Siyo wote, ingawa ni wengi wao!

Siyo wote, ingawa ni wengi wao!

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,648
Reaction score
10,844
Nilipokuwa mdogo, kutokana na niliyokuwa nikiyasikia kuhusu waandishi wa habari, niliamini hiyo ni taaluma ya watu waongo sana. Lakini baada ya kukua, nilibaini kuwa waandishi wenye weledi siyo waongo, bali hutoa habari kulingana na hali halisi.

Nimeligundua lingine la kushangaza zaidi, ni kuwahusu wanasiasa. Sitaki kusema, lakini uzoefu unaonesha kuwa ni waongo mno. Si waliopo Chama tawala au vya upinzani, kote uongo umetamalaki. Hata hivyo, siyo wanasiasa wote ni waongo.

Kiongozi mkubwa, labda wa Serikali, anapoamua kusema uongo huku akijua ni uongo, anatarajia nini kama siyo kuaandaa mazingira ya yeye naye kudanganywa?

Inasemekana Tanzania kuna tatizo la ukwepaji kodi. Kama ndivyo, huo nao ni uongo. Serikali itakuwa na uhalali wa kulalamika watu kukwepa kodi huku na yenyewe imeshajizoesha kudanganya watu wake?

Nilipokuwa mwaka wa tatu chuoni, kuliibuka maandamano baada ya baadhi ya "kozi" kutokupewa haki ya kuhudhuria mafunzo kwa vitendo (field).

Nakumbuka vyombo vya habari vilipofika eneo la tukio, wanachuo waliridhia kuongea na ITV, STAR TV, n.k., lakini wa TBC walifukuzwa. Hawakuwa na imani nao.

Baadaye kwenye taarifa ya habari, vyombo vingine viliripoti kilichotokea kama kilivyotokea, isipokuwa TBC pekee. TBC walitangaza kuwa sababu ya mgomo ni kucheleweshewa hela ya kujikimu.

Kesho yake hilo suala liliibuka bungeni. Waziri mwenye dhamana aliahidi kufuatilia, na baadaye alipokuwa akitoa ripoti ya ufuatiliaji alioufanya, naye alitoa jibu kama la TBC: kwamba sababu ya maandamano ni kucheleweshwa kwa hela ya kujikimu. TBC ilidanganya, na Waziri naye akadanganya.

Ukweli ulikuwa ni field, walikuwa wakidai haki ya kuhudhuria mafunzo kwa vitendo.

Miaka ya hivi karibuni, kumetokea matukio ambayo Serikali ilipotoa majibu, kuliashiria kuwepo kwa uongo.

Wakati fulani, kuliibuka taharuki baada ya miili ya watu kuokotwa kwenye viroba. Waziri mwenye dhamana alipoulizwa, alisema ni miili ya wahamiaji haramu. Kama si uongo, yeye alijuaje kuwa ni ya wahamiaji haramu?

Wakati fulani, kiongozi wa nchi aliadimika kuonekana hadharani tofauti na kawaida yake. Mmoja wa viongozi wakubwa alipopata nafasi ya kulizungimzia hilo, alisema "mkubwa" yupo buheri wa afya. Siku chache baadaye, tukafahamishwa vinginevyo. Aliamua kuudanganya umma au naye alidanganywa na hivyo kujikuta anasema uongo bila kujua?

Wakati fulani, kuliibuka mchezo wa wanasiasa kutoka Vyama fulani kutimkia chama fulani. Lakini hoja walizokuwa wakizitoa, zilikuwa dhahiri kuwa ni uongo uliokosa ubunifu. Zilikuwa zimefanana sana.

Wakati fulani, kuliibuka taarifa yenye taharuki kuwa kulikuwepo na mapigano kati ya Polisi na Wamasai wa Loliondo. Serikali kupitia kwa mmoja wa viongozi wakubwa, ilieleza kuwa hakukukuwepo na kitu kama hicho. Hata picha za majeruhi zilizorushwa mtandaoni, Serikali ilidai hazihusiani na kilichokuwa kikiendelea Loliondo. Muda mfupi baadaye, Mkuu wa Mkoa huo alisikika akimwombolezea Polisi aliyepoteza maisha Loliondo kwa kupigwa mshale. Mtu anapigwaje mshale mahali penye amani?

Wakati fulani, kulitokea ajali ya ndege kuanguka ziwani. Kiongozi wa Mkoa alipokuwa akilizungumzia hilo, alisema rubani alikuwa salama na kwamba ameongea naye kwa simu. Rubani alikuja kutoolewa kwenye ndege akiwa marehemu. Mkuu wa Mkoa aliongea na rubani wa ndege ipi?

Wakati fulani, mwanasiasa mmoja alipigwa risasi mahali ambako palidhaniwa pana usalama wa hali ya juu. Majibu ya Polisi na Serikali kwa ujumla yalionesha kuwa huenda kuna linalofahamika lakini limefichwa.

Wakati fulani, "dereva" na wasaidizi wake waliwahamasiha watu kuvukiza ili kujikinga na "homa". Gari like lile likiwa na abiria wale wale, lilikuja kukabidhiwa kwa dereva mwingine likiwa na wasaidizi wale wale. Ajabu ni kuwa, baada ya dereva mpya kukaa nyuma ya usukani, wasaidizi nao walibadilika. Walianza kuwahamasisha watu watumie njia za Kizungu kujikinga dhidi ya "homa". Kufukiza kulichinjiliwa mbali.
Wasaidizi wale wale waliokuwa wakiwahamasiha watu kuvukiza wakawa wanawahamasisha watu wasivukiza.

Serikali ishasema mengi ambayo mengine yana viashiria kuwa huenda ni uongo. Wanasiasa wameshasema "mauongo" mara nyingi, na bado wanaendelea kusema mauongo, kiasi kwamba kumewafanya watu wengine kuwa na tahadhari nao mno.

Japo si wote, lakini utambulisho unaoweza kuwabeba wanasiasa wengi ni UONGO!

Wanasiasa wengi ni waongo, lakini siamini kuwa uongo ni lazima kwenye siasa na uongozi kwa ujumla.

Ufike wakati, wanasiasa na viongozi waongo wakataliwe hadharani. Vinginevyo, uongo utaendelea kuridhishwa kizazi baada ya kizazi.
 
Jamii ya watu wajinga ni rahisi kudanganyika.
 
You made my day!! By reading your thread it reminds me that in Tanzania never trust a politician.....! Never.
 
Ila wanasiasa nao! Sijui wakati mwingine wanafikirije!!!

Lowassa alipokuwa CCM, alisakamwa na Wana CCM wenzake na wanasiasa wa upinzani. Alipohamia upinzani, wa upinzani waliokuwa wakimponda wakampa jina zuri. Karudie CCM, hakuna kelele tena. Si CCM wala upinzani. Wote kimya!!!

Lazaro Nyalandu alipohamia Upinzani, kuliibuliwa tuhuma kumuhusu katika kipindi alichokuwa Waziri. Sasa hivi Yupo CCM. Sijui zile tuhuma zilioshiaga wapi!

Wanasiasa wengi ni waongo.

Kuna wanaodanganya kwa kuwa walikusudia kudanganya, hivyo kujitahidi kupanga porojo zao kwa namna amabyo inaweza ikauzika, na kuna wanaodanganya kwa kuwa ni waropkaji wanaoongea bila kufikiria.
 
You made my day!! By reading your thread it reminds me that in Tanzania never trust a politician.....! Never.
Hata mimi sitakaa niwaamini ingawa sitaacha kupiga kura, labda tu itokee dharura.
 
Back
Top Bottom