Siyo maajabu, Sanitizer ya bacteria vs Virus Sanitizer

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,206
Reaction score
25,399
Amani kwenu wanajamvi na poleni kwa changamoto za maisha yanayokumbwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo hili la covid19.

Twende kwenye mada.

Nimekuwa mfuatiliaji na baadaye mtumiaji wa hii kitu inaitwa sanitizer, katika kufuatilia nimeona hapo nyuma kabla hii kitu haijawa maarufu, baadhi ya sehemu wamekuwa wanaitumia kama kusafisha mikono kabla ya kula au huko hospitali.

Tukija kwenye janga la covid19 kuna swali kama siyo maajabu, huu ugonjwa tunaambiwa wadudu wake ni virus na siyo bacteria, ukifuatilia kwa umakini naambiwa Sanitizer ni kwa ajili ya bacteria!.

Sasa nini kinafanyika kwenye mdudu au virus wa corona kwa sanitizer wakati hiyo kitu inafanya vizuri sana kwa bacteria?

Ukisoma kipeperushi chake kinasema, Antibacterial "kills 99.9% bacteria"
 
Ili swali nimejaribu kuuliza wee, nimechoka sijapata jibu lake yaani wataalamu wameshindwa kabisa kunidadavulia. Asante mkuu umeliweka wazi ngoja waje wataalam wa JF labda tunaweza pata jibu.
 
Nimeitoa Mahali kupitia Group moja la WhatsApp nadhani huyu kijana amejaribu kuelezea vizuri,kuhusu hivyo vitu vya Sanitizer Mkuu.Na mimi nilikuwa na utata lakini nilimuelewa vizuri kabisa.

HAND SANITIZER
Watu mnajiuliza kuna nini ndani ya Hand Sanitizer na baadhi yenu mkilalamika uwepo wa feki mtaani,Sasa Hii ifuatayo ni elimu kidogo kuhusu Hand Sanitizer na kwanini tunasisitizwa tunawe mikono yetu kila muda.

Lugha za kisayansi kidogo ila ukinunua soma uone Components zake ujue ipi ni bora na ipi sio bora,na kwanini huwezi kunywa hand sanitizer.*

Hand sanitizer zipo za makundi mawili ambayo ni Alcohol-based(Yenye Pombe) and Alcohol free hand(Isiyo na pombe) sanitizer.Ila kwa sasa muhimu kwetu na ambayo ina ufanisi mkubwa ni Alcohol- Based Hand sanitizer.

Sasa Hand sanitizer huwa na components zifuatazo
Alcohol 60-95%
Ambapo alcohol inayotumiwa sana ni Ethanol(CH3CH2OH) na nyinginezo zinazofaa kama ulisoma form four Organic chemistry utakuwa unakumbuka,na hiyo ethanol au Alcohol yoyote ambayo ina faa kuwepo basi ukinunua kwenye chupa inayoonyesha vilivyopo ndani Alcohol yoyote inaishia na herufi za mwisho 'ol' na itakuonyesha na asilimia zake na huwa inakuwepo kwa kiwango kikubwa(Asilimia).

Components zingine ambazo zinaweza kuwepo zikiambata ndani ni kama vile.. Water,Glycerin,Hydrogen peroxide, Isopropyl myristate,Propylene glycol, Tocopheryl acetate,Carbomer,Fragrance(Harufu) ndiyo maana huwa unaona zinanukia vizuri.

UFANISI WA HAND SANITIZER
Ufanisi wake inategemea na jinsi gani au ni kwa namna gani inatumika.Kwa mfano kiwango gani kinatumika,muda wa kutumia,kiasi cha matumizi au unachotumia,Wadudu gani au uchafu uliopo kwenye mikono ya mtu ambapo hivyo vyote vinategemea na mchanganyiko uliopo kwenye Hand sanitizer. Kwa ushauri tu Alcohol-Based sanitizer ndiyo bora zaidi.

Hata hivyo kutokana na utofauti wa ufanisi wa hizo Hand Sanitizer inaweza kudhibiti kusambaa kwa magonjwa ya kuambukiza kwenye mazingira ambayo unawaji wa mikono ni hafifu .Nadhani hapa kwenye group pia nanyi ni mashahidi kwa sisi Watanzania kunawa mikono ni shidaa.

Twende kwenye kama Hand-Sanitizer inaua vijidudu na virusi vilivyopo kwenye mikono na kwanini basi huruhusiwi
kunywa??

Madhara ya kunywa hiyo hand-sanitizer ni kwamba ukinywa unaweza kusababisha kuharibiwa kwa viungo vya ndani ya mwili kama vile INI na Figo,Matatizo ya kuona,Kupoteza kumbukumbu,Sumu za Pombe ambapo zinaweza kupelekea KIFO.Hii ni kwa sababu pombe iliyopo kwenye Hand-Sanitizer haijawekwa tayari kwa ajili ya kunywaa kama zile zingine zinazonywewa.

