Sitta: Waziri Simba kalikoroga

Mkuu Shaycas
Hapa hatumjadili Sophia Simba kama Mwenyekti wa UWT ya CCM,tunamjadili kama Waziri...haina mahusiano na ujinsia wake.

haya mambo ni Logic tu, kama wanawake wote viongozi wamemchagua awe mkuu wao then wao ndo hawawezi, didnt they saw her as extremely low minded? ana majungu, kusema sema ovyo,nahisi hata ngumi anarushaga yule!so ni failure ya wanawake pia, si tunataka kama wanataka usawa leteni watu bora mbele!
 
Ndugu zangu,siasa za Tanzania haziangalii Capacity ya mtu hapa namaanisha uwezo wa kiakili.Kinachozingatiwa ni je mtandao wako ukoje!jina lako likoje!ndio maana hatuna Viongozi ambao ni Think Tanks...Unapewa dhamana ya kuongoza Wizara au taasisi fulani si kwakuwa una uwezo bali kwa vigezo vingine kabisa..Sophia kuwa Mwenyekiti wa UWT haimanishi kwamba yeye ndio the best,nadhani mnazitambua siasa za nchi hii,mara nyingi ni hovyo sana..wapiga kura nao ni hovyo pia,hawaangalii uwezo wa mtu wanayakwao wanayoyataka,ndivyo ilivyokuwa kwa Sophia alipogombea UWT.
 
na Martin Malera

"Hata kama muswada huu ungeenda kwenye kamati yoyote bado usingepita kwa jinsi ulivyoletwa na sijui Waziri anayepeleka kitu kama hiki amefikiria vizuri maana ni wa hatari kweli," alisema Spika Sitta.

Kwa mujibu wa Sitta, muswada huo unapaswa kufanyiwa marekebisho na kama watauona haufai, wanaweza wakauacha kabisa kwa sasa.

Mimi siko kumlaumu SS wala spika ila ninachotaka kusema ni kuwa angalau sasa bunge limeanza kufanyakazi yake kwa angalau asilimia 20 (20%) ya vile linavyotakiwa kuwa

Haya tunayoyaona toka bungeni yalikuwa nadra sana kutokea siku za nyuma mambo yalikuwa yakimalizwa nyuma ya pazia na kamati za CCM kabla ya kuletwa kupigwa muhuri tu bungeni.

I like this: sijui Waziri anayepeleka kitu kama hiki amefikiria vizuri and this; kama watauona haufai, wanaweza wakauacha kabisa
 
Mimi siko kumlaumu SS wala spika ila ninachotaka kusema ni kuwa angalau sasa bunge limeanza kufanyakazi yake kwa angalau asilimia 20 (20%) ya vile linavyotakiwa kuwa

Haya tunayoyaona toka bungeni yalikuwa nadra sana kutokea siku za nyuma mambo yalikuwa yakimalizwa nyuma ya pazia na kamati za CCM kabla ya kuletwa kupigwa muhuri tu bungeni.

I like this: sijui Waziri anayepeleka kitu kama hiki amefikiria vizuri and this; kama watauona haufai, wanaweza wakauacha kabisa

Hii ni faida ya kuwa na strong opposition..haya ni matunda ya kina Dk Slaa,Zitto na wengineo wa Upinzani.
 
Mpaka sasa sijaeleweshwa huu muswada ubovu wake ni nini.

Kama national security council mbona mpaka US wanayo, tatizo hasa ni nini? Kumpunguzia madaraka rais?
 
..huu mjadala usije ukawa muendelezo wa malumbano yaliyotokea ktk kamati ya CCM inayoongozwa na Raisi Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

..naona Mwanasheria Mkuu anaelezea kitu tofauti kabisa na jinsi waandishi wa habari wanavyoeleza.

..tatizo hakuna waandishi wa habari walio-specialize ktk masuala ya Bunge kuweza kuuchambua mswaada na kuuelimisha umma.

..

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JAJI WEREMA AUNGA MKONO MSWADA WA SIMBA KUMPUNGUZIA RAISI MADARAKA.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema amesema kuwa anaunga mkono muswada wa Sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa wa mwaka 2009 akisema si mbaya.
Muswada huo, uliowasilishwa Jumamosi iliyopita na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba, ulikataliwa na Bunge kwa hoja kuwa unapunguza nguvu za rais na unamweka rais katika hatari ya kuondolewa wakati wowote na Baraza la Usalama.

