Idimulwa
Platinum Member
- May 27, 2011
- 5,113
- 2,700
Umefika wakati Dr Slaa anapaswa awe makini sana na maamuzi yake..kama kila kosa ataangalia tu adhabu kwa mjibu wa taratibu za chama kama kwamba anaongoza malaika basi tutaharibikiwa muda si mrefu..si kila kosa ni kufukuza mtu au kumsimamisha uanachama..ambo mengine ya malizwe kidiplomasia...Kumpoteza mtu kama E.Nanyaro ndani ya chama hasa katika kipindi hiki ambacho CCM wanaonekana kuzinduka usingizini siyo afya kwa CHADEMA hata kidogo.Nimeliona hili Mkoani Geita, ambapo Katibu wa Bavicha, Bwana Paulo Vicenti,Mwenyekiti wake Otto na Mratibu wa Uenezi Bwn Filbeti, walifanya makosa ambayo kwangu niliona yanaweza kumalizika kwa njia ya kidiplomasia..lakini Dr aliwasimamisha uanachama...siyo siri kuondoka kwao kumesababisha cdm ifubae Geita...kama kuna mwana Geita hapa jamvini aliye genuine aje akanushe.Hawa vijana wameanza na chama wilayani hapa from zero, lakini kwa kosa moja tu wametupwa nje,nadiriki kusema wazi kuwa vijana hawa kama wangekuwepo tungeweza hata kushinda kata ya Lwenzera ambapo Dr.Slaa mwenyewe alifika kwenye kampeni lakini tukaambulia patupu. Nakumbuka vizuri maneno ya Mwenyekiti mteule wa CCM bwana MSUKUMA alivyokuwa akitamba hadharani kuwa cdm imefifia tangu wawaengue vijana hao na kwamba atatwaa kata ya Lwenzera bila msaada toka makao makuu ya ccm. Slaa tafakari