Slaa azituhumu Kamati za serikali kwa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa azituhumu Kamati za serikali kwa ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 8, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,153
  Trophy Points: 280
  Date::9/7/2008
  Slaa azituhumu Kamati za serikali kwa ufisadi
  Tausi Mbowe
  Mwananchi

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa, amezituhumu baadhi ya Kamati za uchunguzi ikiwemo ya ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu Tanzania (BoT), kuwa zinafanya ufisadi juu ya ufisadi, kwa kushindwa kutoa matokeo yanayotarajiwa na umma.

  Kauli hiyo Dk Slaa, imekuja siku chache baada ya kubainika kwamba Timu ya Rais ya Kuchunguza ufisadi wa zaidi ya sh 133 bilioni za EPA imetoa mapendekezo ambayo tayari yalifanywa na Kampuni ya Ukaguzi wa Kimataifa ya Ersnt&Young.

  Akizungumzia matokeo hayo ya timu ya EPA, alidai kuwa kitendo cha tume hiyo kushindwa kuja na mapendekezo mapya ni matumizi mabaya ya fedha za umma na ucheleweshwaji wa hatua za serikali kuwashughulikia mafisadi.

  Dk Slaa alidai kuwa kinachofanyika sasa ni kiini macho na kuongeza kwamba, inaonyesha wazi kuwa serikali haiko makini au hawasomi ripoti ambazo zimeshafanyiwa kazi na kutolewa mapendekezo.

  "Tumechoka na matumizi ya fedha yasiozingatia kipato halisi cha Mtanzania, kuiongezea muda tume ya Mwanyika hata ukimtuma azunguke dunia nzima, haiwezi kuja na kitu kipya, mapendekezo yote yapo katika ripoti ya Ernst & Young, kinachotakiwa ni kufanyiwa kazi tu," alisisitiza Dk Slaa.


  Dk Slaa alitoa mfano wa Tume ya Jaji Bomani iliyoundwa kupitia upya Sheria za Madini, amabyo alidai kuwa imetumiza zaidi ya Sh1 bilioni lakini imekuja na mapendekezo kama ya ripoti ya Masha.

  Alisema kiini macho hicho kinapelekwa kwa Watanzania, ili kuwapumbaza badala ya serikali kutafuta ufumbuzi katika suala zima la ufisadi ili kuokoa pesa za umma.

  Dk Slaa alisema fedha zilizotumika katika tume hizo zingeweza kutumika katika maendeleo ya sekta mbalimbali kama afya na elimu badala ya kutumiwa na watu wachache kwa kuunda tume ambazo mapendekezo yake uishia kabatini.

  Ukiacha timu ya Jaji Bomani, Tume ya Rais kuhusu EPA, iliyotumia mamilioni ya shilingi kuchungunza suala hilo, inaonekana kupoteza muda katika kushughulikia suala hilo na kisha kushindwa kuja na mapendekezo mapya tofauti na yaliyotolewa na kampuni ya Ernst & Young iliyokagua akaunti hiyo".


  Mapendekezo ya kamati hiyo yaliyopo katika ripoti iliyotolewa bungeni Agosti 18, mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete, yanafanana na mapendekezo ya Kampuni ya Enst & Young ilifanya ukaguzi ndani BOT.

  Timu hiyo iliyokuwa inaongozwa na Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Edward Hosea, inaonekana kwamba imechukua sehemu kubwa ya kazi iliyofanywa na kampuni hiyo.

  Moja ya mapendekezo yanayoonesha kuwa timu ya Mwanyika haikufanya kazi ni pendekezo namba 4.5 la Kampuni ya Enst&Young iliyoitaka serikali kumalizia uchunguzi wa upotevu wa zaidi ya Sh42 zilizochotwa na makampuni tisa.

  Mapendekezo mengine yaliyotolewa na Kampuni ya Enst&Young ambayo pia ndio yaliyotolewa na timu ya Mwanyika, ni serikali kuweka utaratibu wa kisheria ikiwamo kukamata mali za watuhumiwa kuhakikisha zaidi ya Sh90 bilioni zilizochotwa na makampuni 13 zinarudishwa.

