Sitta: Waziri Simba kalikoroga

Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
na Martin Malera

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta amesema madai kwamba ofisi yake ndiyo chanzo cha wabunge kuukataa muswada wa kuundwa kwa Baraza la Usalama wa Taifa ni ya kipuuzi.

Badala yake Spika Sitta alisema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sofia Simba ndiye aliyelikoroga kwani alipeleka bungeni muswada huo bila kufikiria mambo aliyoyaweka ndani yake.

Sitta alitoa kauli hiyo jana akifafanua taarifa zilizoibebesha lawama ofisi yake kwamba ilivurunda kwa kuupeleka muswada huo kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala badala ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma, jana, Spika Sitta alisema hata kama muswada huo ungepita kwenye kamati wanayosema kuwa ndiyo sahihi, bado ungekuwa na kasoro kutokana na mambo yaliyoandaliwa.

Sitta alimshangaa Waziri Simba kwa kuandaa muswada kama huo aliouita wa hatari na kuhoji kama waziri huyo alifikiria vizuri kabla ya kuupeleka bungeni.

“Hata kama muswada huu ungeenda kwenye kamati yoyote bado usingepita kwa jinsi ulivyoletwa na sijui Waziri anayepeleka kitu kama hiki amefikiria vizuri maana ni wa hatari kweli,” alisema Spika Sitta.

Kwa mujibu wa Sitta, muswada huo unapaswa kufanyiwa marekebisho na kama watauona haufai, wanaweza wakauacha kabisa kwa sasa.

“Haya madai kwamba ofisi ya Spika ndiyo chanzo cha kukwamisha muswada huo ni ya kipuuzi kabisa kwa sababu katibu ana maelekezo yote na ametoa maelekezo sahihi kabisa, na hii si mara ya kwanza.

“Kwa mfano wakati wa kuchunguza suala la mgodi wa Barrick, North Mara, ofisi yangu iliunda kamati mbili; moja ya Nishati na Madini na nyingine ya Mazingira na bado tungeweza kuwa na kamati nyingine ya Afya ishiriki, hakuna ubaya, na ndicho kilichofanyika, sasa hili linashangaza kwa kweli kwa sababu hakuna nia mbaya kama wanavyodai,” alisema Spika Sitta.

Sitta amelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa kwamba kulikuwa na msuguano mkali kati ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na ile ya Katiba, Sheria na Utawala.

Naibu Spika wa Bunge, alikaririwa akisema juzi kuwa hakukuwa na ubaya katika kufanya hivyo kwani kamati husika ilikuwa na kazi nyingi.

Wiki iliyopita, katika kile kinachoonekana kugoma kuburuzwa na serikali wabunge kwa mara ya pili waligoma kuupitisha muswada wa Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa wa mwaka 2009.

Muswada huo uliowasilishwa bungeni na Waziri Simba, uliibua mjadala mkubwa kwa wabunge ambao wameweka bayana kuwa serikali isipokuwa makini, kuna kila dalili ikashindwa kuendelea.

Mwaka jana muswada huo ulikataliwa na wabunge kwa madai kuwa una upungufu mkubwa, lakini haukuweza kufanyiwa marekebisho kama walivyopendekeza wabunge.

Wabunge hao wamebainisha kuwa muswada huo unakwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuingilia madaraka ya rais kwa kumuundia chombo ambacho kitafanya kazi zake za ulinzi na usalama wa nchi.

Baadhi walidai kuwa baraza hilo lina mlolongo wa watu wengi ambao ni kama vile kuunda baraza jingine la mawaziri na litakuwa si Baraza la Usalama tena bali ni suala la kisiasa.

Pia muswada huo unadaiwa kutaka kunyang’anya madaraka ya rais na iwapo utapitishwa utaiweka nchi pabaya.

Kutokana na kasoro iliyojitokeza kwenye muswada huo, Mbunge wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa (CHADEMA) amemtaka Rais Jakaya Kikwete kumuwajibisha Waziri Simba iwapo hatajiwajibisha kwa kujiuzulu.

Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, alisema suala hilo linaonekana kuwa dogo, lakini ni kubwa na iwapo litapuuzwa, litakuwa hatari kwa maslahi ya taifa.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa ibara ya 97 ya Katiba ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu cha 69 cha kanuni za Bunge, Waziri Simba angetakiwa kujiuzulu mara moja kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake. Pia alitaka watendaji walio chini ya rais pamoja na Kamati ya Bunge iliyoupitia muswada huo kabla ya kupelekwa bungeni kuwajibishwa mara moja. Baadhi ya kasoro zilizoko kwenye muswada huo, zimo katika kifungu cha 5 (2) g, ambacho hakikueleza wazi maadui wa taifa, hivyo kinatoa nafasi kwa baadhi ya watu kuonekana maadui wakati sivyo.

Hoja zangu!
Viongozi wakubwa Spika wa Bunge na Waziri mwenye dhamana kujibishana hivi,hivi huu ni Utawala Bora?kuna nii nyuma ya pazia?kwani hawawezi kukaa pamoja mpaka wajibizane kwenye media?hivi tutafika kweli?
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,286
Likes
65
Points
145
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,286 65 145
wameanza kumtafuta mchawi!....
tutayasikia yote!
BUNGE LENYE MENO:D
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,407
Likes
5,803
Points
280
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,407 5,803 280
Mkiambiwa simba ni mropokaji wa JK kwenye vikao mnabisha...ameboronga haijawahi kutokea duniani!!aibu sana kwa taifa kuwa waziri kilaza kama sofia!!
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
wameanza kumtafuta mchawi!....
tutayasikia yote!
BUNGE LENYE MENO:D
Tutasikia yote na hata yale ambayo sisi kama Watanzania wa kawaida hatukupaswa kuyasikia.
 
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2007
Messages
586
Likes
6
Points
0
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2007
586 6 0
Hiki kimama kimezidi kuropoka..Mimi nadhani ni vema kingejiuzulu kama ambayo DK Slaa amepropose.
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,286
Likes
65
Points
145
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,286 65 145
Tutasikia yote na hata yale ambayo sisi kama Watanzania wa kawaida hatukupaswa kuyasikia.
unajua nin,
mtu anapozungumzia viongozi wanawake....!AKIFANYA REFERENCE KWA WATU KAMA SIMBA...!conclusion itakuwa wanawake hawawezi kuongoza!alichokifanya simba NI KITU CHA AJABU NA KUSIKITISHA HAIJAWAHI KUTOKEA!.....

sasa kimbembe ni kwa yule ''aliyempa uwaziri''...!kutoka viti maalumu mpaka uwaziri..!:D
 
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Messages
9,844
Likes
1,256
Points
280
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2010
9,844 1,256 280
Huu uandishi kwa kishenzi unaniudhi sana... hayo mapigo ni yapi?? uandishi unaingiza ushabiki kila sehemu, $%^(*)(*&^%$## kabisa!!!

Na bwana Sitta anapobishana na chizi basi na yeye very soon atakuwa chizi, hayo majibu angemuachia msaidizi wake tu amjibu huyo mama maana wote tunajua huyo mama karukwa na akili, kwahiyo kuanza kumjibu ni kujishusha hadhi tu

Keep quiet Sitta fanya kazi yako... na kama ni kumjibu jibizaneni kwenye nyaraka zenu za siri sio kutuletea upuzi wenu vyombo vya habari

Thats why Mwandosya is smarter... he has ethics always
 
B

blackpepper

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
382
Likes
2
Points
33
B

blackpepper

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
382 2 33
sasa bado hamuamini kwamba Sofia Simba ni KILAZA NAMBA ONE NDANI YA BARAZA LA JK??
 
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Messages
7,495
Likes
104
Points
160
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2008
7,495 104 160
sasa bado hamuamini kwamba Sofia Simba ni KILAZA NAMBA ONE NDANI YA BARAZA LA JK??
Mnamwonea tu SS. Muswada ili ufike Bungeni ni mchakato mrefu. Wa kulaumiwa hasa ni AG kama kuna mapungufu. AG amejaribu kupunguza madaraka ya Rais kidogo tu wahafidhina akina Ngwilizi, Malecela wamemjia juu kwelikweli. Ngoja siku tukimpata Rais mchokozi au anayependa vita.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
unajua nin,
mtu anapozungumzia viongozi wanawake....!AKIFANYA REFERENCE KWA WATU KAMA SIMBA...!conclusion itakuwa wanawake hawawezi kuongoza!alichokifanya simba NI KITU CHA AJABU NA KUSIKITISHA HAIJAWAHI KUTOKEA!.....

sasa kimbembe ni kwa yule ''aliyempa uwaziri''...!kutoka viti maalumu mpaka uwaziri..!:D
Mkuu hapo mimi sikubaliani na wewe..si kweli kwamba wanawake hawawezi kuongoza,anapokosea mwanamke mmoja hawamaanishi wote hawafai..mbona kuna viongozi wanaume wengi tu ambao wamefanya blanda?na mbona kuna viongozi wanawake wengi tu waliofanya vizuri?Nadhani tatizo hapa ni Sophia kama individual na sio ujinsia wake..You Know what am Gender Sensitive
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,286
Likes
65
Points
145
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,286 65 145
Mkuu hapo mimi sikubaliani na wewe..si kweli kwamba wanawake hawawezi kuongoza,anapokosea mwanamke mmoja hawamaanishi wote hawafai..mbona kuna viongozi wanaume wengi tu ambao wamefanya blanda?na mbona kuna viongozi wanawake wengi tu waliofanya vizuri?Nadhani tatizo hapa ni Sophia kama individual na sio ujinsia wake..You Know what am Gender Sensitive
...nadhani hujanielewa!...!kaisome tena
 
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2007
Messages
586
Likes
6
Points
0
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2007
586 6 0
Huu uandishi kwa kishenzi unaniudhi sana... hayo mapigo ni yapi?? uandishi unaingiza ushabiki kila sehemu, $%^(*)(*&^%$## kabisa!!!

Na bwana Sitta anapobishana na chizi basi na yeye very soon atakuwa chizi, hayo majibu angemuachia msaidizi wake tu amjibu huyo mama maana wote tunajua huyo mama karukwa na akili, kwahiyo kuanza kumjibu ni kujishusha hadhi tu

Keep quiet Sitta fanya kazi yako... na kama ni kumjibu jibizaneni kwenye nyaraka zenu za siri sio kutuletea upuzi wenu vyombo vya habari

Thats why Mwandosya is smarter... he has ethics always
Ndugu punguza jazba..Kujibu Mapigo maamna yake ni kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwako..Sitta ametuhumiwa kwambayeye ndio aliyesababisha muswada wa usalama usijadiliwe na hivyo yeye amejibu...inavyoonekana hata habri yenyewe hujaisoma umesoma tu kichwa cha habri na kukuirupuka kuijibu kwakuwa wewe ndio shabiki hapa.Dont ruin your day my dia bado ni mapema mno.
 
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
3,849
Likes
29
Points
145
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
3,849 29 145
Mkuu hapo mimi sikubaliani na wewe..si kweli kwamba wanawake hawawezi kuongoza,anapokosea mwanamke mmoja hawamaanishi wote hawafai..mbona kuna viongozi wanaume wengi tu ambao wamefanya blanda?na mbona kuna viongozi wanawake wengi tu waliofanya vizuri?Nadhani tatizo hapa ni Sophia kama individual na sio ujinsia wake..You Know what am Gender Sensitive
KUBWA ZAIDI NI KUWA SINGLE MUDA MWINGI UNAISHIA KURUKARUKA KUTAFUTA SUNGURA................:confused::confused::confused:
 
M

Mchili

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2009
Messages
727
Likes
6
Points
35
M

Mchili

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2009
727 6 35
Jamani kuna mtu mwenye details kuwa mswada wenyewe uli-contain nini haswa?? Then tunaweza kuanalyse kama kulikua na umuhimu wa kuukataa kwa maslahi ya nchi. Mwenye undani wake tafadhali tuwekee hapa.
 
