Siwaelewi Engineers wa Tanzania, hasa Civil Engineers

Siwaelewi Engineers wa Tanzania, hasa Civil Engineers

Ni idea nzuri ila unakuta wakati mwingine unapotaka wachepushe ni ardhi ya mtu. Unajua hizi barabara zilikuwa designed na kutengenezwa zamani. Kwahiyo traffic ya magari haikuwa kubwa. Hizi ni barabara zipo tangu enzi za ukoloni.

Kuhusu barabara kujengwa na wageni si kwamba wahandisi wa hapa hawana ujuzi..makampuni ya kigeni yanakuwa na pesa ya.kuweza kujenga mradi tofauti na kampuni za kitanzania.Hata hivyo bado hayo makampuni ya kigeni yanatumia wataalamu wakitanzania kutekeleza hiyo miradi. Mara nyingi unapoona mambo yameenda isivyo so tatizo la utaalamu ila ukiukwaji wa maadili ya kazi kwasababu ya njaa ya watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa idara ya UANDISI ni mtaalamu P.R. badae akasoma post graduate ya Education. Anamalizia master yake ya.....(why). Nchi yetu huko nyuma ilikuwa inabeba undugu zaidi).

}|~
 
Habari ya week end wakuu.

Kwanza naomba kukiri kua kusomea uinjia wowote ninkazi ngumu sana.

Ila mimi binafsi hua siwaelewi mainjinia wa kitanzania hasa civil engineers, hawa wanaohusika na ujenzi wa mabarabara na majengo.

Sijui ni uwezo wao wa kufikiri mdogo au wana matatizo gani, sina wamshaka ndio maana miradi mingi ya ujenzi ya kuvutia na kupendeza inajengwa na wakandarasi wa nje ya nchi.

Tatizo langu hasa liko kwenye barabara hasa za Dar es salaam na mikoa mingine, hawa civil enginerrs sio wabunifu kabisa, hawafikirii mbele na hawaoni picha nzima ya miradi yao ya hovyo wanaoijenga.

Nimeweka sketch map ya Barabara ya Chang'ombe kama mfano kuonyesha jinsi gani nawadharau hawa watu. Mimi sio injinia ila wangeniuliza mimi ningefanya vizuri kuliko wao.

View attachment 584605
Kwa nini gari inayotoka Tazara, lazima ifike point X ndio iende Ilala na Magomeni, kwa nini wasingechepusha njia kwenye pont A gari zote zinazoenda Ilala au magomeni zipite hapo na zisifike point X kisha ziende Ilala

Like wise gari za kutoka Posta au Kariakoo kwenda Chang'ombe na Temeke kwa nini zifike point X kisha ziende Temeke, kwa nini wasingetengeneza barabara ya kuzipitisha hapo kwenye point C.

Vile vile zinazotoka Ilala kwenda posta, kwa nini zifike point X ambapo ni makutano, kwa nini hawakutengeneza barabara hapo point B.

Foleni nyingi Jiji la Dar zimesababishwa na poor construction and designing toka kw ahawa mainjinia wetu. Hata mtu asie injinia anaona kabisa hawa watu hawako sawa.

Kwa kweli mimi nachelea kusema kua nawadharau sana. Mtanisamehe kw ahilo.
1) Siku ingine ukichora mchoro kama huu jaribu kuweka mwandiko unaoonekana. Maana inawezekana nawe umefikiria kwa upeo mdogo zaidi kua kila mtu anaweza kuusoma mwandiko wako kisha unawalaumu ma engineer.

2) Ramani yako imepinda, hata maandishi yamepinda. Pia pendelea kuchora kwa kuangaliaau kugeukia kaskazini. Ndio stadnard za uchoraji wa ramani zilivyo

3) Kuna sehemu ni viwanja vya watu, Mfano ukitoka Posta/Kariakoo kukunja kwenda Chang'ombe ni Petro Station ya mtu. Hata kutokea Chang'ombe kuelekea tazara pale kona pana petrol station ya mtu, utafanyaje sasa??

4) Hata ingekuwepo njia ya mchepusho kutokea Tazara kwenda ilala still bado kungekua na utata maana magari hayo yangekuja kukutana tu na yale yanayotokea Chang'ombe kunyooshea Ilala. yakikutana hapa yote yanaelekea ilala nani angekua na haki??
 
Inawezekana ukawa na point but elewa,engineer ni mtendaji anayefuata maamuzi ya wanasiasa,kuna drawings ambazo anazitumia na kushauri pale inapobidi,na hawa wanaoandaa hii michoro "consultant"...huwa wanapewa scope of work ambayo pia hutegemea vitu vingi sana kikubwa ikiwa ni funds,sasa kama maamuzi yanafanyikia halmashauri,huyu engineer ataonekana hewa lkn, kiuhalisia sio,tanzania tuna waandisi wazuri saana,sema they'r under utilised!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekosoa design bila kuhusisha professional inge sound good, kwa mfano umbunda wa bashite ziro brain usiufungamanishe na fani ya uzazi.
Sana sana unaweza kuwa question dingi na maza wake tu!
 
Duuh aisee miundo mbinu ya enzi za Nyerere hadi leo haijarekebishwa tu?
 
Inawezekana ukawa na point but elewa,engineer ni mtendaji anayefuata maamuzi ya wanasiasa,kuna drawings ambazo anazitumia na kushauri pale inapobidi,na hawa wanaoandaa hii michoro "consultant"...huwa wanapewa scope of work ambayo pia hutegemea vitu vingi sana kikubwa ikiwa ni funds,sasa kama maamuzi yanafanyikia halmashauri,huyu engineer ataonekana hewa lkn, kiuhalisia sio,tanzania tuna waandisi wazuri saana,sema they'r under utilised!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huyo jamaa anausikia tu uhandisi kwenye bomba.
He has no idea what it means in real life.
 
Kuna kituko kingine kuko Barabara ya kutoka mwananyamala kwenda Magomeni, hapo studio kuna makutano ya barabara.

Baada ya kuzindua barabara ya mwendo kasi, kama unatokea mwananyamala, uende mbele kidogo baada ya kuvuka taa, ugeuke kisha ndio uunganishe kwenda magomeni au mkwajuni.

Sijui kama wamerekebisha hilo tatizo ila ule ni ujinga na ukosefu wa ubunifu
Kuna taa sasa hivi zinaruhusu ukitoka m'nyamala unakata kulia kwenda magomeni.
 
Hivi hapo hata ikichepuka hiyo gari inakua umesolve kitu gani ikiwa inalazimika kusubiri gari inayonyoka ipite or izuie gari inayonyoka...Solution ni kuongeza idadi ya barabara tu na sio kuchepusha maana ikifika mbele na kutaka kuingia barabara kuu bado italazimika kukaa foleni kusubir magari yanayonyooka ndipo aingie
 
Kwani barabara hyo ilikuwa planned mwaka jana au juzi? Ni barabara ilikiwepo tokea enzi za nyerere, wewe unachokitaka ni simplicity ya route zake, n kuna kitu kinaitwe traffic calming, tukifupisha barabara tutakosa junctions,tutasababisha foleni.Na si kweli kuwa maengineer wa Tanzania ni wazembe,hata ukiangalia engineering fields zingine hapa bongo wapo hivyo hivyo, we plan according to future requirements and present resources....Hujui how highway design inafanywajena pia pamoja ya kuwa sketch yako haipo sawa,Uzi wako umekosa kitu kimoja tu,je siasa iliingiliaje design ya barabara hiyo?
 
Back
Top Bottom