  Mengine ni kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wa BoT waliohusika katika mchakato huo, kubadili utaratibu wa Mtendaji Mkuu wa Benki kuu kuwa mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Wizara ya Fedha kuanzisha kitengo maalum kushughulikia masuala ya EPA, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa akaunti ya EPA na BRELA kuanzisha uchunguzi wa makampuni hayo na kuyafuta kwenye daftari lake.

  Katika hotuba yake aliyoitoa Bungeni, Rais Kikwete amewaongezea muda wa siku 71 mafisadi hao kurudisha fedha walizochukua kwa kulinda haki za binadamu na utawala bora na sio kutokana na udhaifu wa tume hiyo.

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, uchunguzi kuhusu Sh 90.3 umekamilika, lakini ule wa Sh 42 umekamilika kwa ndani nje ukiwa bado na kuongeza kwamba, hadi sasa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kupata taarifa zaidi za watuhumiwa.

  Alisema tayari watuhumiwa wengi wa Sh90.3 bilioni kati ya 133 ambazo uchunguzi wake umekamilika, wamezuiliwa hati zao za kusafiria, magari na nyumba zao kukamatwa.

  Rais Kikwete alitoa hutuba hiyo iliyoonyesha kuwa fedha zlizokusanywa zilikuwa Sh53 milioni ambayo zilitofautiana na taarifa zilizotolewa awali na vyombo totauti na kwa wakati tofauti.

  Kamati ya Mwanyika ambayo ilitoa taarifa miezi mitatu baada ya kuundwa na kukabidhiwa Rais kushughulikia suala hilo, ilisema imekusanya Sh60 bilioni na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikasema zimerudishwa Sh64 milioni.

  Ufisadi katika EPA ulibainika baada ya ukaguzi wa awali wa Kampuni ya Deloitte&Touche ya Afrika Kusini, ambayo iliibua katika malipo ya Sh 40 bilioni kwa Kampuni ya Kagoda, hata hivyo BoT ikasitisha mkataba.

  Baada ya tuhuma hizo kuibuliwa bungeni, serikali ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutafuta Kampuni ya kimataifa ya Ernst&Young, kufanya ukaguzi ambao ulibaini ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika hesabu za mwaka 2005/06 ndani ya BoT.

  Kufuatia ufisadi huo, Januari 9, mwaka huu, Rais alitangazia umma kuunda timu chini ya Mwanyika na kuipa miezi sita ambayo ilimkabidhi ripoti Agosti 18 na kumfukuza kazi aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, marehemu Daudi Balali.
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndulu aliwahi kuulizwa hili swali, kwa nini unafanya uchunguzi mwingine, akajikanyaga kanyaga, eti ule wa awali ulikuwa una madhumuni mengine. Crummy press ikampetesha. Ni Dk. Slaa peke yake ndio ameliona hili swala ni muhimu kulifuatilia. Yani hili tamko ni bonge la hatua. Bongo huwa hatufuatilii na kuuliza vitu kama hivi.

  Sasa Kikwete afanye mpango wa kumwambia "Mwema mkamate Slaa."
   
 3. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,084
  Likes Received: 15,718
  Trophy Points: 280
  Yani haya mambo mie sijui hata watafanyaje kurekebisha maana kila siku yanakuwa makubwa
   
 4. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Si amkamate hiyo itakuwa ni kutumia vibaya madaraka ambayo amepewa na wananchi na sidhani maana nzima ya kuwa na mchakato huu mzima wa vyama vingi na freedom of speech si ni haki ya kikatiba ili mradi sheria haikuvunjwa. Unajua zamani enzi za marais walopita freedom of speech ilikuwa kama imeshikiwa chini kwani viongozi hawa wananchi waliwahesimu sana kwa kuwa kufanya maamuzi mengi yalikuwa sahihi kwa kiasi fulani.

  Sasa pale wananchi walipoanza kubwata ni dhahiri kuwa something went wrong na window of opportunity was open as a way through vyama vingi vya siasa.

  Kila aliyepewa dhamana na wananchi anapaswa kuwa answerable kwa wananchi or to be compeled to be answerable.
   
Loading...