Sitta: Uchaguzi ndani CCM umevurugika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Uchaguzi ndani CCM umevurugika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Karibuni masijala, Sep 22, 2012.

 1. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Amesema hayo katika Mahafali ya Darasa la 7 Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa Rafiki yake Lembeli. Ambapo aliialikwa kama mgeni Rasmi kwa nafasi yake ya Waziri wa Afrika Mashariki, Amekiri chama kuwa na wala rushwa na Viongozi wasiofanya mamuzi. Source: ITV Habari Asubuhi. Je, ccm inaweza kuzaliwa upya kwa chaguzi za Jumuiya zake mwaka huu, kwa jinsi mchakato wake unavyoendeshwa katika Jumuiya za Uvccm, Wanawake, Wazazi na upatikanaji wa wajumbe wa NEC wilayani? Wana jamvi; Usikibanie ccm maoni yako ili kijue kama hakitazaliwa upya kwenye chaguzi hizi kijaribu tena vua gamba au mkakati mwingine. Karibuni kwa hoja
   
 2. J

  Jadi JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,403
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Jamani hii imekaaje maana Sita kaitwa kuwaasa vijana wa darasa la Saba,yeye kakomaa na uchaguzi wa CCM, hizi ndo akili?mi sidhani kama ni sawa, maana yule Mbunge amekuwa focused kwa kuwaasa vijana na maisha ya baadae.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Izaliwe upya? ishaoza, haiwezi tena!! Sitta aende CCK
   
 4. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,536
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Mwanza siku hizi imefika mpaka kahama kweli! Au Shy.
   
 5. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania zaidi ya ujuavyo, anayasema hayo kwenye mahafali ya Darasa la 7 badala ya kwenye chama hasa Jumuiya hizo. Sasa hao Darasa la 7 ni Wanajumuiya mojawapo za chama. Walimhitaji awape husia wa maisha baada ya kuhitimu anawaeleza habari za Jumuiya na chama wakati amealikwa kama Waziri wa Afrika mashariki angewaasa sana juu ya Soko la Ajira la Afrika mashariki angekuwa amekitendea haki kizazi kilichohitimu.
   
 6. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shukrani nimerekebisha ni Shinyanga
   
 7. B

  Bukutonaga JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nahisi sita anatumika ili kuwaambia watu hasa watoto wadogo kama hao std VII kuwa CCM si chama cha kukimbilia huko waendako wala kukiamini maana kina hayo matatizo makubwa alowaambia watoto hawa! So Sitta endelea kutoa Elimu ya uraia kwa watanzania wengi kuendelea kuikataa CCM.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  YAani hawa jamaa kila wakipata nafasi wanatupia siasa za chama chao kilichoanguka!!! Badala ya kuwaeleza kuwa "shule imekwisha na shule imeanza" anakazana na uchaguzi wa thithimwewe!!!!!
   
 9. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee Sitta - ili CCM izaliwe upya lazima ife kwanza. Tafadhali amka na uone kuwa unafanya kazi ma mizoga.
   
 10. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rais alijaribu vua Gamba izae upya Gamba likangangania likawa linataka lichomoke na Ngozi. Sasa kuzaliwa upya kwa kutumia chaguzi za Jumuiya akili inagoma kuona kuna uwezekano ssm ya mtandao makundi
   
 11. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Mr Six Hayo unayoyatamani na kuyataka HAYAWEZEKANIKI kutendwa wala kupendwa na wana CCM wenzako. Unakumbuka jinsi ulivyoizima ile hoja hot ya Richmond? Acha unafiki wewe, umezeeka sasa tumia utu uzima wako kuwa mkweli na mwenye busara.
   
 12. C

  Concrete JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hizo ni Ndoto za mchana za mateja baada ya kubwia unga.

  Si ni wao wenyewe walituambia mkakati wa kuvuana magamba ulilenda kuzaliwa upya kwa CCM?
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 22 September 2012 13:04[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  Tausi Mbowe, Kahama

  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kuwa chaguzi zinazoendelea ndani ya CCM zimevurugika kwa kuwa mafisadi wameingilia na kupachika watu wao kwa lengo la kulinda masilahi yao.

  Sitta alisema hayo jana mjini hapa katika mahafali ya 11 ya Shule ya Msingi Kwema yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Shule ya Sekondari Kwema.

  Alisema watu waliojitokeza kugombea ni mapandikizi na vibaraka wa mafisadi hao.

  "Hivi karibuni tumepata aibu kubwa ndani ya chama chetu, wakati chaguzi zetu zikiendelea viongozi wamepitisha vipaza sauti vya mafisadi, kazi yao kubwa ni kulinda masilahi ya mabwana zao na kuwafurahisha," alisema na kuongeza:

  "Wameajiriwa kwa lengo la kupiga kelele, kupiga vijembe, kuwapamba wafalme wao ambao wamefanikisha kuwa wanapata madaraka hayo, lakini kubwa zaidi ni kuwa vibaraka."

  Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alisema lengo kubwa la mafisadi hao ni kuhakikisha wanashika kila sehemu ya nchi ili iwe rahisi kwao kuendelea kutafuna rasilimali za nchi kwa kupitia watu wao.

  Alienda mbali zaidi na kutoa mfano wa miaka ya zamani ambapo nchi za Uingereza na Ufaransa kulikuwa na wafalme ambao walikuwa wakiwaajiri watu ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kumchekesha mfalme huyo hata kama atakuwa amekosea.

  "Wachekeshaji wa mfalme wao wanawajibika kwa mfalme, kumsifia, kuremba kupiga vijembe, kuwa vibaraka, kujipendekeza, kumpamba, lakini kubwa zaidi ni kumchekesha mfalme hata kama amefanya mabaya,” alisema.