Ikumbukwe pia kama huna Hand-Sanitizer Nawa tu mikono vizuri na Sabuni yako na Maji tiririka basi hapo utaua vijidudu vyote vilivyopo mikononi.

TUENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI,CORONA IPO NA NI HATARI,JILINDE WEWE NA WENZAKO PIA,FUATA MAELEKEZO YOTE YA WATAALAMU ACHA MZAHA.NA TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA LETU KWA MUNGU.
 
Bado sijaielewa sana hii article ndugu yangu mazaga one, kwa mimi ambaye sina elimu kubwa kwenye sayansi ya baiolojia ninajua kirusi ni kiumbe kisicho na uhai kikiwa eneo lisilokusudiwa kama kwenye meza, mikononi na sehemu nyingine ila kinapata uhai kikiingia mwilini, sasa kama ni kiumbe mfu mikononi sanitizer ina kazi gani?
Kwa maana hiyo unaweza tumia sanitizer na kikaendelea kuwa mikononi, au mi ndo najichanganya?
 
Nashukuru mkuu kwa kuleta mada hii ambapo hat a mimi nimekua nikijiuliza maswali mengi sana, kuhusu hizi hatua tulizoshauriwa tuzichukue, Muda mrefu sana nimeuliza maswali mengi kuhusu matumizi ya sabuni na maji tiririka kwenye udhibiti wa Virus, lakini nimekua nukijibiwa kirahisi tu wewe nawa.

Lakini ukweli tukirudi hata kwenye biology ya form two, hatujawahi kufundishwa kuwa virusi wanaweza kuuwawa na sabuni isipokuwa bacteria, na ndo maana hata matangazo ya sabuni kama dettol yanasisitiza kuwa sabuni inasaidia kuuwa bacteria na si virus. Kwa uwelewa wangu wa hovyo hovyo ni kuwa bacteria wanauwawa kutokana na kiasi fulani cha joto na ndo maana vifaa vinavyotumiwa kwa magonjwa ya virus ushauri ni kuvichemsha na sio kuviosha na sabuni au maji tiririka.

Naomba kama humu ndani kuna manguli wa mambo ya korona na virusi watusaidie kwenye hili kitaalamu ili na sisi mabush doctor tupate uelewa wa hili.
 
Sanitizer ina Pombe na pombe inakuwa na asilimia kubwa,angalia WHO wanasema angalau iwe na asilimia kama sikosei 70% na kuendelea,kwa hiyo ukinawa tu kwa kutumia hiyo kitu unaviua hvyo virusi ambavyo vinakuwa dormant.Kwa hiyo ukinawa unaepusha hatari.

Hebu fikiria kabla ya zoezi lilivyoanza na kunawa,Jinsi mikono yako ulivyokuwa unafanya mambo mengi,kwenye mizunguko yako ya kila kwa hiyo Huu wimbo wa kunawa kunawa ni Usalama wetu.
 
Nashukuru mkuu kwa kuleta mada hii ambapo hat a mimi nimekua nikijiuliza maswali mengi sana, kuhusu hizi hatua tulizoshauriwa tuzichukue, Muda mrefu sana nimeuliza maswali mengi kuhusu matumizi ya sabuni na maji tiririka kwenye udhibiti wa Virus, lakini nimekua nukijibiwa kirahisi tu wewe nawa.

Lakini ukweli tukirudi hata kwenye biology ya form two, hatujawahi kufundishwa kuwa virusi wanaweza kuuwawa na sabuni isipokuwa bacteria, na ndo maana hata matangazo ya sabuni kama dettol yanasisitiza kuwa sabuni inasaidia kuuwa bacteria na si virus. Kwa uwelewa wangu wa hovyo hovyo ni kuwa bacteria wanauwawa kutokana na kiasi fulani cha joto na ndo maana vifaa vinavyotumiwa kwa magonjwa ya virus ushauri ni kuvichemsha na sio kuviosha na sabuni au maji tiririka.

Naomba kama humu ndani kuna manguli wa mambo ya korona na virusi watusaidie kwenye hili kitaalamu ili na sisi mabush doctor tupate uelewa wa hili.
Mkuu unachosema ni kweli lakini hata vifaa vya Hospital unaweza visafisha na spirit tu nayo ikatosha ,kwa hiyo wimbo wa Kuua virusi ni Pombe tu.
Kuhusu Sabuni kuna kemikali ambayo pia jukumu lake ni kuua vijidudu na vitu vingine pia.

