Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Wananchi 6 kati ya 10 wanasema hawako huru kukosoa kauli zinazotolewa na Rais.
Idadi kubwa ya wananchi (60%) wanasema hawako huru kukosoa kauli zinazotolewa na Rais
wakati asilimia 54 wanasema hivyo kuhusu kauli zinazotolewa na Makamu wa Rais na asilimia
51 Waziri Mkuu.
Wananchi wanajisikia huru zaidi kuwakosoa viongozi katika ngazi za chini za serikali au viongozi
wenye mamlaka ndogo. Wananchi nane kati ya kumi wanasema wanajisikia huru kuwakosoa
mwenyeviti wa vijiji/mitaa (83%), viongozi wa vyama vya upinzani (77%), madiwani (76%).
Inavyoonekana, wananchi wanajisikia huru zaidi kuwakosoa wabunge wao kuliko wakuu wa
mikoa na wakuu wa wilaya. Hii inaweza kuwa ni kwa sababu wananchi wanawachagua wabunge
kama wawakilishi wao na hivyo wanaona kuwa mbunge ana jukumu la kusikiliza mahitaji na
vipaumbele vyao na kuvifanyia kazi ipasavyo. Vinginevyo, inawezekana wananchi wanaona kuwa
wakuu wa mikoa na wilaya wanaonekana wapo karibu na Rais.
Idadi kubwa ya wananchi wanasema ‘wanaamini kabisa’ taarifa zinazotolewa na Rais (70%) au
Waziri Mkuu (64%). Wananchi wengi wanaamini ‘kwa kiasi fulani tu’ taarifa zinazotolewa na
viongozi wengine huku taarifa zinazotolewa na wabunge wa vyama vya upinzani, wanachama na
wafuasi wake zikichukuliwa kwa tahadhari.

Source: Twaweza