Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,092
- 1,077
Kimsingi, nakubaliana na wewe, kuna umuhimu wa ku-acknowledge mawazo ya watu wengine. Hata hivyo, ili hilo litendeke, ni lazima wahusika (vyama vya siasa) vianze utaratibu wa kusajili ilani/manifesto/sera/strategic plan zao nk, ziandikwe vitabuni na vipewe International Standard Serial Number (ISSN) au International Standard Book Number (ISBN) nk. kwa kufanya hivyo, itakuwarahisi kubaini nani ka-copy na ku-paste wapi, kamuibia nani na hapo ndipo copyright laws dhidi ya wote wanao fanya pradgiarism watabanwa vizuri kwa kutumia ushahidi usiokuwa na chembe ya shaka!
Kwa pamoja, tuijenge Tanzania kwa mawazo huru na tunduizi!
Thank you so very much for your critical argumentation
*******
DR. LOVE
nilitaka nisiongezee kitu nikashindwa kufanya hivyo kutokana na mazungumzo yetu kuwa mazuri sana. utata wa documentation zenye alama za kumbukumbu umeleta migogoro mingi sana katika historia ya uvumbuzi kiasi kwamba kila mtu anaweza akasema alikuwa wa kwanza kutengeza tairi, au mashine ya kupiga chapa. lakini bado hili haliondoi umuhimu wa kutambua asili ya kitu na kukiri. wenzetu waliopo katika anthropology na archeology wamejenga fani katika hitihada hii ya kutambua juhudi za mwanadamu na kukiri asili, hata pale ambapo kitabu kilikosekana. kukosekana kwa documentation zenye serial number hakuondoa umuhimu ya kutambua na kukubali asili ya kitu. hili ni jambo linalohusu ustaarabu tu; na si kitu kingine.
uwe na usiku mwema ndugu yangu. nikushukuru pia kwa mchango wako mzuri.
good do!