Sitta: Sasa CCM tuache kupambana wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Sasa CCM tuache kupambana wenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Sep 2, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sitta, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi wa CCM wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

  Alisema mapambano ndani ya CCM yanachangia kukidhoofisha chama hicho hasa wakati huu ambapo Taifa lipo katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

  Sitta alisema mapambano ndani ya CCM ni chanzo cha migogoro inayosababisha viongozi na wanachama wake kutakiana mambo mabaya, hivyo kutoa mwanya kwa miongoni mwa waliomo ndani yake, kuhamia upinzani.

  Sitta aliyesisitiza kuendelea kukubalika kwa chama hicho nchini, alisema pamoja na tahadhari hiyo, ipo haja ya kuendeleza na kufanikisha vita ya viongozi wasiokuwa waadilifu hasa mafisadi, ili kurejesha hadhi ya CCM na kuzidi kukubalika kwake kwa umma.

  HOJA ZA UPINZANI

  Sitta alisema wakati umefika kwa viongozi wa CCM katika ngazi zote, kujibu hoja za upinzani zinazolenga kuikosoa serikali iliyopo madarakani, ionekane haijafanya mambo mazuri tangu kupatikana kwa Uhuru.

  Alisema inashangaza kuona viongozi wa CCM wanashindwa kufanya mikutano yenye lengo la kuelezea mafanikio yanayotokana na utekelezaji wa sera na ilani za chama hicho, hivyo kuwapa mwanya wapinzani ‘kukishambulia’.

  “Tumefanikiwa katika maeneo mengi ya huduma za jamii kama afya, elimu, miundombinu na mawasiliano, viongozi wa CCM katika ngazi zote mnapaswa kuyajua hayo na kuyasema kwa wananchi,” alisema.

  CCM YALIA VIINGILIO, ADA KIDOGO

  Katibu wa CCM wilaya ya Karagwe, Anatory Nshange, alisema mapato kidogo yanayotegemea viingilio na ada za uanachama, ni miongoni mwa vikwazo vinavyochangia kufanikisha mbinu chafu za mafisadi kupenyezwa kwa viongozi wake.

  Nshange ambaye ofisi yake ina hazina ya majengo, ukumbi na eneo la wazi vinavyoweza kutumika kama kitega uchumi, alisema viingilio na ada za uanachama havitoshi mahitaji yao.

  Hivyo alitoa wito kwa Sitta kuifikisha hali hiyo katika ngazi na vikao vya juu vya CCM, ili hatua za kukinusuru chama hicho zichukuliwe.

  Naye Mwenyekiti wa CCM wilayani humu, Justinian Kazungura, alisema ukosefu wa fedha za kujiendesha unaweza kutumika kama mwanya wa wale aliowaita ‘manyang’au’, kuwarubuni ili wawaunge mkono.

  Kauli hiyo ya manyang’au ilitafsiriwa kulenga viongozi na wanachama wa chama hicho ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na tuhuma za ufisadi.

  Hata hivyo, Sitta aliunga mkono hoja ya kuwepo mapato kidogo ya viingilio na ada, ana akaahidi kuwasilisha hoja hiyo Nec ili ubuniwe mfumo utakaoiwezesha CCM katika ngazi ya wilaya kupata fedha zinazokidhi shughuli za uendeshaji.
   
 2. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Naona aliyekuwa mbele kuwagawa wana CCM ni yeye Mh 6. Kayapata majibu kutoka kwa Dr. Slaa yaliyomtosha sasa eti anajuwa kuwa ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe unadhoofisha chama chake.
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu alikuja na thread inasema force kingi hii ndio force kingi yenyewe?
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  mzee kaongea factor moja ambayo ccm wote wanairudia kila mara kwa vile hawan akitengo cha research makini.Kwanza malumbano ndio yanasaidia ccm na ndio maana watu kama yeye wanaonekana kuwa si sehemu ya uozo, na ndio wanaowachanganya wananchi waone kuwa ccm sio mbaya iala watu wachache ambao wanaitwa mafisadi ndio shida.Ila hao mafisadi hata ccm haiijui.

