SIZONJE Ahadi si neno, Tunangoja hatima

SHADOWANGEL

JF-Expert Member
Sep 15, 2014
528
348
Sizonje kiukweli watu wanalia kama asemavyo mrisho mpoto kwa kubainisha kuwa watu wanalia tofauti lakini msiba ni mmoja.

Lakini ningependa kukuambia Mpoto Asiyekujua hakuthamini kwa kuwa Cha kichwa kitamu, na cha mkia kitamu kwani waswaili wanasema "Chetu si changu, usitumaini cha mwenzako"

Sizonje kumbukumbu yangu katika kukumbuka ni kuwa Furaha hukolea mkiwa wengi ingawa kila mmoja anafuata mto haone bahari ila kumbuka hata katika kundi mtu anaweza kuwa peke yake pia usisahau sizonje waswaili waliposema heri jirani karibu kuliko ndugu mbali.

Sizonje, Mpoto kanikumbusha kuwa Jana hufufuka leo wakati mwingine ikiwa hujui jinsi anavyokula mtu, je utampa chakula katika jani? Sizonje usisahau waswaili wanasema Ila ya kikwapa kunuka pasipo kidonda.

Sizonje, Mpoto kanikumbusha kuwa Jicho haliwezi kuangalia, pua inalia ndo maana kila mmoja akafundishwa Jirani mwema ni bora kuliko rafiki na ndo maana waswaili wakasema Kidole kimoja kikiumia, vingine vyatoa damu kama unakumbuka nawe ili Sizonje.

Sizonje, Mpoto kanikumbusha kuwa TUHESABU IDADI ZA MAITI ZINAZOTEMBEA AU TUZIKE KWANZA MAANA KIUKWELI HUKU NJE WATU WANALIA WAPO WANAOLIA KIMYA KIMYA NA WANAOLIA KWA SAUTI LAKINI WOTE WANALIA KWA JAMBO MOJA TU...............
 
Back
Top Bottom