Siwalaumu Wananchi...

Siwalaumu Wananchi...

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Juzi nilipita hapa na andiko juu ya utendaji usioridhisha utendaji wa mazoea business as usually kwa ofisi ya Msemaji Mkuu wa serikali: kurugenzi idara ya habari Maelezo.

Baada ya Rais kukamilisha ziara ya Dubai ilitoka taarifa ofisi ya DPC kitengo cha mawasiliano ya Rais Ikulu kwa kile nchi ilichonufaika nacho toka falme za kiarabu.

Kwakuwa Vijana wetu tumewapa Elimu ni wadadisi ofisi ya msemaji ilitakiwa kuaanda taarifa maalum ziara ya Rais Falme za kiarabu mikataba 36 na Trilioni 17 si haba na ajira zaidi ya 200,000.

Hata team Join the chain hapa waliamini Mama amelamba karata dume. Ukweli uliowazi kama kawaida msemaji wa serikali alienda kulala usingizi wa pono post mbili tatu za mitandao ya kijamii kwake kazi aliona amemaliza.

Pinde Watu wapo Dubai wanaona bendera ya Taifa inaangaza katika jengo la Burji Khalifa wenye kujua kwingi wanaleta tathimini zao na kuhoji imekuwaje tuwe pale?

Hili ni Jukumu la Ofisi ya msemaji wa serikalì na ofisi yako kuleta maelezo kina ya mambo na kwa kile kinachofanywa na Serikali.

Kwasasa Serikali imekuwa defensive inajibizana na Join the chain jambo lililohitaji Dkt. 10 kuondoa ukakasi. Haikugharimu kitu kuchukua muda wako na kufafanua mazuri ya ziara ya mheshimiwa Rais.

Angalizo ishara ya unayoyatenda ni uhujumu kwa serikali ya awamu ya sita.
 
Mwekezaji gani atakuja kwa sera mbovu za kubadilika badilika? unategemea CCM watakiri kuwa wanalipia tangazo 200m per day wana kichaa?
 
Ukiona hivyo ujue kuna mengi sana tunafichwa wananchi..wapigaji wametaradadi..ndio wapo jikoni wazee wa mikataba..mnakuja kushituka mbuga za wanyama sio zetu..migodi sio yetu..n.k

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom