Siwezi kuwatenga. Nakuja tufanye tour ya kibabe Dar tukitumia "magari" na nyie ndugu zangu

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Habarini za Tanzania? Wadau nmekuwa kimya sababu nipo busy nchi za watu huku hawana masikhara wanapiga kazi hasa.

Wadogo zangu wanawasalimia maana nilipotoka Swedeni nikaenda Norway, Netherland then Canada huko wadogo zangu wamechukua uraia.

Wananishauri sana nami nichukue uraia wa Canada au Norway. Nawagomea hawanielewi kabisa.

Nikawaza sasa na mimi napaswa kuwa Mtanzania hasa hasa.nibadilike hata tabia. Nimepanga nikirudi Dar this time sitaki kujichimbia Oysterbay peke yake.

Nataka nifike maeneo ya watu wa kipato cha chini hasa maeneo haya nayasikia sikia sana. Maeneo ambayo watu wanaishi kwa milo mitatu tu kwa siku kutokana na umaskini.

- Sinza
- Tandale kwa Mtogole
- Tandale kwa Tumbo
- Kijitonyama
- Magomeni Mikumi
- Magomeni Mapipa
- Yombo Dovya
- Yombo Kigilagila
- Vingunguti
- Tabata
- Maji Matitu
- Ubungo
- Mabibo
- Buguruni Mnyamani
- Ilala
- Mbezi
- Mwenge

Baadhi ya maeneo nmekuwa nikipita tu ila sijangia ndani ndani. Napenda nipate wenyeji wanipeleke mpaka matako bar,nyegekeni bar.

Haya maeneo kuna dereva mmoja huwa ananitajia sana akitaka kunitembeza huko ila nmekuwa sipati muda.this time nmewaza nikasema inabidi nijumuike na waswahili wenzangu wanaoishi katika mazingira magumu.

Wadau mnisaidie tu kuwa napaswa kubeba nini na nini napoenda maeneo hayo.hili wazo nililipata jumamosi nlikuwa nmekaa na jamaa yangu Mc Gregory Bar flan hivi jamaa aliagiza kinywaji flani glass moja USD 500.

Mimi situmii alcohol so nikawa nimeagiza non alcohol drink chupa moja ni USD 700 kinywaji tulivu sana.basi ndo nikamkumbuka Ally siku moja tulikuwa tumekaa naye Lounge moja Dar ndani ya Hotel moja ya nyota 4.

Ally alikuja na rafikiye Fred.siku ile nlikuwa na cash 750,000 tupo watatu.jamaa walikunywa mpaka wakawa wanatapika.nikashangaa hiyo starehe ni ipi? Yaani kuna starehe gani kunywa hadi unatapika?

Si bora tu mtu angejitia vidole kooni kama alitaka kutapika.kwa aibu niliwapa tsh 300,000 wakagawane kwa ajili ya usafiri mimi nikaondoka.maana wahudumu pale walinishangaa haikuwa kawaida yangu kuwa na watu wa namna hiyo.

Nikiwa na Mc Gregory ndo nikakumbuka hasa baada ya yeye kusema glass mbili tu zinamtosha hanywi ili alewe ana kunywa kwa starehe tu.

Nawakumbusha ndugu zangu wa hayo maeneo tunywe kistaarabu tu haina haja ya kulewa na kutukana wahudumu au wanywaji wengine.

Nimepamiss Tanzania nakuja tufanye tour.mtaniambia kwa maeneo hayo tutumie Range Rover, BMW, JEEP, GMC au Benzi.
 
Vipi Like Gari Lako Kule Tabata

 
Back
Top Bottom