Siwezi kumsamehe milele, ameyaharibu maisha yangu pakubwa sana

Superleta

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
466
538
Habari za jumatatu wana MMU

Ni jumatatu nzuri ya siku ambayo taifa letu linaadhimisha siku ya uhuru

Nitaandika kwa ufupi mno kilichonisibu mimi hapa,

Mosi,mimi baada ya kuhitimu diploma katika chuo fulani hivi (sitotaja jina) na kuona changamoto za ajira nilirudi nyumbani na kufikiria kuanza kupambana nikaja na wazo la kufanya ufugaji wa kuku wa kisasa na kwa kua sikua na pesa na kukosa support nilianza kukomaa wenyewe

Familia yetu ni familia ya kikawaida kama zilivyo za kitanzania wazazi,na ndugu zangu walinipigania kwa nguvu zao zote huku wakishinda njaa na hata kushindwa kufanya mambo yao mengine ili tu niweze kufika angalau diploma...na mungu akalifanikisha hilo

Kutokana na kuamua kuanza kufuga nilifuga vifaranga wa nyama vijogoo na nikawakuza nikawauza nikapata pesa kidogo maana nilikua nao 20 tu

Nilipata pesa kidogo maana niliuza 14 maana hao ndo walipona hadi kukua na kupata pesa kidogo nikajiongeza nikanunua vifaranga wa malawi wa mwezi mmoja nilinunua vifaranga 25 basi bwana wakakua wakafikisha miez 5 wezi wakapita wakafanya yao maana hapo tayari walikua wanakaribia kutaga hili jambo nikikumbuka daaah siwezi kusahau hili

Wakuu naomba nifupishe kwamba baada ya kuona biashara ya kufuga imenishinda kutokana na wizi niliamua kuhamia kwenye vipodozi nikawa naagiza vipodozi kopo 5 au kumi mpaka 30 nauza kwa wateja kupitia kujitangaza kwa fb kiukweli hii biashara iliniinua kiasi fulani nikawa navaa na kununua hadi mahitaji kadhaa pale nyumbani siku mambo yamekua mazuri nikanunua hadi kitanda,godoro,tv,deki,sabufa na king'amuzi

Nilipanga kuja kuongeza elimu yangu katika chuo kikuu kimoja hapa dar

HAPA NDO MAMBO YANGU MIMI NA MJOMBA YALIPOANZIA NA NDO KIINI CHA KUYAANDIKA HAYA

Huyu ni mjomba yangu kabisa na yeye kiukweli tulikua na mashauriano mazur sana yeye na mkewe walikua wakija kwangu kunikopa kama elfu kumi au elfu 20 akiniahidi mwisho wa mwezi atanipa pesa yangu maana yeye kaajiriwa katika shule moja huko mkoani kama msimamizi wa wapishi shuleni na pia msimamizi wa stoo ya vyakula na mshahara wao ni nzuri tu nilikua namkopesha ananipa japo muda mwingine alikua akichelewa kurejesha deni langu

Niliomba chuo kikuu kimoja hapa dar na nikapata na ikawa natakiwa nije kuripoti chuo ukawa umewadia na hapa nilikua sina fedha za kutosha za kujikimu maana pesa ya mkopo huwa inatoka imechelewa hivyo niliangalia mfukoni nina laki na 40 ya ile biashara yangu ambayo ndo nilikua nimebakiwa nayo pesa nyingi ziliishia kwenye kuomba mkopo wa chuo,kuaply,kuchukua trascpt chuo nk...
Niliomba kwa ndugu zangu wengi wakawa hana dadangu alikua kajifungua lakin kutokana na kuhisi hali yangu na kunionea huruma akanipa shilingi laki moja jumla nikawa na 240k sasa niliamua kuuza vitu vyangu vya ndani kama tv,deki na kingamuzi ili nipate pesa ya kuanzia maisha dar

