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ground Zero, May 3, 2012.

 1. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali ya Zanzibar imevitaka vikundi vyote vinavyotoa mihadhara juu ya katiba na muungano kuacha mara moja kuruhusu tume ya katiba ifanye kazi yake.

  Source: ITV
   
 2. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nimeona...bwa ha ha ha ha ...!nasubiri comment ya mpemba mbishi,takashi nk.
   
 3. d

  dandabo JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Serikali ilitakiwa kutoa marufuku hii mapema sana!
   
 4. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  kama sumu ishasambaa...wamechelewa mno...
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hii si haki kabisa kuwazuia watu wasijadili jambo linalohusu maisha yao kwa uhuru. Kwa taarifa ya SMZ na wanaCCM wenzao kuzuia watu wasijadili muungano wanaoutaka inawaaminisha wananchi kuwa muungano huu ni sawa na ukoloni. Sisi watanganyika tulilazimishwa kuungana na wazanzibar. Je kutoa maoni kupitia JF unakwepa mkono wa sheria hii?
   
 6. k

  karafuu Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatusimami hadi kieleweke mbona wanavuta shuka jua lishachomoza.
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Sio mara ya kwanza kusema kauli hizo.

  Wazanzibar hawataweza kamwe kuburuzwa this time, Never..........

  Huyo mohamed abood aliyetoa tamko hilo ni wale wale watumwa wa kifikra.

  Hii ni haki yetu na kamwe hakuna mtu anayeweza kuizuia
   
 8. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Yaleyaleee..
  Hawana tofauti na viongozi wa bara
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Sioni mantiki ya kucheka hapa, kama hukubaliani na uamsho si lazima ushindwe kufikiria beyond uamsho. Hili suala la katiba mpya linahitaji mdajala mpana sana. Leo wameanza na uamsho unachekelea kesho wakiwapiga marufuku CDM au wakiwakataza kina Pengo kuongelea sidhani kama tutapata katiba bora. Ni matarajio yangu kuwa Uamsho wataupuuzia wito huu wa SMZ
   
 10. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mnafiki na kibaraka huna lolote zaidi ya undumila kuwili. Tundu Lissu alipoongelea hii sheria kandamizi ulikuwa ni mmoja wa wabezaji kisa tu unajikomba kwa magamba.
  Angalizo: Wazanzibari wenye uchungu na nchi yao pekee ndio waipiganie nchi yao, vibaraka na mapndikizi kama Tume ya Katiba ni hatari kwa mustakabari wa Zanzibar na Tanganyika huru
   
 11. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  binafsi napenda huu muungano uangaliwe upya ila staili ya ubaguzi na lugha chafu kwa wabara/nyerere waliyokuwa wanatumia hawa jamaa wa uamsho kwa kweli sikuipenda...nimecheka kwa sababu walikuwa wanasema sasa wameungana pamoja na wote nia yao ni kuuvunja muungano lakini hii kauli mpya imewaweka njia panda...!
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..waachwe tu watoe maoni yao, as long as hawamdhuru mtu yeyote, au kuharibu mali za watu.

  ..wa-znz wapewe madaraka kamili ya kuendesha nchi yao.

  ..serikali ikiwanyima hilo ni kujitafutia matatizo tu.
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  walikuwa wanasubiri nini siku zote hizo?
   
 14. m

  mzaire JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya ndio majibu kutoka kwa UAMSHO na JUMIKI dhidi ya SMZ kupitia kwa Waziri Mohammed Aboud na leo hii wamefanya mhadhara mjini Unguja na kesho watakuwa Maisara.


  Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI  Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.
  TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR.
  KWA VYOMBO VYA HABARI BAADA YA KAULI YA MHE. MOHAMED ABOUD YENYE NIA YA KUVUNJA NA KUVURUGA AMANI YA NCHI ILIYOTOKA JANA TAREHE 2/5/2012 ZBC.
  03/05/2012

  NDUGU WAANDISHI WA HABARI
  ASSALAMA ALAYKUM WARAHMATU -LLAH WABARAKATU

  Awali nachukua fursa hii kumshukuru Allah subhana wataala muumba mbingu na ardhi mwenye kumpa Ufalme amtakae na kumnyima amtakae pia tunamtakia rehma kipenzi cha umma Mtume wetu Muhammada (S.A.W) baada ya shukurani hizo tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Rais wetu mpenzi Dr. Ali Mohammed Shein kwa uongozi wake imara uliojaa uadilifu, hekima pamoja na serikali yetu ya Kitaifa na usimamizi wake madhubuti wa kuhakikisha anatandika zulia la demokrasia na kuhubiri amani, umoja na mshikamano.