Kwa hiyo yote kwa yote Tumia Sanitizer Yenye Pombe na ndio maana unaweza ipaka tu peke ake na kuna baadhi ya watu wanatembea nazo wengine kwenye mikoba yao na kwenye gari zao.
Ila kwenye sabuni kitaalamu wanasema nawa na maji tiririka,kwa hiyo hapo ndio utaua kabisa na kuwaondoa hao virusi
 
Amani kwenu wanajamvi na poleni kwa changamoto za maisha yanayokumbwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo hili la covid19.

Twende kwenye mada.

Nimekuwa mfuatiliaji na baadaye mtumiaji wa hii kitu inaitwa sanitizer, katika kufuatilia nimeona hapo nyuma kabla hii kitu haijawa maarufu, baadhi ya sehemu wamekuwa wanaitumia kama kusafisha mikono kabla ya kula au huko hospitali.

Tukija kwenye janga la covid19 kuna swali kama siyo maajabu, huu ugonjwa tunaambiwa wadudu wake ni virus na siyo bacteria, ukifuatilia kwa umakini naambiwa Sanitizer ni kwa ajili ya bacteria!.

Sasa nini kinafanyika kwenye mdudu au virus wa corona kwa sanitizer wakati hiyo kitu inafanya vizuri sana kwa bacteria?

Ukisoma kipeperushi chake kinasema, Antibacterial "kills 99.9% bacteria"
Ni germs, sio bacteria, maana virus hufa kwa sabuni au Amfifiro iliyopo kwenye sabuni, pia virus hufa kwa alcohol ndio maana kuna sanitizer zole za spirits
 
Hapa kuna vitu viwili au vitatu vinavyotakiwa kuzingatiwa. Kikubwa ni namna gani hizi bidhaa sabuni na sanitizer zinazoweza kufanya kazi kumkabili kirusi.

Sio kweli kwamba sanitizer au sabuni humuua kirusi.laah hasha....bali sifa za kirusi na kemikali zilizopo kwenye hizi bidhaa ndizo zinazompatia kirusi ugumu wa kusurvive katika surface.

Kirusi ni particle iliyoundwa kwa protein na lipid (mafuta). Mafuta (lipid) ndio hutengeneza kasha la nje la kirusi.

Kama ilivyo sifa za alcohol..huwa na uwezo wa kudesolve mafuta. Kuna wakati hutumika kuchakuchanganya na rangi za mafuta kuifanya iwe nyepesi..kuyeyusha mafuta etc.

Sanitizer iliyoundwa na walau 70% ya alcohol inauwezo wa kuyeyusha kasha la mafuta la kirusi na kukikosesha kirusi nguvu ya kuwa na madhara. Hivi ndivyo sanitizer inavyofanya kazi kwa kirusi.

Sabuni mechanism yake ni tofauti kidogo. Sabuni zote za kufulia au kuogea zinafanya kazi ya kudhoofisha nguvu ya mgando wa uchafu kwenye surface. Angalia ukipaka greese mkononi. Ukinawa na maji pekee...bado greese itabaki mikononi. Ila ukitumia sabuni....zile molecules zinazokuwa zimeganda mkononi huwa weak na kuondoka kirahisi na maji tiririka.

Kwa kirusi hicho ndicho hutokea ukinawa na maji na sabuni. Nguvu ya kirusi kung'ang'ania mkononi hudhoofishwa kwa sabuni. Hivyo kuondolewa kirahisi na maji yanayotiririka.
 
Sawa mkuu nilivyoelewa tangu awali ni kuwa kazi ya sanitizer ni kuharibu muundo wa huyo kirusi hivyo kumfanya asiwe na madhara.
 
Mkuu Ginnwe kama nimekuelewa hebu ni dadavulie ni vipi kuosha condom na sabuni isiwe ni njia ya kupambana na kirusi cha ukimwi.
 
Virusi sio viumbe hai, isipokuwa ni kipande (molecule) cha DNA kilichoZUNGUKWA au kinacholindwa na mafuta mafuta mazitoo (fat) ambacho hunyonywa kwa urahisi zaidi kinapokutana na ile ngozi laini (mucous membrane) mfano, ngozi ya mdomoni, ndani ya pua, ndani ya macho au mkunduni.

Kirusi ni kitu kilaini sana kuharibika, isipokuwa tu haya mafuta yanayokizunguka ndio hukipa ulinzi na kiburi cha kusavaivu na kuishi popote kinapoangukia, kwa hiyo ili sisi tuweze kukiharibu hiki kirusi tunatakiwa tudeal na hili koti lake la nje ili kishindwe kuishi katika mazingira yetu haya ya nje kabla hakijaingia ndani.

