Lissu: Nchi yetu iko njiapanda

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Kwa ufupi


Swali: Tundu Lissu, unautazamaje mustakabali wa nchi kwa sasa?

Lissu: Nchi yetu iko njiapanda. Nasema iko njiapanda kwa sababu hapa tulipofika inabidi ama tusimame kama Taifa kupinga jinsi Serikali inavyoendesha nchi au tunyamaze tupoteze kila

Mwananchi ilifanya mahojiano maalumu na Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu. Pamoja na mambo mengine, alisema nchi iko njiapanda na utawala wa sasa umetoa fursa muhimu kwa upinzani kuimarika. Endelea.

Swali: Tundu Lissu, unautazamaje mustakabali wa nchi kwa sasa?

Lissu: Nchi yetu iko njiapanda. Nasema iko njiapanda kwa sababu hapa tulipofika inabidi ama tusimame kama Taifa kupinga jinsi Serikali inavyoendesha nchi au tunyamaze tupoteze kila kitu.

Na kupoteza kila kitu maana yake ni kupoteza Katiba yetu ambayo inaruhusu mfumo wa vyama vingi, inayolinda uhuru wa mawazo, inayolinda uhuru wa habari, haki za kuishi na haki zetu za msingi. Hapo ndipo tulipo. Hivyo tusimame na kusema sasa imetosha, au tunyamaze.

Swali: Ni nani unafikiri anatakiwa kuyafanya yote haya?

Lissu: Ni sisi wenyewe. Ni makundi mbalimbali katika jamii yetu. Ni vyama vya siasa, taasisi za kidini, vyombo vya habari, vyama vya kiraia na vyama vya wafanyakazi. Taasisi zote hizi za kijamii tutengeneze harakati na kuweka nguvu ya pamoja.

Na hili katika mapambano si kwa akina Nay wa Mitego tu. Katika historia ya mapambano yoyote yale, wasamii siku zote wamechangia sana. Kuna makundi tangu miaka ya 50 wakati wa kupigania uhuru. Kwa hiyo wa kubadilisha hii hali ni kila mmoja wetu.

Kuna watu ambao wasiposhiriki mapambano yanakuwa magumu sana. Kama hakuna vyombo huru vya habari, mapambanao yanakuwa magumu, vivyo hivyo, kama wanasheria wanajifungia wanaendelea na kazi zao tu, mapambano yanakuwa magumu sana.

Swali: Vyama vya upinzani na ninyi ni kama mmekubali hiyo hali, mmezuiwa mikutano ya hadhara mmenyamaza, au mmerudi nyuma?

Lissu: Kimsingi si kwamba tumekubaliana na hii hali, lakini kurudi nyuma yes (ndiyo). Kwenye vita, hii vita ya majeshi, kuna kurudi nyuma kimbinu, kama mbele hakuendeki na adui amejipanga vizuri zaidi yenu, mnarudi kwa ajili ya kujipanga upya.

Sisi tumekabiliwa na hali ambayo hatujawahi kukabiliana nayo tangu tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Kwanza, tangu mfumo wa vyama vingi uanze miaka ya tisini, hoja kubwa ilikuwa kwamba vyama vya upinzani ni dhaifu, havina uwezo wa kufanya mikutano hadi wakati wa uchaguzi, na hii ilikuwa kweli. Na issue (suala) hapa lilikuwa ni namna gani tunajengaje uwezo, leo issue siyo tena hatuna uwezo wa kufanya mikutano, bali hoja sasa ni kwamba walio madarakani wana hofu kubwa na mikutano yetu.

Kwa hiyo tumesafiri kutoka kutukanwa kwamba hatuna uwezo wa kufanya mikutano, hadi walio madarakani wanaona mikutano ya vyama vya siasa ni hatari kwao, na wako tayari kutumia mabavu.

Kuna kipindi walikuwa tayari kutumia jeshi, jeshi lilihamasishwa kuelekea Septemba Mosi 2016 (Siku ya Ukuta), jeshi ambalo wakati linaundwa mwaka 1964 walitoa ahadi kwa Mwalimu Nyerere kwamba ‘hili ni jeshi la wananchi, hatutanyoosha bunduki zetu kwa wananchi wa Tanzania’, lakini mwaka jana, kwa mara ya kwanza nafikiri, bunduki za jeshi, ndege za kivita, magari ya delaya na silaha kubwakubwa ambazo zinatumika kwenye vita zilitolewa barabarani na wanaosema tuna haki ya kufanya mikutano na maandamano kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira hayo unachagua, twende tukauawe au turudi nyuma tufikirie upya.

