Kwa nini vuguvugu la M4C halina mashiko kwa wa Tanzania? CHADEMA inapenda saana kushika dola kwa hali na mali. Lakini haijajiweka sawa kwa watanzania hasa katika mambo makuu manne.
1 nini itikadi ya CHADEMA?? Wakati hiki chama kinasajiliwa kilisema ninafuata itikadi ya kibepari na ndo maana kikapata urafiki wa conservative party na hatimaye uanachama wa conservative union lakini majukwaani chadema inaimba sana siasa za ujamaa yaani egalitarian
2 kwa nini CHADEMA ilibadilisha bendera yake na kuweka rangi nyekundu?? Nini maana ya hii rangi kwetu sisi Watanzania??
3 kwa nini haitoi mbadala wa mambo ya kuleta maendeleo badala yake ni kulaumu tu kila jambo hata kama viongozi wenyewe wa CHADEMA ni matunda wa hayo wanayoyabeza.
4 kwa nini ushabikia kila uasi ndani ya nchi, ina maana hata chadema ikishika dola itabariki vurugu za kila aina ndani ya nchi??