Wakuu swala ya Middle East ni tete sana.Sisi inakuwa vigumu sana kuwaelewa hawa ndugu wa Mashariki ya Kati.
Kwanza hawa wote ni ndugu wa asili moja na itikadi zinazolingana.Tusijejidanganya kuwa waIsraeli ni waKristo na waPalestina ni waislamu ndio maana wanapigana la hasha.
Kwanza waIsraeli ni Wayahudi na wengi hawautambui Ukkristo.
Pili suala la Uyahudi, Ukristo na Uislamu usichanganywe, kwa kuliona suala la mashariki ya kati.
Tatizo kubwa pale ni ARDHI, pure and simple.
Wayahudi waliondoka Israeli miaka mingi iliyopita, wakarudishwa pale baada ya vita kuu ya pili. Waingereza wakifikiri wanawahurumia sana wakawarudisha pale kwa wingi.
Hapo mahala hapakuwepo ombwe, walikuwepo waPalestina, wakafukuzwa-sasa hawa waende wapi?
Wapalestina wamekuwa katika makambi ya ukimbizi nchini mwao na katika nchi ya Jordan na Syria.Kosa lao nini.Mbaya zaidi baada ya vita ya 1967 ardhi zaidi ya waarabu ikatekwa ingawaje Misri iliingia mkataba kurudishiana ardhi hiyo.
Masikini waPalestina hawana mtetezi, Israel inayo Marekani.
Hvi vitimbi vya Hamas ni vya mtu aliyechanganyikiwa maana hata nchi hana, sana sana sehemu ndogo ya kujidai ambayo haitambuliwi kama Taifa.
Deep frustration na resentment ya jumuiya hizi mbili ndicho kinachoonekana sasa.
Hizi jamii zote mbili waIsraeli na waPalestina ni watu wa visasi, watu wa jino kwa jino.
Tusisahau kuwa Kurani na Torati(karibu sawa na Agano la Kale) ni vitabu vinavyolingana sana.
Jamaa zetu hawa hakuna kitakacho wasuluhisha , pengine mpaka Yesu arudi tena!