N

Nanu

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
1,224
Likes
9
Points
135
N

Nanu

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
1,224 9 135
Jamani wa kulaumiwa hapa sio Simba. Kwanza ujue huu muswada uliletwa 2009 ukarudishwa kwa ajili ya marekebisho ukaletwa tena 2010. Huu muswada ulindaliwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama mara ya kwanza, ikarudishwa na kipindi hiki ikafanyiwa kazi na Kamati ya Sheria na Katiba. Kamati hizi ambazo pia ina wabunge wamepitia muswada huu na kuridhia na ndiyo maana S.Simba kaupeleka mezani bungeni. Pamoja na hayo cabinet pia ilipitia akiwepo JK mwenyewe au mwakilishi wake nao pia waliridhia upelekwe bungeni. Sasa kama hawa wote waliona sawa kwani lawama yote tumtwishe Simba leo? Lawama inabidi iende kwa wote waliohusika yaani kamati zote mbile na baraza la mawaziri. Isitoshe kipindi hiki wanataka marekebisho madogo ambayo ni kupunguza ukubwa wa baraza la usalama kutoka wajumbe 20 kuwa chini ya hapo (confidentiality reasons) halafu na pia kipengele kisomeke pia kuwa baraza litamshauri Rais (amiri jeshi mkuu) na siyo kuwa linakuwa la utendaji kama ilivyoletwa. Ni positive thinking ya wabunge na ni muhimu kuwapongeza kwa hilo lakini si kupeleka lawama kwa Simba bali kwa msururu wa wahusika wote!!! Wabunge wawe wangekuwa makini siku zote tusingekuwa na mikataba mibovu au sheria ambazo hazitekelezeki!!!!!!
 
K

Kachoki

Member
Joined
Feb 2, 2010
Messages
29
Likes
0
Points
3
K

Kachoki

Member
Joined Feb 2, 2010
29 0 3
Mkuu hapo mimi sikubaliani na wewe..si kweli kwamba wanawake hawawezi kuongoza,anapokosea mwanamke mmoja hawamaanishi wote hawafai..mbona kuna viongozi wanaume wengi tu ambao wamefanya blanda?na mbona kuna viongozi wanawake wengi tu waliofanya vizuri?Nadhani tatizo hapa ni Sophia kama individual na sio ujinsia wake..You Know what am Gender Sensitive
copy and paste,
hapo ni suala la mtu binafsi na siyo kundi zima!!! mbona kina karamagi walipoboroga ina maana wanaume wote vilaza???

nawakilisha
 
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Messages
9,844
Likes
1,256
Points
280
Janjaweed

Janjaweed

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2010
9,844 1,256 280
Ndugu punguza jazba..Kujibu Mapigo maamna yake ni kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwako..Sitta ametuhumiwa kwambayeye ndio aliyesababisha muswada wa usalama usijadiliwe na hivyo yeye amejibu...inavyoonekana hata habri yenyewe hujaisoma umesoma tu kichwa cha habri na kukuirupuka kuijibu kwakuwa wewe ndio shabiki hapa.Dont ruin your day my dia bado ni mapema mno.

  • bwana we nimekula magimbi na uji... hali mbaya tumboni aisee... ila habari niliisoma mara mbili na nikachukia kwasababu
  • sitta kamjibu yule mama ambaye tunajua matatizo yake
  • habari imekaa kishabiki
  • sakata zima linaudhi

sasa ukichanganya na magimbi unadhani ntakuaje?
 
M

Mapinduzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2008
Messages
2,427
Likes
23
Points
0
M

Mapinduzi

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2008
2,427 23 0
Jamani wa kulaumiwa hapa sio Simba. ....
Kama waziri husika, she should have known earlier and better kwamba hicho kitu ni famba. Kwa mweledi na mwenye kujali umakini wa kazi yake, angekataa kuwasilisha ule muswada.

Unakumbuka sakata kati ya Masha na katibu mkuu wa wizara yake pamoja na katibu mkuu kiongozi? Masha alishtukia mambo kama haya kutokea.

Mwisho wa siku hakuna kuchambua nani alisababisha Simba kuchemsha, ni yeye mwenyewe. Smart people take rensposibility of their actions and be accountable for them.
 
Forum statistics

Threads 1,250,505
Members 481,371
Posts 29,736,013