  Mzee kajisahau tena, kajisahau kuwa yeye ndie mmojawapo ya wanaoendeleza malumbano, na kama kweli hiyo ingekuwa ni factor na yeye anaamini hivyo kwanini asingeacha malumbano?Yaani hapo hapo anapinga malumbano huku anayaendeleza kwa kuwazodo awanaoitwa mafisadi.Au ndio kusema kajiruhusu yeye tuu kulumbana?

  Mzee hajui kuwa ccm imefanya uovu sana , na maendeleo waliyoleta ni kidogo sana ukilinganisha na miaka waliyokaa, na umasikini wa watu ambao hawajaona faida zake, CCM imekuwa ikifany ahsara mabzo hata raia asiye na elimu anaona na kupata uchungu.
  Mzee yupo mbali na reality, CCM inaendelea kukubalika?sasa kalalamikia nini malumbano?Au malumbano hayapunguzi kukubalika?ukwelini kwamba CCM inaendelea kukataliwa na kubomoka yenyewe.
  wapinzani wameenda mbali kuonyesha ambayo CCM hijafanya, na yale iliyofanya kwa kiwango cha chini, na yale CCM iliyoshindwa kabisa kufanya.Mzee hajui hoja hapa si kufanya mzuri.Ila kufanya mazuri ya kutosha.Mzee hajui kuwa katik biashara kuna kitu kinaitwa "Thamani halisia",CCM imetumia rasilimali za wananchi na kuwapa kitu kisichofikia dhamani ya kilicholipwa.hapa upinzani aunaongelea ufanisi na viwango, mzee anaongelea hovyo hovyo.
  Sasa kam hakuna waonyeshe nini?wenzie wameamua kuziba hiyo mianya kwa kutumia vyombo vyote ila hakuna walichoweza.Yaani wamekosa cha kuonyesha wakaamua kuzima yasisemwe na yeye akiwa mmojawapo akiwa spika.
  mbona hajawajulisha wakiwa katik vikao vya NEC alipolala na kuamka.Iweje akawaelezee katik mikutano?huyu mzee kimeo taabu kwelikweli, ndio maana ana shida na CDM, anajua watu wamemsitiri ila kaenda wachokonoa akiwa katik mkutano ili waseme alichofanya.Sijui alidhani ni jambo la sifa,ili awaambie CCM kuwa kaenda chukua siri tuu.
  wameshafulia mapema hivi?ndio kukosa ubunifu na utawala bora fedha, na competency katik uchumi na ubunifu wa vetaga uchumi.Hii inaelezea kwanini CCm hawawezi tukomboa kiuchumi.

  Wamebuni ujinga kunyima vyama ruzuku na mengine wakidhani wanaia CDM sasa wao ndio wanajikuta katik ukata.Wafadhili nao wamebana miradi ambayo wangeiba hela.sasa CDM watakuwa na hela zaidi yao+wana mvuto kuliko wao.Kweli mwaka wa giza
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Anatafuta pa kutokea baada ya kuingia choo cha kike.
   
 6. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  mzee 6 (a.k.a dansa) bado yupo yupo...anacheza kila Disco.Ngoja DJ wake aje, kwani walipigisha disco kwake si ma-dj
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  mzee 6 (a.k.a dansa) bado yupo yupo...hajui kama anahitaji siasa gani...anakesha katik majukwaa kama popo..anacheza kila Disco.Ngoja DJ wake aje, kwani waliompigisha disco kwake si ma-dj.Mzee kawa adicted na disco la kisiasa.Akiwa anacheza madisco mengi kiu haijaisha.
   
 8. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bahati mbaya na mlango umejifunga mkuu....kwi kwi kwi
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Sitta ni bogus kabisa...sijui anaongeaga nini huyu mzee
   
 10. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu mzee amesahau kuongeza mambo matatu hapo nayo ni unafiki ,majungu na ufisadi .
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sitta bana ananifurahisha nani anaanzishaga vita huko ccm ka sio yeye?
   
 12. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sitta

  Simply
  Impossible
  To
  Take
  Action
   
 13. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  hee!yaani chama kiko mahututi halafu muongeze ada ya viingilio vya wanachama!hamjui kwa nini Tigo ilipata umaarufu kwa vijana eh!twende sasa na kuongeza hivyo viingilio tuone kama mapato yataongezeka!
   
 14. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  sitta anatapatapa
   
Loading...