Siyabonga - Robert Mangaliso Sobukwe: Simulizi iliyonitoa machozi

Nicodemas Tambo Mwikozi

JF-Expert Member
Aug 13, 2016
663
1,047
Mwaka 1952 Bunge dhalimu na la kibaguzi lililokua chini ya Makaburu Afrika kusini lilipitisha sheria ya kibaguzi, sheria hiyo iliyomtaka kila mtu Mweusi kuwa na kitambulisho kilichopewa jina la DOMPAS ID, kitambulisho hicho kilifanana na Hati ya kusafiria (passport)

Kitambulisho hicho (Dompas Id) kiliainisha jina la mwenye kitambulisho, jinsia, na Muda ambao mwenye kitambulisho hicho alitakiwa kukaa ndani Afrika kusini na Maeneo aliyoruhusiwa kutembelea.

Kitambulisho hicho kiliuzwa, Mtu mweusi alitakiwa kukinunua ,na kila baada ya miezi sita ili mtu mweusi aendelee kukaa ndani ya Afrika kusini alilazimika kukihuisha (kuki-renew) tena, kukosa kufanya hivyo angeonekana sio Mkazi halali wa Africa kusini hivyo angekamatwa na kuchukuliwa kwa kosa la MUHAMIAJI HARAMU.

Sheria hiyo maarufu kama "PASS LAW ACT" ya mwaka 1952 iliendelea kusisitiza kila mtu aliyekua na kitambulisho ilikua ni lazima kutembea nacho kama mtu hakua nacho alifungwa na kama alikua nacho ila hakutembea nacho pia alikamatwa na kufungwa.

Kwa kifupi sheria hii iliwafanya watu weusi na wana wa Afrika kusini kua wageni ndani ya nchii yao na makaburu kua wazawa, kwa majibu wa takwimu Zilizopo watu 250,000 walikamatwa na kufungwa kwa kushindwa kumiliki Dompas Id, au kwa kusahau kutembea nacho kwa waliokua wameshanunua vitambulisho hivyo.

Robert Mangaliso Sobukwe Mmoja wa viongozi wa Juu na mwenye ushawishi ndani chama cha Wapigania uhuru ANC ambaye badae alihama na kuanzisha chama chake cha PAC, ni kiongozi ambaye kwa Mujibu wa Taarifa zinaeleza Kuwa Sobokwe alikua Mtu hatari kwa ushawishi na mikakati na aliogopwa na makaburu zaidi kuliko Nelson Mandela kwa wakati huo, kiongozi huyu hakukubaliana na sheria hiyo ya PASS LAW Ya Mwaka 1952 ndipo alipokuja na mkakati ambao ulihitimisha udhalimu huo wa Dompas ID lakini pia Uhai wake.

Kwa kua sheria hiyo ilimtaka mtu mweusi asipokua na kitambulisho cha Dompas au asipotembea nacho kukamatwa na kufungwa , Tarehe 21 March 1960 Robert Mangaliso Sobukwe aliwaamuru watu weusi wote kutoka ndani ya nyumba zao bila kitambulisho cha dompas na waelekee polisi, ili polisi wawakamte na wawafunge watu wote weusi, wawauwe wote au wawafukuze wote kama wahamiaji haramu jambo alilojua kamwee haliwezekani maana hakuna gereza lenye uwezo wa kufungwa raia wote.

Siku hiyo watu walifurika barabarani kuelekea vituo vya polisi wakiimba nyimbo za kupinga udhalimu huo maandamano yalikua makubwa polisi na makaburu walichanganyikiwa wakaanza kuwapiga risasi waandamanaji ili kuzuia maandamano watu wengi waliuwawa kwa wapenzi wa somo la uraia au history shuleni tulifundishwa mauwaji haya kama sharpeville massacre.

Baada ya maandamano hayo kuzimwa na serikali ya Makaburu , Robert Sobukwe alijua atatafutwa, atakamatwa, na atauwawa hivyo hakutaka kujipa wakati mgumu wa kujificha jioni ya siku hiyo alienda nyumbani kwake eneo liloitwa Molofo akafanya utaratibu wa kuisafirisha familia sehemu iliyo salama (Kusikojulikana) kisha akaelekea kituo cha polisi kujisalimisha alipokua akielekea kituoni watu zaidi ya elfu tano walitembea nae kwa mguu kumsindikiza.

Baada ya kukamatwa alipelekwa mahakamani ambako alihukumiwa kufungo cha miaka mitatu Gerezani Sobukwe hakupinga kosa wala hakutaka kukata rufaa baada ya kuhukumiwa mwaka huo huo Bunge likatunga sheria ndogo ilioitwa "Sobukwe Clause" kifungu hicho kilimpa mamlaka waziri wa mambo ya sheria kumuweka kizuizini mwaka mmoja mmoja Sobukwe. hivyo baada ya miaka mitatu kuisha sobokwe aliongezewa mwaka mmoja kizuizini tena na hali ilindelea hivyo katika wakati wote alipokua gerezani mpaka mauti yalipomkuta mwaka 1978 kutoka mwaka 1960 lakini Kihalali angetoka mwaka 1963 hivyo sobukwe alihukumiwa na mahakama na Bunge.

Maisha ya Robert Mangaliso Sobukwe gerezani Robbin Island

Kutokana na nguvu yake kubwa ya ushawishi alilazimika kupewa Huduma Maalumu ya VIP akiwa gerezani kwanza alipelekwa gereza lenye ulinzi mkali ambalo tangu kujengwa kwake hakuna mfungwa yoyote aliwahi kutoroka
Pili hakuchanganywa na mfungwa yoyote, msanifu hodari wa majengo aliitwa kusanifu na kujenga gereza dogo maalumu kwa ajili ya Robert Sobukwe.

