Siwezi kusahau nguvu ya hii pesa $(U.S. D)

Kakole

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,094
1,745
Ilikuwa mwaka 2009 miaka 7 iliyopita kipindi hicho nikiwa naishi kwenye jiji letu la raha Dar town, nilikuwa na jamaa yangu ambaye tulipata kufahamiana vzr na kuunda urafiki wa kiaina kwa sababu nilikuwa mteja wake mzuri wa biashara yake.

Sasa siku moja nikiwa nimetoka job nikiwa nimejichokea yule mshikaji wangu akaniona nikijongea kuelekea nilikokuwa nikiishi kwa kipindi hicho, alikua

amekaa bar ya jirani na nilipokuwa naishi, nikaitikia wito nilipofika pale jamaa akaniuliza unakunywa nini? nikamjibu natumia castle lager, palepale ghafla

castle 3 baridi zikaletwa, kwakweli mshikaji siku hiyo alichafua meza si
mchezo huku pembeni akiwa na mrembo mkali vibaya, alifanya utambulisho hlf tukaendelea na kikao chetu cha kukata mti na kupanda mti, baadae bill ikaja ya elfu 60 hivi jamaa akaniambia mkuu hebu ongezea elfu 20 hapo,

bahati mbaya kwenye wallet nilikuwa na dola 20 nikazitoa hlf nikamuuliza hii hela inaweza kukubalika hapa? bar medi akajibu kuwa hiyo pesa haitumiki pale, sasa yule mrembo ambaye ni shem wangu kwa mshikaji wangu yule ghafla akawa anakosentrate sana kuniangalia, mshikaji alipoenda chooni kupunguza maji na kwa vile simu yangu ilikuwa juu ya meza yule she akachukua simu yangu akajibp huku mimi sina hili wala lile,

baada ya jamaa kulipa bill tukaamua kuondoka kila mtu akashika njia yake, nikiwa nimekaribia ghetto mara simu yangu ikaita akajitambulisha kuwa yeye ni yule shem wangu kwa yule jamaa yangu akaniambia tukutane millennium tower, nilipofika pale akaanza kujitongezesha na kwa vile tulikuwa tungi basi ikawa uji kwa mgonjwa kiulainiiiiiii......usiulize nini kilitokea.........nguvu ya $ ni balaa.

enjoy your w'end, drink responsibly.
 
Ulipata faida gani kuharibu urafiki Kwa starehe ya dakika 10??
Soma vzr mkuu, demu alijipendekeza mwenyewe hlf hakuwa mke, ingekuwa ni mke lazima heshima ingechua nafasi yake
 
hii story kama sio ya kutunga, bac sidhani kama uyo dem alikupendea kwasababu ya hicho kidola 20 chako...bac tu alikuwa na hamu ya dyudyu yako
 
I will never ever https://jamii.app/JFUserGuide another man girlfriend especially a person i regard as a friend hata kama wataachana wanawake wapo wengi sana kujirahisisha kihivyo
 
Kila kitu kina nguvu inategemea na nyakati
wapo watu wamepata wanawake kwa simu za twanga pepeta
wapo wlio honga hadi unga au pipi tu
nyakati....acha kabisa....
kwani wanao hongwa magari now wanajiona wajinga?
nyakati zikifika ndo ujinga unaonekana
 
Haaa Haaa Kila mtu anahonga kulingana na Urefu WA kamba yake. Kuna watu wanahonga buku , buku mbili. It's depends on your earning potentialities.
 
Issue hapo sio 20 usd. Maybe katika kukaa kwenu na kuongea ongea Kuna vitu ulimvutia. $20 mkuu?
 
Issue hapo sio 20 usd. Maybe katika kukaa kwenu na kuongea ongea Kuna vitu ulimvutia. $20 mkuu?
Issue haikuwa $20 tatizo nilipotoa hiyo $ alijua ninazo nyingi kwenye wallet, hlf hakung'amua kuwa ilikuwa $20 alijua nina dola nyingi pale kumbuka jamaa alitaka niongeze elfu 20 mda huwo hlf exchange rate nakumbuka ilikuwa 1500 kwa dola moja kipindi hicho, kwahiyo ilikuwa hela ndogo mnoo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom