SMZ kutekeleza ujenzi wa miradi mikubwa

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Uchukuzi Zanzibar, Dk Sira Ubwa Mamboya amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kutekeleza Miradi miwili ya Ujenzi wa Jengo la Abira la uwanja wa Kimataifa Abeid Amani Karume na Ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri ambapo Ujenzi huo unatekelezwa kwa Fedha za Ndani.

Waziri Mamboya aliyasema hayo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu hoja za wajumbe wa baraza hilo wakati wakichangia bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2019/2020.

lisema mradi wa ujenzi wa jengo la abiria terminal 3 hadi sasa haujapata ufadhili baada ya Benki ya Exim kutoka China kushindwa kutoa fedha za kugharamia mradi huo.

Alisema baada ya serikali kushindwa kupata fedha za ufadhili za mradi huo, serikali imelazimika kutumia fedha zake za ndani kugharamia ujenzi huo.

”Mheshimiwa Spika napenda kuwajulisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba mradi wa ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume utatekelezwa kwa kutumia fedha zetu za ndani baada ya kukosa ufadhili,” alisema.

Aidha alisema ujenzi wa bandari ya Mpigaduri iliyopo eneo la Maruhubi Unguja utatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani zinazotokana na makusanyo ya kodi.

Alisema ujenzi wa bandari hiyo ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha huduma za mizigo na usafirishaji kutokana na bandari iliyopo sasa ya Malindi kuzidiwa na utoaji wa huduma.

Alieleza kwamba serikali itaimarisha huduma za mawasiliano ya baharini kwa kununuwa boti tano zitakazotoa huduma kwa wananchi wanaoishi katika visiwa vidogo.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipitisha makadirio mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo.
 
Back
Top Bottom