Smart /bol ndio mtandao gani wa simu?

Smart /bol ndio mtandao gani wa simu?

ugali dagaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
1,277
Reaction score
1,121
Salaam,

Nikiwa Moshi kama wiki mbili tatu zilizopita walikuja vijana watatu katika hoteli nayolala wamevaa fulana zina maandishi ya bol, wakanisalimu "shkamo blaza" kwani niikuwa nimewazidi umri.

Baada ya salam wakaniambia kuwa wao ni wawakilishi wanatoka kampuni ya mawasiliano ya BOL hii kampuni mi naifahamu kwa Dar ilikuwa na ofisi pale karibu na ubalozi wa ufaransa nakumbuka nilikuwa naenda pale kulipa "internet" lakini badae wakahamia pale makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi Titi kuna jengo linamilikiwa na msalaba mwekundu.

Wale vijana wakaendelea kunipa ubora wa huduma yao kwamba laini zao zinatumia satellite kwa hiyo hakuna ardhi nitakayo kayanga chini ya jua nipoteze network nikavutiwa sana kwani shughuli zangu zinahusisha safari za mara kwa mara ndani na nje ya nchi hivyo nikawaza hakutakuwa na haja ya kubadilli line popote nitakapoenda wakanionesha na maandishi kwenye kile kiboksi ya line yameandikwa kwa lugha ya kizungu communication unlimited kweli aise walinishawishi nikajipatia line kwa gharama za shilingi elfu mbili wakanipa angalizo kwamba line ile inatumika kwenye smart phone zenye 3G na modem zinazoingia line zote na kwamba muda wa maongezi (vocha) nitanunua kwenye vibanda vya max malipo.

Baada ya kununua ile laini nikagundua ule mtandao haushiki network mpaka uwe katikati ya jiji la Dar es salaam pekee, namba zao za huduma kwa wateja hazipokelewi mara hazipatikani.

Kama kuna anayejua zaidi labda kuna maelekezo nakosea naombeni msaada manake hata ukifungua ukurasa wa jamiiforum kwenye computer lipo tangazo lao kubwa.

Nimemaliza.
 
Wana akaunti facebuk,nilishawahi kuwauliza swali toka mwaka jana hadi sasa hawajanijibu,nadhani ni kikundi cha matapeli au wahuni,hawako smart kabisa.
 
Hongera kwa kuwapa vijana mchango wa kitochi cha mbege. Ogopa sana mtu anaegawa shiamoo kama hamfahamiani
 
Back
Top Bottom