Wakati nikijiandaa kutafuta mteja haraka haraka mjomba angu alijitokeza na kunambia kuwa atanunua vitu vyote hivyo na hela atanikabidhi cash baada ya siku 5 na akanambia anategemea mshahara utakua umetoka maana zilikua zimebaki siku tano kabla ya mwisho wa mwezi
Alizidi kunihakikishia hilo kwamba nimpe hivyo vitu kwasabab tayar nilikua nimeshapanga kuwahi kuripoti chuo ili walau nikapate chumba cha kupanga maana ukishachelewa tena haiwi rahisi kupata

Tulikubaliana vitu vyote hivyo tv ya inch 21 singsung flat chogo,deki mpya ya singsung,na kisimbusi cha startimes vyote vitatu tulikubaliana anipe laki na 50

Kwa kua alikua ameshaniahidi ilibidi nimpelekee hivyo vitu kwake na mimi nilikua nimepata namba ya dalali mmoja wa maeneo ya karibu na chuo nilichotarajia kwenda
Nilimuuliza kama naweza pata chumba cha 40k nilimuomba sana akanitafutia na nikapata kimoja hivi nilimuomba kodi nitatoa miez mitatu kwanza na akanambia nijitahidi niwahi kuripoti maana nikichelewa nitakikosa maana hicho cha 40 kilikua kimebaki kimoja

Nilimsubiri mjomba anipe hiyo pesa niweze kuondoka ndani ya siku 5 alizoniahidi alinambia hajapata na tayar vitu nilishamkabidhi

Nilisubiri kwa siku nyingine tano sasa hapo nikachoka akasema kuwa kuna mtu atampa hiyo pesa hivyo niende tu dar kesho nikifika tu nikashukie kwa mwanae then atakua ameshanitumia alinambia hilo mbele ya familia yake na kuniomba nimwamnini kwani ni uhakika

Kesho yake nilifunga safar ya dar kutoka huko kwetu kaskazini nikakata ticket naul 30000 kutoka kwenye zile pesa zangu

Cha ajab nimefika dar nikampigia mwanae ili nimwambie nimefika ubungo hakupokea simu na nilipga mpaka nikachoka nikaona niende tu gest sikua na namna nikampgia mjomba ili nimwambie kilichotokea na anitumie pesa yangu kesho ili nikamtafute dalali ili nilipe chumba mjomba hakupatikana

Kesho yake huyo mwanae alipatkana akadai hana sehemu ya kunilaza maana rafiki yake kaja ghafla na hawezi kumfukuza

Nilimpigia mjomba nikamueleza nikamuuliza mbona hajatuma hela???

Alinambia hajapata na niwe na subira niliumia sana kwasababu mtoto wake tumekua tukishirikiana sana hata alikua akituma mizigo ya nyumbani kwao naenda kuipokea mimi wakati mwingine hadi mizigo nilikua nikipewa nikimtumia kwa bus nililia sana hakika na pia mtoto wake ni mtu tayar anayo hadi maduka na biashara zake nakumbuka nilimuomba hata anikopeshe hiyo 150 nikalipe kodi babake akituma hiyo pesa nimpe hakujibu msg alisoma tu watssap na kuipotezea

Nilikaa gest siku nne wakuu nilikua tayar nimeshapata hasara gest nilikua nishapoteza pesa nyingi hadi wahudumu wa gest walinionea huruma

Nilimpigia mwenye chumba dalali akanambia nimechelewa sana kwani vyumba vya 40,50,na 60 vimekwisha chukuliwa

Nimesota sana mwishowe alikuja kunitumia elfu 50 tu ikabaki huko laki ambayo mpaka leo hajanipa

Nilikua nimeshakwisha sina pesa tena kuna jamaa mmoja alinionea huruma akanambia kuna chumba g.mboto kodi elfu 25 niende niongee na mwenye nyumba nilikuja kuzungumza na mwenye nyumba akakubali nikampa hiyo 50 miezi miwili

Hapo na chuo kuna direct cost nilijikuta nimebakiwa na buku mfukoni

Mjomba hakukosa hiyo pesa katu maana mshahara anapata karibia laki 3 na 50 na pia huku dar watoto wake wawili wana pesa na hutuma kwao kila mwezi

