Sitta: Uchaguzi ndani CCM umevurugika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Uchaguzi ndani CCM umevurugika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 23, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,561
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Sitta: Uchaguzi ndani CCM umevurugika
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 22 September 2012 13:04
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta

  Tausi Mbowe, Kahama
  Mwananchi

  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kuwa chaguzi zinazoendelea ndani ya CCM zimevurugika kwa kuwa mafisadi wameingilia na kupachika watu wao kwa lengo la kulinda masilahi yao.

  Sitta alisema hayo jana mjini hapa katika mahafali ya 11 ya Shule ya Msingi Kwema yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Shule ya Sekondari Kwema.

  Alisema watu waliojitokeza kugombea ni mapandikizi na vibaraka wa mafisadi hao.

  "Hivi karibuni tumepata aibu kubwa ndani ya chama chetu, wakati chaguzi zetu zikiendelea viongozi wamepitisha vipaza sauti vya mafisadi, kazi yao kubwa ni kulinda masilahi ya mabwana zao na kuwafurahisha," alisema na kuongeza:

  "Wameajiriwa kwa lengo la kupiga kelele, kupiga vijembe, kuwapamba wafalme wao ambao wamefanikisha kuwa wanapata madaraka hayo, lakini kubwa zaidi ni kuwa vibaraka."

  Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alisema lengo kubwa la mafisadi hao ni kuhakikisha wanashika kila sehemu ya nchi ili iwe rahisi kwao kuendelea kutafuna rasilimali za nchi kwa kupitia watu wao.

  Alienda mbali zaidi na kutoa mfano wa miaka ya zamani ambapo nchi za Uingereza na Ufaransa kulikuwa na wafalme ambao walikuwa wakiwaajiri watu ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kumchekesha mfalme huyo hata kama atakuwa amekosea.

  "Wachekeshaji wa mfalme wao wanawajibika kwa mfalme, kumsifia, kuremba kupiga vijembe, kuwa vibaraka, kujipendekeza, kumpamba, lakini kubwa zaidi ni kumchekesha mfalme hata kama amefanya mabaya," alisema.

  Sitta alisema wachekeshaji hawana aibu kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa mfalme anafurahi kwa kila kitu hata siku akitembea uchi wao wanasema mfalme umependeza na kanzu yako inang'aa dhahabu.

  Alisema kuwa hali inazidi kuwa mbaya zaidi pale watu hao ambao ni vibaraka wanapojivunia kuwa vibaraka wa watu fulani huku wakipita na kujisifu usiku na mchana wakiwatambia wajumbe.

  Waziri huyo alisema umefika wakati wa chama hicho kuzaliwa upya vinginevyo kitaendelea kupata upinzani hata kutoka katika vyama vidogo.

  Hata hivyo, Waziri huyo alisema ataendelea kusema na wala hataogopa kitu chochote na atakayenuna na anune kwani yeye ni 'Chuma cha Pua' kwa kuwa anaamini anasimamia katika ukweli.

  "Ndiyo maana wengine nikisema huwa wananuna, wananuna kwa sababu hawawatendei haki Watanzania. Nchi imejaa mali na rasilmali, lakini zinatumiwa na watu wachache wenye uchu badala ya kuzitumia sote," alisema na kuongeza:

  "Mimi ni msemakweli ndiyo maana kule kwetu Urambo wananiita 'Chuma cha Pua.' Watu wengine wanasema nailaumu Serikali wakati mimi nipo serikalini na kwamba hiyo ni aibu... Sasa aibu ipo wapi? Hapa mimi nipo ndani ya Serikali lazima niseme vitu hivi kamwe siwezi kunyamaza na kuacha mambo yakiharibika."

  Sitta alilaani tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali wanaonyamazia maovu kwa kuwa tu wanaogopa kuonekana wabaya ndani ya jamii.

  Alisema viongozi wengine wamekuwa wanafiki kwa kuwa wako ndani ya Serikali na mambo yanaharibika wananyamaza hivyo nao kuwa kama wachekeshaji wa mfalme.

  Alisema watu wanatumia vibaya madaraka, kuna watu wazima wanafikiri kwa kutumia matumbo yao badala ya akili wakati mwingine wanajisahau na kuwa na matumbo makubwa mpaka yanawashinda.

  Aliwataka watu wote wanaohusika kuleta viongozi katika chaguzi hizo watumie fursa hiyo kuweka viongozi bora na si bora viongozi ambao wana masilahi yao binafsi.

  Wakati hali katika chaguzi hizi zikienda ovyo, Waziri Sitta alisema pia kuwa amepata fununu mafisadi hao wanafanya kila njia kuhakikisha wanaweka vibaraka wao katika uongozi wa wilaya hiyo ili kuhakiksha wanaendelea kunufaika na migodi iliyopo katika wilaya hiyo.

  "Nimepata taarifa kuwa eti umeme unapatikana katika migodi ambayo inazunguka wilaya hii saa 24, lakini cha ajabu wananchi hawafaidiki na umeme huu. Hii inamaanisha nini hasa? Yaani wawekezaji ni bora sana kuliko wananchi? alihoji Sitta.

  Mahafali hayo pia yalihudhuriwa na Mbunge wa jimbo hilo, James Lembeli ambaye alisema shule hiyo imeujengea sifa mji wa Kahama kwa kuwa mwaka jana ilikuwa ya pili kitaifa na kutoa wanafunzi bora watatu katika 10 bora ambao walishika nafasi ya kwanza, tatu na ya nne.

