Mrengwa wa kulia
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 1,145
- 3,765
Historia ya vita haioneshi kwamba ni lazima mwenye nguvu ashinde.
Vipo vita vingi viliwahi kutokea ambapo mataifa yaliyoonekana dhaifu yaliibuka washindi.
Franco Prusian War ya 1870-1871 kati ya Ufaransa na Ujerumani ni moja ya mfano mzuri wa taifa lenye nguvu kutandikwa na taifa dogo.
Katika vitahiyo Chancellor wa Ujerumani kipindi hicho Otto Von Bismarck alimshauri mfalme wasikubali fedheha waliyokuwa wanafanyiwa na Ufaransa na wapambane kutetea utu na utaifa wao dhidi ya miamba ya kipindi hicho Ufaransa.
Hata hivyo katika hali ambayo si Ujerumani wala Ufaransa aliyetarajia, majeshi ya Ujerumani yaliibuka washindi na hatimaye kuwapora Ufaransa maeneo yao ya Alsace na Lorraine.
Vita ya Vietnam 1955-1975 pia iliacha fedheha kubwa kwa Marekani na Ufaransa.
Ufaransa ambao ndio walianza vita hiyo dhidi ya Vietnam ya kaskazini walionja joto ya jiwe na kutokomea kusipojulikana.
Marekani aliyejiingiza kichwakichwa kutaka kujaribu kuficha aibu ya Ufaransa na yeye alijikuta amekosea hesabu zake na kulala Yombo baada ya kupigana kwa takribani miaka 20.
Baada ya vita ya Vietnam kuliibuka kile walichokiita "Vietnam Syndrome" ambapo raia wa Marekani wanapinga nchi yao kujipeleka hovyo vitani.
Kwa muda mrefu sasa Marekani wamekuwa wakitengeneza filamu za kuuhadaa ulimwengu kuhusu kilichowakuta Vietnam.
Lakini pia kwa waliosoma Biblia kuna vita maarufu ya Daudi na Goliati imeelezewa ambapo Goliati mwamba aliyetarajiwa kushinda alikalishwa chini kwa kombeo la Daudi bwana mdogo ambaye hakupewa kabisa nafasi ya kushinda.
Umeshawahi kusikia habari ya watu wanne wenye ukoma waliotimua jeshi la Washami waliokuwa wameiteka Israeli?
Basi kwenye vita usikimbilie kusema sababu huyu ana nguvu lazima amshinde yule.Lolote linaweza kutokea.