Lakini Jaji Werema alisema jana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuwa haoni ubaya kwenye muswada huo.

"Muswada si mbaya, lakini umerejeshwa kutokana na wabunge kutaka baadhi ya vipengele, hasa cha ukubwa wa baraza na Usalama na maamuzi ya mwisho virekebishwe," alisema Werema.

"Hakuna haja ya kujinyonga kwa kuwa muswada umekataliwa, zipo 'altenative' (njia) nyingine. Lakini muswada si mbaya, kazi yangu ni kuwasilisha miswada na kuwashauri mawaziri, si kutunga sheria. Wabunge ndio wana wajibu wa kutunga sheria na wametoa mapendekezo urekebishwe... kamati husika inafanyia kazi na utaletwa tena bungeni," alisema Jaji Werema.

Alisema kimsingi walichokifanya wabunge ni haki yao kama watunga sheria, lakini muswada huo hauna tatizo kama ulivyopitishwa katika michakato yote inayohitajika.

Mchangiaji wa kwanza baada ya muswada huo kuwasilishwa, Brigedia Hassan Ngwilizi alisema kuwa Baraza la Usalama linachukua ukubwa wa baraza la pili la mawaziri, jambo ambalo linatishia usiri wa mambo ya usalama wa nchi.

Ngwilizi pia alisema kuwa kipengele kinacholipa baraza nguvu ya kupiga kura ili kupitisha maamuzi makubwa kama ya kwenda vitani, kinamfanya rais, ambaye ni amiri jeshi mkuu, kuwa katika nafasi sawa na watu ambao wanatakiwa kutekeleza maamuzi yake, jambo ambalo linapoteza maana ya dhana nzima ya usalama wa taifa.

Pia kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid alikwenda mbali zaidi na kuuita muswada huo kuwa wa kihaini kwa sababu linawapa wajumbe wa Baraza la Usalama mamlaka ya kupiga kura ya kumuondoa rais.

Waziri Simba alikubaliana na hoja za kuondoa muswada huo.
Naye Simba aliiambia Mwananchi jana kuwa ameridhika na muswada aliouwasilisha bungeni.

Alisema kupingwa kwa muswada huo kumetokana na makosa ya kiufundi baada ya kutopitishwa kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayohusika na suala hilo na badala yake kupitishwa na kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba tu.

Waziri Simba alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana katika mahojiano na Mwananchi ikiwa ni siku mbili baada ya muswada huo kupingwa na wabunge wakitaka kuondolewa kwa vipengere vinavyoingilia madaraka ya Rais.

"Niliusoma, niliridhika na muswada wa Sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa, Siwezi kuleta kitu ambacho sijaridhika nacho," alisema Waziri Simba.

Aliongeza kusema kuwa "kuna tatizo sisi wahusika tuliliona, awali muswada huo haukupitia kamati husika ya Mambo ya nje Ulinzi na Usalama. Kuna tatizo... ofisi ya bunge, ilipaswa kuupeleka katika kamati hiyo ambayo ingepitia kwa pamoja na kamati ya bunge ya sheria na mambo ya katiba."

Hata hivyo, alisema kwa kuzingatia kanuni za bunge na kusikiliza maoni na michango ya wabunge, kwa kutumia busara na taratbu zilizopo aliahirisha hoja hiyo ili atafakari michango ya wabunge.

Wakati huo huo serikali imeahirisha mjadala wa sheria ya udhibiti wa matumizi ya fedha za uchaguzi uliokuwa ufanyike leo hadi Jumatatu ijayo kutokana na marekebisho madogo yanayofanywa katika muswada huo.
 
Ukiona moshi jua kuna moto. Mwisho tutajua japo tukiwa tumeungua nani anatumikia Watz na nani anatumikia tumbo lake
 
Huu uandishi kwa kishenzi unaniudhi sana... hayo mapigo ni yapi?? uandishi unaingiza ushabiki kila sehemu, $%^(*)(*&^%$## kabisa!!!