BAADHI YA VITU VINAVYOWEZA KUMHARIBU KIRUSI KORONA

Sabuni/Mapovu (Amfifilo) ya aina yoyote ile yana uwezo mkubwa wa kuyeyusha mafuta haya yanayokizunguka kirusi endapo tu utakisugua sugua kwa muda walau wa sekunde 40 na zaidi ili kutengeneza povu jingi mkononi litakaloyeyusha yale mafuta mazito yanayokilinda kirusi, ndio maana tunaambiwa kunawa maji na sabuni kwa sekunde kadhaa.

Kitu kingine kinachoweza kuyeyusha lile futa zito linalolinda kirusi ni POMBE au mchanganyiko wowote wenye POMBE ya kiwango cha asilimia 65 na zaidi, tena hii ndo inayeyusha kiurahisi zaidi, sasa hapa wakulungwa wangu ndio tunakutana na kitu cha kuitwa KITAKASA MIKONO lakabu SANITIZER, ili kitakasa mkono chako kiwe sahihi kuweza kummaliza huyu dogo korona hakikisha kina POMBE(alcohol) zaidi ya asilimi 65.

SASA DOGO KORONA ANAKUFAJE AKIKUTANA NA SANITAIZA
Baada ya kufanikiwa kuliyeyusha lile futa zito ambalo ndio koti linalomlinda huyu dogo K, yeye kwake atakosa ulinzi na kubakiwa na DNA peke yake ambayo haiwezi kufanya chochote, yaaan kama wewe hapo sasa hivi tukuvue hyo ngozi yote halafu tukuache uende sokoni, nafikiri unaelewa itakavyokua basi ndivyo hivyo dogo korona atakavybaki na kushindwa kukudhuru wewe.

KUMBUKA; kile kitakasa mikono cha bacteria sio lazima kiwe POMBE ya kiasi kikubwa hivi.

Ndio mchango wangu mdogo katika hili, mnisamehe kwa uandishi na mapungufu mengine.

NAWA MIKONO KWA SABUNI (POVU JINGI) NA UPAKAE KITAKASA MIKONO
 
Nashukuru kwa swali...
Ni muhimu kusoma composition wa kirusi husika kabla ya kutafuta mbinu za kumuangamiza. Sina hakina na composition ya kirusi cha ukimwi ila naweza kugusia kidogo tu japo sio rasmi.

.kwa mbinu nilioieleza hapo juu..hili ni kitu kinachofanyika. Nakumbuka kunawakati jamii za wafugaji walikuwa wakifua na kuazimana condom huko vijijini.

Ila tukumbuke...condom inaundwa na materials ya plastic yanayotanuka na kuwekewa kilainishi ili kuzuia michubuko.

Unapoifua condom...unaweza kuitanua na kuifanya ikose uimara wake wa awali. Pia utapoteza kilainishi kilicho mahususi kwaajili ya kupunguza michubuko wakati wa tendo.

Japo kuna mbinu isiyo rasmi hutumika kuuosha sehemu nyeti kwa maji na sabuni ili kuua kirusi....
 
Hapa kuna vitu viwili au vitatu vinavyotakiwa kuzingatiwa. Kikubwa ni namna gani hizi bidhaa sabuni na sanitizer zinazoweza kufanya kazi kumkabili kirusi.

Sio kweli kwamba sanitizer au sabuni humuua kirusi.laah hasha....bali sifa za kirusi na kemikali zilizopo kwenye hizi bidhaa ndizo zinazompatia kirusi ugumu wa kusurvive katika surface.

Kirusi ni particle iliyoundwa kwa protein na lipid (mafuta). Mafuta (lipid) ndio hutengeneza kasha la nje la kirusi.

Kama ilivyo sifa za alcohol..huwa na uwezo wa kudesolve mafuta. Kuna wakati hutumika kuchakuchanganya na rangi za mafuta kuifanya iwe nyepesi..kuyeyusha mafuta etc.

Sanitizer iliyoundwa na walau 70% ya alcohol inauwezo wa kuyeyusha kasha la mafuta la kirusi na kukikosesha kirusi nguvu ya kuwa na madhara. Hivi ndivyo sanitizer inavyofanya kazi kwa kirusi.

Sabuni mechanism yake ni tofauti kidogo. Sabuni zote za kufulia au kuogea zinafanya kazi ya kudhoofisha nguvu ya mgando wa uchafu kwenye surface. Angalia ukipaka greese mkononi. Ukinawa na maji pekee...bado greese itabaki mikononi. Ila ukitumia sabuni....zile molecules zinazokuwa zimeganda mkononi huwa weak na kuondoka kirahisi na maji tiririka.

Kwa kirusi hicho ndicho hutokea ukinawa na maji na sabuni. Nguvu ya kirusi kung'ang'ania mkononi hudhoofishwa kwa sabuni. Hivyo kuondolewa kirahisi na maji yanayotiririka.
Case closed!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom