Hivi mafisadi waliliona hili kuwa bado maamuzi ya Sitta pale kanuni zikibaki bubu zitatumiwa na anayemfuatia?
2
-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba, Kanuni hizi zitatumika kwa
mambo yote yanayohusu utaratibu wa uendeshaji wa Shughuli za Bunge. (2) Iwapo jambo au shughuli yoyote haikuwekewa masharti katika Kanuni hizi, Spika ataamua utaratibu wa kufuata katika jambo au shughuli hiyo, kwa kuzingatia Katiba, Sheria nyingine za nchi, Kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya Maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge na uamuzi huo utaingizwa katika Kitabu cha Maamuzi ili kuongoza
mwenendo wa baadaye wa uendeshaji wa Shughuli za Bunge.