  Ndugu waandishi wa habari.
  Kwa kweli tumesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Mohammed Aboud aliyoitoa jana kwenye vyombo vya habari yenye lengo la kuzuia mihadhara inayoendeshwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa kusimamiwa na Jumuiya ya Uamsho JUMIKI kwa kisingizio cha sheria No. 8 ya mabadiliko ya Katiba kwa maana hiyo tunapenda tutoe ufafanuzi juu ya sheria hiyo katika ibara zake zinazohusu suala la utoaji elimu. Ibara ya 17:8 “Mtu au asasi yoyote itakayotaka kuendesha programu ya kutoa elimu juu ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, kabla ya kuanza kutoa elimu hiyo sharti, iwe imesajiliwa ……… na itawajibika kueleza kwa tume chanzo cha fedha ya kuendesha programu hiyo” ibara ya 21:2C “Mtu yeyote atakaeendesha programu ya elimu… kinyume na masharti ya sheria hii atakuwa ametenda kosa”

  Ndugu waandishi wa habari
  Napenda mzingatie kuwa:
  1. programu ya elimu inayomtia mtu hatiani kwa mujibu wa sheria hiyo ni elimu inayohusu sheria ya mabadiliko ya Katiba.
  2. Masharti yaliyoekwa ni kuwa Jumuiya imesajiliwa Serikalini.
  3. Inalazimika kutoa taarifa tu na kueleza chanzo cha fedha sio kutaka ruhusa au kuomba kibali.
  Kwa bahati nzuri Jumuiya za Kiislamu imeliona hilo mapema na tayari
  programu za elimu juu ya mabadiliko ya Katiba zimemaliza kwa muda
  mrefu kwa sasa hivi Jumuiya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuweza
  kujua sheria za nchi na Katiba yao jambo ambalo kwa muda mrefu Serikali
  haikuwa na utaratibu endelevu wa kuelimisha raia zake na hiyo ndio kazi
  inayoifanya Jumuiya kuisaidia Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa sambamba
  na kutoa elimu ya Kiislamu kufunza maadili mema, kudumisha amani,
  umoja, utulivu na mshikamano kwa wazanzibari wote bila kujali tofauti zao
  za kidini, kisiasa, rangi na ukabila pamoja na kusisitiza umuhimu wa kudai haki zao na uhuru wa maoni pamoja na kulinda mali ya umma na kutii Katiba ya Zanzibar na sheria za nchi. Ibara ya 23:1 ya Katiba ya Zanzíbar inasema “kila mtu anawajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Zanzíbar” 23:3 inasema “watu wotewote watatakiwa na sheria kulinda vizuri mali ya Zanzíbar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu… kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya badea ya Taifa lao”.

  Ndugu waandishi wa habari.
  Jumuiya ya Uamsho inaendesha mihadhara kwa miaka mingi kuzingatia Katiba yake pamoja na kufuata Katiba ya Zanzíbar inayotoa uhuru wa maoni kutipia ibara ya 18 inayosema “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yupo huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”.
  Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.

  Jumuiya za Kiislamu zinawatahadharisha watu hao na kuwataka mara moja waache kuhubiri uchochezi na uvunjifu wa amani na kuwakumbusha kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria ibara ya 12 ya Katiba inasema “ Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote” vile vile wajue hizi ni zama za uwazi haki na sheria hivyo tunawasihi wasijisahau wakavitumia vyeo na ngazi za uongozi kwa maslahi ya wachache sana wasioitakia mema Zanzíbar watambue kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Zanzíbar na sheria za nchi rejea ibara ya 14,16,23 ya Katiba ya Zanzíbar.

