Bado alikuwa na kaheshima fulani kamebaki, lakini kama amerudi afanye mambo kwa maagizo ya CCM waliokuwa adui zake wakubwa nitaamini kuwa Dr.W.Slaa ana laana ambayo hatujui aliipatia wapi. Pole yake sana na tunamwombea kwa Mungu amfunulie huyu mtumishi wake, na kama ni mchumba ndio chanzo amwepushe naye haraka sana kama sisi tunavyomwomba Mungu katika sala kuu, "Utuepushe na yule Mwovu kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu"
Mwambiye kuwa tunamkaribisha. Asiisahau kadi huko uzunguni tuu aje ampe kura yake LOWASA japo kishakula hela ya miccm.
Asijaribu tu kumtusi Lowasa kwani ni kumwinua juu Zaidi. Hakuna atakachokisema kiwabadili watu tena. Hana tofauti na kina Juliana wa shuzi huyo
siraha alikuwa na mwanakijiji wakijaribu kuangalia maneno mapya ya kuwalaghai Watanzania... tutawasikiliza bila kujali hadaa zao ili wajisifu japo kidogo
Hivi bado ana-impact yoyote huyu mtu? Labda aitishe conference ya kuchukua kadi rasmi ya ccm,! Hata hivyo,nadhani hii tamaa ya Dr na Mkewe imepita kipimo. Mungu atawahukumu hapa hapa,
Maskini kodi za Wananchi,watoto wanakaa chini,wakina mama wanajifungua vichochoroni,vijana wameharibika kwa madawa ya kulevya,wananchi wanachangishwa ujenzi wa maabara huku mamilioni yanalipwa kwa wapinga demokrasia na wabakaji wa weledi pamoja na kununua wanasiasa mamluki..Eee MUNGU, OKOA TANZANIA kutoka katika rangi ya Kijani na njano!!MTANZANIA kwa kupiga kura yako moja kwa LOWASSA utakuwa tayari umeikomboa nchi yako!!