  Sitta alisema wachekeshaji hawana aibu kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa mfalme anafurahi kwa kila kitu hata siku akitembea uchi wao wanasema mfalme umependeza na kanzu yako inang'aa dhahabu.

  Alisema kuwa hali inazidi kuwa mbaya zaidi pale watu hao ambao ni vibaraka wanapojivunia kuwa vibaraka wa watu fulani huku wakipita na kujisifu usiku na mchana wakiwatambia wajumbe.

  Waziri huyo alisema umefika wakati wa chama hicho kuzaliwa upya vinginevyo kitaendelea kupata upinzani hata kutoka katika vyama vidogo.

  Hata hivyo, Waziri huyo alisema ataendelea kusema na wala hataogopa kitu chochote na atakayenuna na anune kwani yeye ni 'Chuma cha Pua' kwa kuwa anaamini anasimamia katika ukweli.

  "Ndiyo maana wengine nikisema huwa wananuna, wananuna kwa sababu hawawatendei haki Watanzania. Nchi imejaa mali na rasilmali, lakini zinatumiwa na watu wachache wenye uchu badala ya kuzitumia sote," alisema na kuongeza:

  "Mimi ni msemakweli ndiyo maana kule kwetu Urambo wananiita 'Chuma cha Pua.' Watu wengine wanasema nailaumu Serikali wakati mimi nipo serikalini na kwamba hiyo ni aibu... Sasa aibu ipo wapi? Hapa mimi nipo ndani ya Serikali lazima niseme vitu hivi kamwe siwezi kunyamaza na kuacha mambo yakiharibika."

  Sitta alilaani tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali wanaonyamazia maovu kwa kuwa tu wanaogopa kuonekana wabaya ndani ya jamii.

  Alisema viongozi wengine wamekuwa wanafiki kwa kuwa wako ndani ya Serikali na mambo yanaharibika wananyamaza hivyo nao kuwa kama wachekeshaji wa mfalme.

  Alisema watu wanatumia vibaya madaraka, kuna watu wazima wanafikiri kwa kutumia matumbo yao badala ya akili wakati mwingine wanajisahau na kuwa na matumbo makubwa mpaka yanawashinda.

  Aliwataka watu wote wanaohusika kuleta viongozi katika chaguzi hizo watumie fursa hiyo kuweka viongozi bora na si bora viongozi ambao wana masilahi yao binafsi.

  Wakati hali katika chaguzi hizi zikienda ovyo, Waziri Sitta alisema pia kuwa amepata fununu mafisadi hao wanafanya kila njia kuhakikisha wanaweka vibaraka wao katika uongozi wa wilaya hiyo ili kuhakiksha wanaendelea kunufaika na migodi iliyopo katika wilaya hiyo.

  "Nimepata taarifa kuwa eti umeme unapatikana katika migodi ambayo inazunguka wilaya hii saa 24, lakini cha ajabu wananchi hawafaidiki na umeme huu. Hii inamaanisha nini hasa? Yaani wawekezaji ni bora sana kuliko wananchi? alihoji Sitta.

  Mahafali hayo pia yalihudhuriwa na Mbunge wa jimbo hilo, James Lembeli ambaye alisema shule hiyo imeujengea sifa mji wa Kahama kwa kuwa mwaka jana ilikuwa ya pili kitaifa na kutoa wanafunzi bora watatu katika 10 bora ambao walishika nafasi ya kwanza, tatu na ya nne.

  Lembeni ambaye ndiye aliyeonyesha wazi kuanza kuchochea moto huo wa Sitta alisema kuwa wahitimu wa shule hiyo ndio wanaohitajika katika taifa la Tanzania kwa kuwa wamekuzwa katika misingi ya kutokupenda rushwa, kwani hata kujiunga na shule hiyo inahitaji uadilifu wa hali ya juu.

  Mkurugenzi wa Shule hiyo, Pauline Mathayo alisema hata siku moja hawezi kuruhusu vitendo vya kifisadi katika shule yake kwani anaamini elimu ikitumika vibaya inaweza kuzalisha watu hatari sana katika taifa.

  "Wote ni mashuhuda, sasa wizi wa benki kwa njia ya mtandao umezidi kuongezeka yote hii inatokana na kutumia elimu vibaya,"alisisitiza Mathayo.

  E & P
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ndio Maana CCM SHINYANGA wanamfanyia Mizengwe MWENYEKITI WA CCM SHINYANGA jina lake lisipite NEC; Kwa kumsifia Dr. SLAA?

  Mbona ZITTO KABWE anamsaidia Rais KIKWETE mfano ule wa KUVUNJA BUNGE na bado CHADEMA wanamkumbatia?
   
 15. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Wauane tu maana hawana faida kwangu.
  I'm proud to be born an Adventist member.
   
 16. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Ameelemewa
   
 17. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Naona Sitta anazeeka vibaya. Sijui amepumbazwa? Au kalogwa? Au ni kuzeeka vibaya tu? Au M4C imemchangaya akili kiasi cha kuchanganyikiwa? Na kwa taarifa yake atabwabwaja sana tu mpaka kufika 2015 atakufa kwa presha. Chadema hatumtaki maana mnafiki, CCM ndo hivyo mafisadi wameshamzidi kete, maskini cjui aende wapi
   
 18. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm hawana jipya
   
 19. k

  kula kulala Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hebu nammbieni toka lini mzee wa miaka hamsini akarudi kuwa kijana wa miaka kumi na nane
  sisiem ni kizee tuu hata wafanye nini hawawezi kuwa kama chadema kwani ndio kwanza kijana
   
 20. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Analikia urais tu huyo Six, hana jipya! Mbona alitishwa hakuwataja wamiliki wa Dowans, nae ni mnafiki tu! Na CCM yake wameoza wote!
   
Loading...