Shondola
Member
- Apr 2, 2014
- 95
- 58
Unapozungumzi Kikao cha Bunge kinachotazamiwa kuanza mapema wiki ijayo si rahisi sana kusahau kuzungumzia skendo ya SUKARI ambayo kwa sasa imekuwa ikiitafuna Nchi.
Tumetoka kwenye Skendo kubwa ya Account ya Tegeta Escrow majuzi na sasa Skendo ya Sukari limekuwa ni janga kwa Taifa hasa kutokana na swala hili kuhusisha viongozi wakubwa waandamizi wa Taifa hili.
Taifa hili linajua kuwa ni vigumu sana kuzungumzia swala la Sukari ukaacha kumtaja mtu kama Pinda na mfanyabiashara maarufu kutoka Zanzibar Bwana Turkey.
Skendo hii ya Sukari sasa imechukua sura mpya hasa baada ya Ofisi ya Bunge kumpiga Stop Mhe. ASUMPTA MSHAMA (Mb) kuwasilisha hoja yake binafsi kuhusiana na Skendo hiyo.
Mhe. Asumpta Mshama aliiomba ofisi ya Bunge kama kanuni zinavyomtaka ili aweze kutoa hoja binafsi kuhusiana na skendo hiyo ya sukari lakini bila hata ya kupewa majibu ya kuridhisha Mbunge huyu alipigwa stop.
Wabunge walio wengi wamesema wanajua na wanaelewa ni kwa nini Asumpta kapewa zuio kimsingi ni ili kumlinda Waziri Mkuu ambaye ndiye muhusika mkuu katika Skendo hii. Wabunge wameapa kwamba hata kama Asumpta akipigwa Stop hili swala ni lazma lizungumziwe.
"Wao wanadhani kumnyamazisha Asumpta ndiyo suluhu?? Hatuwezi acha Nchi inatafunwa namna hii halafu tuendelee kukaa kimya tulianza na Escrow na hili la Sukari nalo lazma lichukue mkondo wake." Alisikika akizungumza kwa hasira Mhe. Kigwangala..
Wabunge vile vile wameonekana kusikitishwa sana na jitihada anazozifanya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Ndgu William Vangimembe Lukuvi za kutoa kiasi kikubwa cha HONGO kwa baadhi ya wabunge ili kuhakikisha swala hili linazimwa na linafia mbali. Katika hili Lukuvi anasaidiana sana na mfanyabiashara kutoka Zanzibar bwana Turky.
"Sikiliza mwandishi sisi tulio malofa tunajua na tumeshaona jitihada za Lukuvi za kugawa pesa tena pesa zenyewe zinagawiwa kwa staili anazamwa nani apewe nini.... Hela tutapokea angalau tukajiandae vyema majimboni ila nakuhakikishia huu moto ushakama bati hauzimiki tena huko Bungeni lazma tutatoana roho.. Huu unafiki wa mtu kujifanya masikini kumbe anatuzunguka na ana mihela kibao hatuutaki tena tumechoka bwana" aliongea huku akisisitiza Mhe. KESSY.......
Hata hivyo tulitamani vile vile kupata maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC juu ya Skendo hii. Na mwenyekiti wake alilikugusia kwa juu tu "kamati yangu ilikwenda mpaka kwenye kiwanda cha sukari tumezungumza kwa kina na wahusika na bodi ya sukari vile vile na tumepata tunachohitaji..... Yatosha kusema hata wagawe Mabilioni hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe jingine....."
Mpambe mmoja wa Waziri Mkuu Pinda ambaye ndiye anayesemekana kuwa mbeba mikoba na mshika fedha za Uraisi alipotakiwa kuzungumzia hili sakata hasa kutokana na Mkubwa wake kuhusishwa na Skendo hii moja kwa moja hakuonekana kukubali wala kukataa alisema sentensi fupi sana ambayo bado tunaifanyia tafakuri alisema hivi "Wao wanamwona Pinda tu wakaulize na ziara zinazofanywa na Chama fedha zinatoka wapi...." Hapa tuliachwa njia panda na kutufanya tuendelee kutafiti maneno haya ya bwana mkubwa huyu..... Kwa kuwa sentensi yake ina maana zaidi ya Moja. Kwanza yeye anakubaliana na hilo la Sukari dhidi ya Mkubwa wake lakini pili anataka kuaminisha watu kuwa si Pinda peke yake ila kuna vigogo wengine.
Macho na Masikio ya watanzania sasa yanaanza kuelekea Dodoma kuanzia tarehe 27.............