-alinisababishia hasara kubwa sana ambayo siwez kuifidia

-alinifanya niishi huku napoishi kwa sababu ya kukosa chumba na hostel

-amenirudisha nyuma hatua 50

Ameivuruga mipango yangu yote

Naumia sana ndugu zangu na sitomsamehe milele kwa hili moyo wangu unaumia hali yangu ya kulala gest iliniumiza sana hadi nakumbuka niliandika uzi humu wa kuomba nikopeshwe 50 au 100k kwa kipindi kila niliandika hadi uzi huu
Kipindi kile daaah

Nikikumbuka naumia sana nilivyojitoa kwa family yake kuwasomesha watoto wake wengine masomo nyumbani bure kumsaidia akiwa hana leo hii ni wa kunifanyia hivi na watoto wake?

Kwa sasa ni kama ndo naanza maisha upya tu niliugua week nzima yeye na watoto wake ambao tulisaidiana wakat toka utotoni hakuna cha simu wala msg ya pole
Bado namdai laki moja

Ila kiukweli alichonifanyia sitamsamehe machozi yangu mungu atamlipa.....

Mrejesho:Nilikwishamsamehe.
 
Samehe, sahau na endelea na maisha yako. Nilishajiapiza namna hiyo lkn baadaye niligundua ni ujinga, na wala haiongezi wala kupunguza kitu. Basi nikasamehe, kisasi ni kazi ya Mwenyezi Mungu

Mjomba hakukosa hiyo pesa katu maana mshahara anapata karibia laki e na 50 na pia huku dar watoto wake wawili wana pesa na hutuma kwao kila mwezi

-alinisababishia hasara kubwa sana ambayo siwez kuifidia

-alinifanya niishi huku napoishi kwa sababu ya kukosa chumba na hostel

-amenirudisha nyuma hatua 50

Ameivuruga mipango yangu yote

Naumia sana ndugu zangu na sitomsamehe milele kwa hili moyo wangu unaumia hali yangu ya kulala gest iliniumiza sana hadi nakumbuka niliandika uzi humu wa kuomba nikopeshwe 50 au 100k kwa kipindi kila niliandika hadi uzi huu
Kipindi kile daaah

Nikikumbuka naumia sana nilivyojitoa kwa family yake kuwasomesha watoto wake wengine masomo nyumbani bure kumsaidia akiwa hana leo hii ni wa kunifanyia hivi na watoto wake?

Kwa sasa ni kama ndo naanza maisha upya tu niliugua week nzima yeye na watoto wake ambao tulisaidiana wakat toka utotoni hakuna cha simu wala msg ya pole
Bado namdai laki moja

Ila kiukweli alichonifanyia sitamsamehe machozi yangu mungu atamlipa.....
Pole. msamehe ili upate baraka nyingi kutoka kwa Mungu baba
 
Mjomba ni mama yako, futa picha ya mjomba wako weka picha ya mama yako mzazi halafu itazame kwa upya kwamba aliyekufanyia hayo ni mama mzazi.

He bado moyo utajazwa chili hata kama ni mama mzazi?? Kama ndivyo sina neno Ila ukiona moyo unalegea sababu ni mama samehe na songa mbele ila usijitenge nao na usiwashirikishe mambo yako, pambana uje kuwaalika kwenye graduation yako.
 
watu wanakazana samehe samehe ila nadhani hayajawahi kuwakuta,aisee kibongo bongo mchawi namba moja ni ndugu!!binafsi sikushauri umsamehe ghafla tu,take ur time,ila wewe mpotezee tu weka akili kwenye masomo,mshukuru Mungu kwa yote ila bado unapumua!!
 
bado ukifanikiwa Chuo ndio wa kwanza kuja kujichekesha
na ukifanikiwa maisha watahamia kabisa kwa vinyimbo na vijembe
bora samehe na piga chini Mjomba
 
Back
Top Bottom