  Lembeni ambaye ndiye aliyeonyesha wazi kuanza kuchochea moto huo wa Sitta alisema kuwa wahitimu wa shule hiyo ndio wanaohitajika katika taifa la Tanzania kwa kuwa wamekuzwa katika misingi ya kutokupenda rushwa, kwani hata kujiunga na shule hiyo inahitaji uadilifu wa hali ya juu.

  Mkurugenzi wa Shule hiyo, Pauline Mathayo alisema hata siku moja hawezi kuruhusu vitendo vya kifisadi katika shule yake kwani anaamini elimu ikitumika vibaya inaweza kuzalisha watu hatari sana katika taifa.

  "Wote ni mashuhuda, sasa wizi wa benki kwa njia ya mtandao umezidi kuongezeka yote hii inatokana na kutumia elimu vibaya,"alisisitiza Mathayo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ha ha ha ha
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Duh!nahisi kizunguzungu vile!huyu si waziri wa serikali ya ccm au ccj?!!
   
 4. A

  Andras Mahenge Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mwenyewe huyo...! Kazi ipo...!
   
 5. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Mr SIX ya nini kulalama? Mwenyekiti wako si Kikwete wewe? Hujui anapatikana wapi? Au unazuiwa kuonana naye kama mpinzani? Peleka hoja zako kama unaziamini mbele y Halmashauri ya Ccm. Acha unafiki, fisadi uliyekubuhu. Kilio chote hicho ni kudanganywa na Kikwete kuwa, atakuteua kuwa PM, kumbe alikuwa anakuzuga tu. POLE WEE!
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mahafali na Habari za CCM? Kweli wazee wanapagawa
   
 7. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,648
  Likes Received: 5,242
  Trophy Points: 280
  wapi ritz, rejao, zomba and others wachekeshaji.?????????????
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Sitta bana mtu wa ajabu sana..anapugapiga makelele tu hana lolote la maana analoliamua
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Sita anaweweseka....yeye amewageuka wenzake!alitubu lini?maana na yeye alikuwemo humo kwenye mtandao wa JK, EL na wengine...alipotoswa U-PM ndio akapagawa wakampooza na Uspika!asiseme wenzake hali na yeye ni mmoja wao!mimi simuamini sababu na yeye ni mmoja wao sema ametoswa
   
 10. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Samuel Sitta hana kiti kwenye Baraza la Mawaziri? Pengine CCJ inamuita sasa anaamua kunyea kambi. (Japokuwa wliyoyasema ni ya kweli) bado ccm haiko tayari kuusikiliza na kuuhifadhi ukweli.
   
 11. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  kuishiwa kubaya. Waziri wa A. mashariki kwenda kwenye mahafali halafu badala ya kuzungumzia kilichokupeleka unaongelea chaguzi za CCM? sasa hao wahitimu wajifunze nini kutoka kwako?
   
 12. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Humu JF wachekeshaji wa serikali ya ccm ni wengi kweli..!
   
 13. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  Sitta is here again...... kaz ipo mwaka huu
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,561
  Trophy Points: 280
  Mir namshangaa sana Sitta kwa kuamua kuweka mbele maslahi yake binafsi badala ya yale ya nchi. Anayafahamu madhambi chungu nzima ya viongozi wa juu wa magamba na Serikali lakini ameamua kuyafumbia macho huku nchi ikizidi kuangamia, lakini yuko tayari kuyatumia madhambi hayo kuwatisha watenda dhambi hao ili kulinda maslahi yake. Sitta naye ni mnafiki anayejali maslahi yake binafsi tu.
   
 15. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  Naona kaamua kumchana JK na wapambe wake aina ya Magufuli. Wanaosifia safari za nje ambazo hazina tija kwa taifa zaidi ya kutuongezea ufukara na madeni yasiyolipika.!
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  tatizo la sitta ni mkweli kupita kiasi na watu wa aina yake bahati mbaya sana kwenye nchi zetu hizi huwa hawatakiwi kuwepo
   
 17. i

  iseesa JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huna sababu ya kuhisi kizunguzungu kwa sababu ni waziri wa CCM. Kama kuna ukweli acha aseme ili dhamira isimsute. Mr6 katenda jema kwa kusema ukweli
   
 18. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  sitta amechanganyikiwa, yeye yupo kamati kuu ya ccm, ni mbunge , mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm, pia ni waziri wa serikali anaingia baraza la mawaziri linalopitisha sera na mipango ya serikali sasa huku kulalama nje tena aibu analalamika mbele ya wanafunzi wa primary maanake nini ?
  maana yake sasa amechanganyikiwa kwani mbio zake za ikulu zinaelekea kuanza kushindwa, wenzie kina Lowasaa, Sumaye na wengine kampeni zao kubwa sasa anagwaya
  sitta ni mnafiki mkubwa, tunajua alishiriki kuuza mashirika mengi tu wakati ule alikua mkuu wa ubinafsishaji, na vingi ya viwanda vilivo uzwa vimegeuzwa ma godwn tu
  kweli ccm inahitaji fikra mpya na uongozi mpaya wenye uono wa hali wa mambo yanavokwenda sasa duniani lakini ni dhahiri sitta hayumo katika hao...yeye ni sawa tu na waliopo--
   
Loading...