Siwaamini tena CCM, ni waongo

Siwaamini tena CCM, ni waongo

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,180
Uwongo wao unaonekana wazi wazi mbali ya vitendo vyao hata kauli zao, hawa si wa kuwaamini. Huyu Polepole aliapa na kuwaambia wananchi wasiipe kura CCM au wasiichague CCM na hawa waliofikia hadi kuwa mawaziri na kufika kugombea uraisi wote walisema na kuapa kuiswaga CCM, leo wote wamerudi.

Una sababu gani ya kuwaamini wagombea wao wa uchaguzi? Mwaka huu ni kuwapiga na chini tu.

Jamaa waongo sana na mahodari wa kupangilia. Utawaona wanazungumza kwa makeke kama wanauwa drakula lakini wanayoyasema ni uwongo uliovuka mipaka.
 
Ila Rais wa sasa ndio amezidisha sana Uongo.

Anaishi kwa Neema ya uongo

"Nitatoa milioni 50 kwenye kila Kijiji kwa ajili ya kuwakopesha wananchi ili wajikwamue kiuchumi"

Baadae kauli ikabadilika "Milioni 50 zimepelekwa kwenye Vijiji kupitia huduma za kijamii kama elimu bure, madawa, umeme, nk"
 
Uwongo wao unaonekana wazi wazi mbali ya vitendo vyao hata kauli zao, hawa si wa kuwaamini. Huyu Polepole aliapa na kuwaambia wananchi wasiipe kura CCM au wasiichague CCM na hawa waliofikia hadi kuwa mawaziri na kufika kugombea uraisi wote walisema na kuapa kuiswaga CCM, leo wote wamerudi.

Una sababu gani ya kuwaamini wagombea wao wa uchaguzi? Mwaka huu ni kuwapiga na chini tu.

Jamaa waongo sana na mahodari wa kupangilia. Utawaona wanazungumza kwa makeke kama wanauwa drakula lakini wanayoyasema ni uwongo uliovuka mipaka.
Miaka 60 Chama hicho kimekuwa madarakani bado ulikuwa hujatambua kuwa hata huo uongo unaongezeka kila Uchaguzi kuupiku uongo uliotumika kupata ushindi wa kishindo wa Awamu iliyopita ndo maana Serikali zilizopita zinasahaulika kabisa. Awamu hii imevunja rikodi kwa uongo wa utekelezaji wa miradi utadhani Awamu zilizopita hazikuwepo kabisa au hazikutekeleza miradi yoyote ya maendeleo ingawa miradi yote inayoonekana na kuhesabika ni ya huko nyuma.
 
Kula baada ya fiesta ya CCM lazima Hali kama hii utaikuta kwenye eneo la.tukio
FB_IMG_1601899612959.jpg
 
Lumumba pale kuna kiwanda cha fix. Usimwamini mtu yeyote kutoka Lumumba, kufanya hivyo basi kama si wewe basi utaumiza kizazi chako kijacho. hawa ni wa kuogopa kama ukoma.
 
Kuna mmoja alisema huyu kala maharage ya wapi?? Leo nae anagombea.
 
"Nitatoa milioni 50 kwenye kila Kijiji kwa ajili ya kuwakopesha wananchi ili wajikwamue kiuchumi"

Baadae kauli ikabadilika "Milioni 50 zimepelekwa kwenye Vijiji kupitia huduma za kijamii kama elimu bure, madawa, umeme, nk"
Hayo madawa yangekuwepo sawa. Unalikumbuka like igizo la kuanzishwa kwa duka la dawa la msd pale muhimbili???
 
Kuna mmoja alisema huyu kala maharage ya wapi?? Leo nae anagombea.

Ilikua Arusha 2015 wakati kama huu kwenye mkutano mkubwa wa kampeni. Alipewa nafasi ya kutoa neno! Ni wakati huo ndipo alikuja na ule msemo wake wa "Asiyemtaka Lowassa, akale malimao"

Ila baada tu ya ile clip yake mauno kuvuja, naona kidogo akaanza kunywea! Ghafla tunashangaa akianzia kuisifia serikali ya awamu ya tano! Na leo hii eti ndiye anayepeperusha bendera ya chama pale Kawe! Wizi mtupu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom