Siwezi kusahau maisha......

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Wana JF kwa hakika mwenzenu niko katika njia panda nakuombeni msaada.

Maisha yamekua tafu sana kila mtu analalamika ila kwangu yamezi tatizo ni kwa sababu yangu dini ndio inaniambia hivyo tazizo nimeshatubu na nataka nimuombe mungu aniondoshee hii hali ila najisikia aibu kwa makosa niliomtendea kumuomba msaada hasa ukizingatia kua nimeishi maisha ya kawaida ya kujikimu kwa muda mrefu leo miezi 3 tuu nielekee kwake nataka niwe na imani kama ya Ayuobu alioeumwa kwa muda mrefu hadi kuliwa na mafunza kwa kua alikua mzima miaka 40 basi alisema hamuombi mola wake hadi aumwe kwa miaka 40.

Kikwazo changu baadhi ya dhambi lilizofanya ni lazima niwaombe wanaadamu wezangu samahani na unaenda kumuomba hujui ulimkwanza vipi au atalipokeaje akikubali kukusamehe sawa jee akitaka kukupa adhabu.
Mfano kweli inawezekana kumuomba mtu samahani kwa kumchukulia mkewe jee akiamua kukuhukumu jee? Na yeye kapewa haki ya kukuhukumu ili upate msamaha au akusamehe inakuwaje wenzangu?

Mungu anasema.
Hakika ya dhambi haisahauliki na mlipaji hafi kiwango ulichomfanyia mwenzako nawe utafanyiwa hivyo hivyo.

Nisaidie wenzangu.
 
++
Dhambi inakutafuna?
Sema kweli Utue mzigo.
++
 
Nasikitika kua sitoiandika kwani mungu anasema
"Anaetenda dhambi kwa siri basi nami nitamuhukumu kwa siri ama nitamsamehe na anaetenda dhambi hadharani au akaitangaza kwa watu basi huyo hatopata msamaha wangu na nitamuhuku watu wote wamuone "
Kwa mnasaba wa ayya hio siwezi kuanika dhambi zangu
 
Ijapokuwa dhambi zenu ni nyekundu kama damu Yeye ana uwezo wa kusamehe na kukutakasa kuwa nyeupe kama theluji.Haupaswi kumwogopa mwanadamu,Ni Mungu tuu mwenye kutoa hukumu.Mtafute yeye atakuondolea maovu yako yote tena atakuepusha na kaburi.Hakika ulolifanya ni jambo jema tena kwa wakati unaostahili.Mrudie Bwana nawe utasamehewa makosa yako yote.Tena basi utasamehewa Duniani na hata mbinguni.Bwana akubariki sana.Enenda kwa amani.:kev:
 
Anza kutenda wema, ili zizidi maovu uliyofanya!
 
si ungemuomba tu mungu kisirisiri msamaha huko huko kwani lazima uje huku.......
halafu maelezo yako ni kama yanadetect hiyo dhambi uliofanya



 
Wee nenda tu na upanga mkononi. Akukusamehe shukuru Mungu, akikugeta pepo yako. Si ndo mnavyofundishwa!
 
Nijuavyo mimi mwanadamu huwa hana mamlaka ya kuhukumu, hence hatuna uwezo wa kusamehe dhambi zako.
 
Sasa si umfate huyo ulomkosea muombe msamaha uwe huru....ninavyoamini mimi kama umemtendea kosa mwenzio kuomba msamaha ni lazima ikiwa atakusamehe au hatokusamehe hiyo sio tatizo lako muhimu ushajisafisha kwa upande wako.

Huwezi ukawa umemdhulumu mwenzio halafu mungu akusamehe bila kumtaka msamaha ulomdhulumu.

Naamini dhambi baina yako na mungu ndo unasamehewa ukiwa ni msamaha wa kutorudia tena lakini kama kuna 3rd person involved haikuji hivyo lazima uombe msamaha ndugu

Onana na mkubwa wa dini akuelekeze jinsi ya kujisafisha.
 
Nijuavyo mimi mwanadamu huwa hana mamlaka ya kuhukumu, hence hatuna uwezo wa kusamehe dhambi zako.
Binadamu hahukumu lakini
kuomba msamaha kama umemkosea ndio inavyotakikana.

Nauliza mtu akiungama kwa mchungaji inasaidia nini..is it counseling tu or thru him ndo unasamehewa
 
Ungekuwa mkristo ingekuwa nafuu kisaikolojia. Unamfuata mchungaji wako, unatubu na kurudishwa kundini afu mambo mswano. Manake Biblia inasema nitakusamehe dhambi zako wala sitazikumbuka kabisa, halafu inasema kama mashariki ilivyo mbali na magharibi ndivyo zitakavyokuwa mbali na wewe . Hata ziwe nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kuliko theluji.

Onana na kiongozi wako wa dini akushauri style ya kutubu. Akiona unafaa kufungiwa jiwe shingoni basi nafsi yako itapona.
 
Nauliza mtu akiungama kwa mchungaji inasaidia nini..is it counseling so thru him ndo unasamehewa

Kipenzi mchungaji anachofanya ni ushauri na kumuongoza mtu namna ya kutubu...lakini mwisho wa siku ni mtu mwenyewe ndio atamconsult Mungu ampe msamaha kupitia toba ya kweli(moyo inabidi umaanishe kutubu).

Ila sisi kama binadamu tuna wajibu wa kusameheana pale tunapokosana. Hata Mwenyezi Mungu huagiza watu wake kuwa wenye kusamehe wenzao.
 
Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea....

Mimi na wewe sote twaongelea jambo moja.
Maana ya hicho kifungu ni kwamba ili usamehewe yakupasa nawe kusamehe kabla lakini haimaanishi mwanadamu anao uwezo wa kuondoa dhambi za mtu.
Laiti kama angelikuwa na uwezo huo sidhani kama kungekuwa hata na haja ya sisi kusogea mbele za Mungu na kutubu.
 
Hakika hiyo dhambi itaendelea kukutesa mpaka hapo utakapo amua kuutua huo mzigo kwa kutubu...!
Nenda kwa huyo uliye mkosea au kiongozi wako wa dini ukaungame hiyo dhambi ili nafsi yako iache kutapatapa.
 
Jikabidhishe kwa Mungu..,,mnyenyekee..Mlilie....atakusamehe 2 na kamwe usitangaze dhambi uloifanya kwa mtu..we mlilie Mungu ni mwingi wa Msamaha,,aman na faraja ipo kwake 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…