Na bwana Sitta anapobishana na chizi basi na yeye very soon atakuwa chizi, hayo majibu angemuachia msaidizi wake tu amjibu huyo mama maana wote tunajua huyo mama karukwa na akili, kwahiyo kuanza kumjibu ni kujishusha hadhi tu

Keep quiet Sitta fanya kazi yako... na kama ni kumjibu jibizaneni kwenye nyaraka zenu za siri sio kutuletea upuzi wenu vyombo vya habari

Thats why Mwandosya is smarter... he has ethics always

Chizi lakini kapewa rungu sasa usipomkemea atadhuru wengi. Sita anabisha na nafasi ya Waziri iliyopeleka muswada ambayo imekaliwa na huyo unayesema chizi.
 
..huu mjadala usije ukawa muendelezo wa malumbano yaliyotokea ktk kamati ya CCM inayoongozwa na Raisi Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

..naona Mwanasheria Mkuu anaelezea kitu tofauti kabisa na jinsi waandishi wa habari wanavyoeleza.

..tatizo hakuna waandishi wa habari walio-specialize ktk masuala ya Bunge kuweza kuuchambua mswaada na kuuelimisha umma.

..



Joka Kuu,

Mimi nimeuliza takriban mara tatu sasa hivi.

Jamani, muswada wa kumpunguzia rais madaraka una ubaya gani? Nauliza genuinely kama mtu asiye na details za muswada anayetaka kuelimishwa ubaya wake nini.

Si kila siku tumekuwa tukipiga kelele kwamba moja ya matatizo yetu ni kwamba rais ana madaraka makubwa sana?

Sasa zaidi ya kusikia hii mantra ya boilerplate kwamba "ni hatari kwa usalama wa taifa" bila details hatari ipo wapi? Kutakuwa na constitutional crisis? Kivipi? Kwa nini rais asipunguziwe madaraka? Akipunguziwa tunaweza kupatwa na jaa gani? Mbona nchi nyingine zimeweza? Kuna models za serikali ambazo hata amiri jeshi mkuu si rais/ head of state.

Sijapata jibu, kila nikosma naona catch-phrases zao, "usalama wa taifa" etc etc.Tukumbuke gia hii ya "usalama wa taifa" ndiyo hii hii ilipitisha uchafu wa Mreremeta na EPA.

Mimi nataka details, muswada una mapungufu gani? Sio mnasema tu "miuswada haukuandaliwa vizuri" "umeandaliwa kitoto" details details please.

Au hata details zao ni swala la usalama wa taifa?

Kwamba kama England ya Henry VIII, aliyekuwa haruhusiwi hata kwenda msibani kwa sababu akienda msibani watu wa England wata perceive kifo cha mfalme, which amounts to treason, hata sababu za kwa nini huu muswada ni mwiko on grounds of usalama wa taifa haziwezi kusemwa, less they give some people ideas?

How medieval of us !
 
- Jamani wenye huo mswaada watusaidie tuuchambue hapa, au? Maana Rais wangu Dr. Slaa hawezi kutaka Sophia afukuzwe uwaziri kwa kutaka kupunguza madaraka ya Rais wa CCM, haingii akilini dawa wenye huo mswaada wauweke hapa, tukate mzizi wa fitina, au?

Respect.


FMEs!
 
Unadhani hajamsikia Sheikh Ubwabwa Yahya?

Ah hana lolote yule tapeli mkubwa anayewaaibisha waislamu. Angelikuwa yeye mtabiri wa kweli abashiri yeye atakufa lini na sio kutishia wenzie. Mie bwana safari namsupport rais ambaye msomi na makini wa kazi. Ndani ya CCM kwakweli namuona ni magufuli na mwandosya ndio wanafaa wengine wote makelele mengi. Wakiwa hawawezi wawape akina Lipumba na Slaa tunahitaji umakini katika uongozi
 
Huyu waziri ni balaa,ebu fuatilieni alivyofanya Loleza sekondari last week- shameful ++++????
analazimisha mtoto wa jirani yake arudishwe shule wakati anatumikia adhabu, kwa kudai yeye ndie waziri pekee aliye na ofisi kivukoni karibu kabisa na mkulu ,nani anababisha-JK toa aibu ya mama huyu akaimbe mipasho na mzee yusuph?????ovyooo?????????
jamani naogopa cctv.ningesema mengi.
 
i will be so puzzled, mwaka huu, huyu SS atakapo teuliwa kuwa waziri again.
 
Back
Top Bottom