Gereza hilo lilizungukwa na uzio wa fensi 3 kutoka fensi ya kwanza kwenda ya pili kulikua na Mbwa walifundishwa na wakakwiva hawa walikua masaa 24 wakimlinda kutoka fensi ya mbwa kwenda ya tatu kulikua na askari waliokua wakimlinda masaa 24 .

Haki za Robert Sobokwe ndani ya gereza lake binafsi
1. Hakuruhusiwa kufanya kazi yoyote ile Bali kupumzika tuu
2. Aliruhusiwa kulala na kuamka muda atakaotaka
3. Aliruhusiwa kusoma magazeti
4. Hakuruhusiwa kutembelewa na ndugu yoyote
5. Hakuruhusiwa kuzungumza na mtu yoyote wala kusikia sauti ya mtu yoyote hata mtu aliempelekea chakula hakuzungumza nae akiwa na shida yoyote alitumia maandishi tuu.

Kisiwani hapo kulikua na wafungwa wengine ambao walimuona kwa mbali tuu na hawakuruhusiwa kumsalimia wala kumkaribia hivyo waliishia kumpungia mkono tuu. Wafuasi wa chama cha ANC waliofungwa kisiwani hapo Walipomuona kwa mbali walimpa ishara ya mkono juu na kukunja ngumi alijua hapo ni wafuasi wa ANC yeye hakunyoosha mkono bali aliniima na alichota mchanga chini kisha kuachia kuurusha juu akimaanisha "Hii ni Aridhi yetu lazima Tuipiganie "

Miaka sita ilipita bila kuzungumza na mtu wala kusikia sauti ya binadamu yoyote
Robert Mangaliso Sobukwe alianza kupata matatizo ya saikolojia yaliopelekea kuanza kua na matatizo ya akili kutokana na upweke mkali aliokua nao,

"kijana acha mzaha ukiachika na mpenzi wako kulialia na kupigia kelele watu ohoo am lonely nadhani kupitia Sobukwe umeelewa maana halisi ya Lonely " baada ya matibabu ya muda mrefu alihamishwa gereza mwaka 1978 arifariki dunia Zipo taarifa na imani zisizo rasmi kuwa Sobukwe aliwekewa sumu katika chakula akiwa gerezani katika kisiwa huko cha Robbin.

Robert Mangaliso Sobukwe kama Nabii Musa alivyoahidiwa na Mungu Ataiona nchi ya ahadi ila hataikanyaga vivyo hivyo kwa Sobokwe Alitamani kuiona kesho ya Afrika kusini ilio na haki, utu, usawa na isio na ubaguzi kwa mtu mweusi lakini hakuishi kuiona siku hiyo, Kwani siku hiyo ilichelewa kufika, miaka 16 baada ya kifo chake Africa kusini ilipata uhuru,

Sobukwe anabaki kua mbegu iliyokufa na kuoza lakini ikachipua na kuleta matunda mazuri ya uhuru haki na usawa baina ya mtu mweusi. Mwaka 2015 alipewa heshima ya kujengewa sanamu kubwa Pretoria, sehemu inayoitwa Fountains Valley, vizazi na vizazi viweze kumuona na kutunza kumbukumbu ya mpigania uhuru huyu shupavu aliepitia mateso makali.

Nikiwa katika utulivu na usikivu wa hali juu nilimsikia dada aliekua akituongoza akisema sasa tuelekee sehemu wafungwa walipokua wakifanya kazi za mikono ndani ya kisiwa cha Robbin, tukaanza kuelekea huko, ni katika eneo hilo nilijua wafungwa wa Robbin Island walipasua kokote katika mwamba wa Red Quarry na green Quarry kokoto hizi wakati wa mchana ziliakisi mwanga wa jua na kuwaumiza macho wafungwa kwani Hawakua na miwani wala vitendea kazi vyovyote vya kujali afya zao, miale hiyo ilikua na chembechembe za kemikali zilizokua na sumu kemikali hizo ziliawaathiri Macho,

Kwa miaka 27 ambayo Mandela alikua hapo kisiwani miale hiyo ya kokoto za kijani alimuathiri macho yake hali iliyosababisha kutotokwa na machozi katika maisha yake yote, hivyo mpaka Mzee mandela anafariki Chozi halijawahi kutoka katika macho yake iwe kwa furaha au uchungu. Kuhusu mandela nitaandika wakati mwingine.

Ukiingia uwanja wa ndege wa Capetown utakutana na msemo maarufu aliwahi kusema Mandela umebandikwa kwenye lango la kutokea msemo huo unasema
WHEN MAN HAS DONE WHAT CONSIDERED HIS DUTY TO HIS PEOPLE AND HIS COUNTRY HE CAN REST IN PEACE -SIYABONGA TATA MADIBA HAMBA KAHLE

Siyabonga maana yake "Asante" hamba kahle maana yake "kwa heri "

Robert Sobukwe Alitimiza wajibu wake, kwa watu wake, na nchi yake Apumzike Kwa Amani, Asante na kwa heri?

SIYABONGA - Robert Mangaliso Sobukwe


IMG_20200219_132010_145.jpeg
IMG_20200219_133026_139.jpeg
images%20(4).jpeg
IMG_20200219_133913_357.jpeg
IMG_20200219_133416_444.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhh makaburu waliua vipaji vingi sana,watoto wa Afrika wenye vipaji,uchungu na bara lao walizimwa mapema.
 
Wewe mlaini sana cha kukutoa machozi hapo kipi hasa?

Some pipo bana!!!!...me niko tofauti sana. Sijui sababu ya jeshi hili!!!

Matatizo ya kukimbia jeshi haya unaona!!!

Tundu lisu kapigwa hukulia acha unafiki.
Ila umajitahidi pamoja na yote
 
Back
Top Bottom