  Pia Jumuiya zinapenda kuchukua fursa hii kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 17:8 na 21:2C kwa kuzingatia uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar. Pia kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 10 cha Sheria hiyo hiyo No.8 ya mabadiliko ya Katiba kinachoipa Tume uhuru na mamlaka kamili ambayo Mhe. Mohamed Aboud anaonekana kuvikiuka na kuingilia kazi za tume kwani Katibu Mkuu wa Tume hakuwa na taarifa yoyote wakati Jumuiya zinawasiliana nae akiwa bado ndio kwanza anataka kuisoma taarifa hiyo kwenye mtandao.
  Imani yetu huu ndio Mwanzo wa uvunjifu wa sheria hiyo. Tunapenda kumkumbusha Mhe. Mohamed Aboud maneno ya Rais Dr. Shein aliwataka wananchi wa Zanzíbar wanaishi kwa umoja na mshikamano inapaswa hitilafu ziondolewe ili Wazanzibar waishi vizuri kwa amani na utulivu na kamwe asitokee mtu akiwa ana lengo la kuivunja amani iliyopo rejea gazeti la Zanzíbar leo lenye kichwa cha maneno TUSICHAFUE AMANI toleo No 3743.

  Ndugu waandishi wa habari .
  Tunapenda kumalizia taarifa hii kwa kutoa shukurani zetu za dhati kwa jeshi la polisi kusimama imara katika kudumisha amani ya nchi na kutokubali kuburuzwa na hao wachache wasioitakia mema nchi yetu ya Zanzíbar.
  Ahsanteni sana.

  Nakla:
  Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
  Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar,
  Waziri wa Katiba,
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais,
  Jeshi la Polisi,
  Idara ya Mufti Zanzibar ,
   
 15. m

  mzaire JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi hilo lisikuweke njia panda wala sio la kucheka kaka, katika watu wengi kuna mengi, pia kuna Mzanzibari wachahe wanaupenda muungano akina Seif Idd, Mohamed Abud, Shamhuni, Samia Suluhu, Shamsi Vuai etc, lakini wengi wao hawaupendi.

  Na hio kauli ya Waziri Mohamed Abud haina uzito wowote kwa Wazenji kwani tayari UAMSHO wameonana na Dr. Shein leo hii na wame pewa ruhusa kama kawa, hiyo kauli yenyewe sio ya SMZ ila ni ya hao vibaraka wetu huko Zenji.
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya nchi jirani hayanihusu, nawatakia mjadala mwema.
   
 17. M

  Mahembe Kuimyola Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wawaache watu watoe mawazo yao kwani wameshaona muungano wa aina ya sasa hauna tija kwa pande zote mbili
   
 18. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wanawaogopa wazanzibari...ingekua chadema ndio wameitisha hii mikutano ungekuta wako polisi siku nyingi sana
   
 19. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani eee chonde chonde smz wapeni uhuru hao watu wajadili nini wanacho taka .
   
 20. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1]Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI[/h]Posted on May 3, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]
  Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 "Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi" kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.  TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR.
  KWA VYOMBO VYA HABARI BAADA YA KAULI YA MHE. MOHAMED ABOUD YENYE NIA YA KUVUNJA NA KUVURUGA AMANI YA NCHI ILIYOTOKA JANA TAREHE 2/5/2012 ZBC.
  03/05/2012

  NDUGU WAANDISHI WA HABARI
  ASSALAMA ALAYKUM WARAHMATU -LLAH WABARAKATU

  Awali nachukua fursa hii kumshukuru Allah subhana wataala muumba mbingu na ardhi mwenye kumpa Ufalme amtakae na kumnyima amtakae pia tunamtakia rehma kipenzi cha umma Mtume wetu Muhammada (S.A.W) baada ya shukurani hizo tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Rais wetu mpenzi Dr. Ali Mohammed Shein kwa uongozi wake imara uliojaa uadilifu, hekima pamoja na serikali yetu ya Kitaifa na usimamizi wake madhubuti wa kuhakikisha anatandika zulia la demokrasia na kuhubiri amani, umoja na mshikamano.

  Ndugu waandishi wa habari.
  Kwa kweli tumesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Mohammed Aboud aliyoitoa jana kwenye vyombo vya habari yenye lengo la kuzuia mihadhara inayoendeshwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa kusimamiwa na Jumuiya ya Uamsho JUMIKI kwa kisingizio cha sheria No. 8 ya mabadiliko ya Katiba kwa maana hiyo tunapenda tutoe ufafanuzi juu ya sheria hiyo katika ibara zake zinazohusu suala la utoaji elimu. Ibara ya 17:8 "Mtu au asasi yoyote itakayotaka kuendesha programu ya kutoa elimu juu ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, kabla ya kuanza kutoa elimu hiyo sharti, iwe imesajiliwa ……… na itawajibika kueleza kwa tume chanzo cha fedha ya kuendesha programu hiyo" ibara ya 21:2C "Mtu yeyote atakaeendesha programu ya elimu… kinyume na masharti ya sheria hii atakuwa ametenda kosa"

