contask
JF-Expert Member
- Jan 3, 2021
- 257
- 438
Habari wanajukwaa,
Leo nimeona niwaelezee smartphone ilivyonipeleka polisi katika kituo ca msimbazi then njkahamishwa hadi kituo cha Mbweni kilichopo Bagamoyo Road, nisiwachoshe ngoja niende moja kwa moja kwenye kichwa cha uzi wetu.
Mimi ni kijana nipo chuo fulani nikiwa najihusisha kuuza simu plae Kariakoo. Sasa siku moja kuna rafiki yangu naye anapiga mishe za uwinga pale Karikaoo kuuza hizi smartphone hasa used from Dubai aliniunganisha na jamaa mmoja yupo pale Navy Kigamboni, alitupigia simu siku moja akiwa anauza simu ya siku moja na kutuambia kwamba ana simu yake Samsung Note 10 Plus anaitoa kwa laki mbili tu (200000) kutokana na sababu zake binafsi.
Alituchek, tulitafuta hela tuinunue then tuje tuize katika price yake ambayo inarange 450k hadi 400k ikashindikana maana tulikosa pesa. Sasa ilipita kama mwezi hizi asubuhI akanipigia, akaniambia kuwa anasimu nyingine kama ile maana alinunua mbili yake na ya mke wake anaiuza laki mbili tu. Nilifurahi sana na kuona dili la hela limekuja lenyewe bila nguvu na wakati huo kwenye account yangu kulikuwa na ela kama 430k.
Nikaona sio kesi nitoe 200k ninunue simu the nije kutengeneza faida, kweli nikampigia simu nikafika hadi pale kambi ya Jeshi Navy Kigamboni akatoka akaniletea simu nikaiona kwa hakika ilikua ipo clean no dot na krek kwenye kioo, ila kreki kidogo kwenye back glass ila ilikuwa sio tatizo, nikanunua nikaondoka nayo nikafika home kisiwani ambako nayo ipo Kigamboni ni wastan wa dakika 10 hadi kufika Navy Ferry nikachukua nguo niende nyumbani Kisarawe kama ilivyokuwa kawaida yangu kila Ijumaa naenda Kisarawe narudi Jumapili.
Niliondoka na ile simu usiku yule jaama yangu ananipigia kuwa amapata mteja wa ile Samsung Note 10 Plus alikuwa anaitaka kwa 360000 kesho yake jioni nikapanda gari haraka Kisarawe to Gongo la Mboto then nikapanda gari za Temeke nikashuka Sudan ni sehemu ambayo tulipanga tukutane baada ya nusu saa jamaa kafika na mteja biashara haikuachukua muda mrefu ndani ya dakika 10 tu mteja kalipia ile simu 360000 nikachukua 50 nikampa jamaa yangu ambae aliniletea mteja then nikaendelea na safari hadi nyumbani Kigamboni maeneo ya Kisiwan nikawa nimetulia napanga matumizi ya profit ambayo nimeipata.
Wakat huo yule jamaa yangu kampeleka jamaa yangu Kariakoo kubadilisha mfuniko wa nyuma, picha ndio lilianzia hapo!