Slaa aibua mgogoro wa kikabila

Slaa aibua mgogoro wa kikabila

Upanga Mkali

Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
96
Reaction score
83


. Waluguru, wakwere, wazaramo waja juu
. Wasema tambiko lao limekhanithiwa


KITENDO cha baadhi ya wazee wanaojiita kutoka Dar es Salaam, kumvika uchifu Katibu Mkuu wa Chadema Wilibroad Slaa, kimelaaniwa na wazee wa kabila la Waluguru, Wakwere na Wazaramo.


Wazee hao wanasema, wameshangaa kuona watu wachache waliojipachika uwakilishi kwa watu wengine na kumvika uchifu Slaa ambaye hana nasaba na makabila ya Pwani.


Wanasema wasingeshangaa iwapo uchifu huo angevikwa Mwenyekiti wa CUF Ibrahimu Lipumba ambaye ni mtani wa makabila hayo, lakini sio Slaa ambaye anatoka mbali nao.


"Yani hawa wazee wenzetu wamekhanithi matambiko yetu, hivi kweli Slaa ambaye anatoka mbali na sisi anaweza kuwa Chifu wetu? Tusingeshangaa kama hilo angefanyiwa Lipumba ambaye ni Mnyamwezi, na mtani wa wazaramo, wakwere na waluguru, lakini sio Slaa" alisema Mzee Mwinyi Mgeni mkazi wa Bagamoyo.


Mwinyi Mgeni alisema, wazee waliomvika uchifu Slaa wanaonekana wazi ni watu walionunuliwa ili kukamilisha jambo hilo, lakini hawana wanachojua kuhusu historia ya makabila hayo na hata Slaa hajafuatilia kubaini uhalali wa uchifu aliovikwa.


"Tunasikia kwenye maeneo mengine machifu wakibadilishwa kila mara, tena ukifuatwa utaratibu maalum, huu uchifu wa Slaa una Silsila gani? Hao waliomvika uchifu walikaa na nani na kukubaliana kumpa uchifu Slaa?" alihoji mzee huyo.


Taarifa zaidi zinasema mchezo huo umebuniwa na Slaa kwa lengo la kujiwekea mazingira ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa UKAWA, nafasi ambayo wanaigombea yeye na Prof. Lipumba.


"Slaa amewalipa wale wazee ili kuitisha UKAWA ionekane anakubalika na watu wengi, hivyo wamteue kuwa mgombea ingawa watu wengi wamegundua mchezo huo na amezua mgogoro mkubwa na wenye makabila yao" alisema kada mmoja wa Chadema.
 
Teh teh teh, mazingira ya kuteuliwa eeeh kama naniii?
 
Kama hamtaki awe chief kale malimao
 
Back
Top Bottom