  Ndugu waandishi wa habari
  Napenda mzingatie kuwa:
  1. programu ya elimu inayomtia mtu hatiani kwa mujibu wa sheria hiyo ni elimu inayohusu sheria ya mabadiliko ya Katiba.
  2. Masharti yaliyoekwa ni kuwa Jumuiya imesajiliwa Serikalini.
  3. Inalazimika kutoa taarifa tu na kueleza chanzo cha fedha sio kutaka ruhusa au kuomba kibali.
  Kwa bahati nzuri Jumuiya za Kiislamu imeliona hilo mapema na tayari
  programu za elimu juu ya mabadiliko ya Katiba zimemaliza kwa muda
  mrefu kwa sasa hivi Jumuiya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuweza
  kujua sheria za nchi na Katiba yao jambo ambalo kwa muda mrefu Serikali
  haikuwa na utaratibu endelevu wa kuelimisha raia zake na hiyo ndio kazi
  inayoifanya Jumuiya kuisaidia Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa sambamba
  na kutoa elimu ya Kiislamu kufunza maadili mema, kudumisha amani,
  umoja, utulivu na mshikamano kwa wazanzibari wote bila kujali tofauti zao
  za kidini, kisiasa, rangi na ukabila pamoja na kusisitiza umuhimu wa kudai haki zao na uhuru wa maoni pamoja na kulinda mali ya umma na kutii Katiba ya Zanzibar na sheria za nchi. Ibara ya 23:1 ya Katiba ya Zanzíbar inasema "kila mtu anawajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Zanzíbar" 23:3 inasema "watu wotewote watatakiwa na sheria kulinda vizuri mali ya Zanzíbar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu… kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya badea ya Taifa lao".

  Ndugu waandishi wa habari.
  Jumuiya ya Uamsho inaendesha mihadhara kwa miaka mingi kuzingatia Katiba yake pamoja na kufuata Katiba ya Zanzíbar inayotoa uhuru wa maoni kutipia ibara ya 18 inayosema "Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yupo huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi".
  Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 "Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi" kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.

  Jumuiya za Kiislamu zinawatahadharisha watu hao na kuwataka mara moja waache kuhubiri uchochezi na uvunjifu wa amani na kuwakumbusha kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria ibara ya 12 ya Katiba inasema " Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote" vile vile wajue hizi ni zama za uwazi haki na sheria hivyo tunawasihi wasijisahau wakavitumia vyeo na ngazi za uongozi kwa maslahi ya wachache sana wasioitakia mema Zanzíbar watambue kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Zanzíbar na sheria za nchi rejea ibara ya 14,16,23 ya Katiba ya Zanzíbar.

  Pia Jumuiya zinapenda kuchukua fursa hii kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 17:8 na 21:2C kwa kuzingatia uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar. Pia kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 10 cha Sheria hiyo hiyo No.8 ya mabadiliko ya Katiba kinachoipa Tume uhuru na mamlaka kamili ambayo Mhe. Mohamed Aboud anaonekana kuvikiuka na kuingilia kazi za tume kwani Katibu Mkuu wa Tume hakuwa na taarifa yoyote wakati Jumuiya zinawasiliana nae akiwa bado ndio kwanza anataka kuisoma taarifa hiyo kwenye mtandao.
  Imani yetu huu ndio Mwanzo wa uvunjifu wa sheria hiyo. Tunapenda kumkumbusha Mhe. Mohamed Aboud maneno ya Rais Dr. Shein aliwataka wananchi wa Zanzíbar wanaishi kwa umoja na mshikamano inapaswa hitilafu ziondolewe ili Wazanzibar waishi vizuri kwa amani na utulivu na kamwe asitokee mtu akiwa ana lengo la kuivunja amani iliyopo rejea gazeti la Zanzíbar leo lenye kichwa cha maneno TUSICHAFUE AMANI toleo No 3743.

  Ndugu waandishi wa habari .
  Tunapenda kumalizia taarifa hii kwa kutoa shukurani zetu za dhati kwa jeshi la polisi kusimama imara katika kudumisha amani ya nchi na kutokubali kuburuzwa na hao wachache wasioitakia mema nchi yetu ya Zanzíbar.
  Ahsanteni sana.

  Nakla:
  Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
  Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar,
  Waziri wa Katiba,
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais,
  Jeshi la Polisi,
  Idara ya Mufti Zanzibar ,
   
Loading...