Sitta, Mwakyembe Mmekubali Kushindwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta, Mwakyembe Mmekubali Kushindwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Mar 2, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Waziri Mkuu Jana alitangaza kuwa Mitambo ya Dowans itawashwa. Baraza la Mawaziri limetoa baraka zote kwa Tanesco kuingia mikataba mingine ya gharama kubwa ya kuzalisha umeme.

  Sitta na Mwakyembe ni wajumbe wa baraza, mbona mmekaa kimya? Je mmekubali kushindwa? Kule kusema mpaka mate yanawatoka mdomoni na viapo vyote kwamba hamkubali, moto utawaka, patachimbika,ndio mmeamua kutuchinjia baharini.

  Nimeamini hakuna mtetezi wa kweli ndani ya zimwi CCM.

  Wananchi ni lazima tufanye kitu, kuna Richmond na Dowans nyingi zinakuja, hawa watu wataendelea kutengeneza matatizo ya umeme (nina uhakika ni ya kutengeza mbona wakati wa uchaguzi hatukuwa na mgawo, na ukaanza mara baada ya uchaguzi, na hukumu ya Dowans ikaja wakati huo, na hii ni ili warudishe mapesa walotumia kwenye uchaguzi) na kutumia kodi zetu kujinufaisha. Mungu inusuru nchi yetu.
   
Loading...