Nafikiri it was a retreat, no doubt (ilikuwa ni kurudi nyuma, bila shaka). Na kwa kurudi nyuma tulikuwa sahihi kabisa, kwa sababu Serikali, na tulikuja kuambiwa baadaye. Tulitumiwa ujumbe.

Baadaye (Mtoa ujumbe) alikuja kutuambia, ‘jamani, nimeambiwa msitoke, msitoke barabarani.

Swali: Kwa hiyo baada ya kusikia hayo Ukuta ukaishia hapo hapo?

Lissu: No, Ukuta haukushia pale. Ukitaka kujua kuwa tulikuwa sahihi kwa kutofanya maandamano Septemba Mosi 2016, leo nafikiri upinzani dhidi ya Magufuli umetapakaa kuliko ilivyokuwa Septemba mwaka jana. Kwenye media (vyombo vya habari) tu, sasa anaungwa mkono kiasi gani. Ni makundi gani yanajitokea kumuunga mkono kama ilivyokuwa Juni mwaka jana. Upinzani kwa sababu ya sisi kutochukua uamuzi ambao ungekuwa na madhara makubwa, nafikiri kila mtu anayeangalia kwa macho, anajua anakotupeleka.

Pamoja na giza nene hili tunalokabiliana nalo kuna weupe weupe mwingi tu pembeni. Upinzani umekuwa wa jumla kila mahali, siyo wa Chadema peke yake, siyo wa CUF peke yake. Umesambaa unakwenda nje, unaingia kwenye sekta nyingine za kijamii. Na hilo ni jambo jema, ndilo tumaini kwa nchi hii.

Swali: Mnadhani hii ya kukaa hadi mwaka 2020 bila mikutano ya vyama vya siasa itaendelea? Na ikiendelea mtafanya nini?

Lissu: Haitadumu, walifikiria hivi; ukiwanyima mikutano, ukazima Bunge nguvu ya upinzani itapungua. Je, imepungua? Nguvu ya upinzani imekuwa kubwa zaidi na imesambaa zaidi. Kwa hiyo hii ya kuwanyima mikutano na Bunge haina maana tena kwa sababu kila mtu amekuwa mpinzani. Ukisoma mitandao, mimi niko kwenye magroup mengi ya Whatsap, hana tena wanaomuunga mkono, niliwahi kusema hivi vigelegele havitadumu, na sasa hana vigelegele tena.

Watu wa aina hii wanaweza tu kuongoza mahali ambapo hakuna uhuru wa vyombo vya habari na hakuna upinzani.

Bahati mbaya kwa sasa hapa kuna vyombo huru vya habari. Kwa hiyo hii marufuku ya mikutano haina maana kwa CCM, haina maana kwa Magufuli.

Swali: Baada ya hali hiyo kujitokeza na upinzani ukasambaa, Chadema imekaa pembeni ikitazama au kuna jambo inafanya?

Lissu: Hapana, hatujakaa pembeni, tumebadili mbinu ya mapambano kulingana na uwanja wa mapambano ulivyo. Magufuli amezuia mikutano ya hadhara, tunafanya mikutano ya ndani. Tunaji-oganize (tunajipanga) kwelikweli. Ndiyo maana sasa chama kizima kwa maana ya viongozi wakuu wako kaskazini wakitengeneza structure (muundo) ya uongozi tayari kwa mapambano ya 2019 na 2020.

Kipo kitu kingine ambacho hakikuwa cha kawaida, Chadema ilikuwa chama cha mikutano ya hadhara. Siasa zetu zilikuwa ni matukio na mikutano ya hadhara, na kwa sababu hiyo vikao vya ndani havikuwa vya umuhimu sana. Na ilikuwa ukiita mikutano ya ndani watu hawaji, sasa wameona nje tumekwamishwa ukiangalia hii mikutano ya kanda ni kama mikutano ya hadhara. Kuna mahudhurio makubwa na wanachama wana moyo wa ajabu. Wanaona kama tusipofanya mikutano ya ndani tunakwisha.

Mikutano ya hadhara itarudi, CCM wanaihitaji na 2019 ni uchaguzi wa Serikali za mitaa, utafanyika uchaguzi bila mikutano ya hadhara? Na 2020 ni Uchaguzi Mkuu, Mikutano isiporudi baada ya miaka mitatu ya kuzuiwa, tutapambana. Akitaka alete utawala wa kijeshi.

Swali: Kuna watu wanasema mikutano ya ndani ni mkakati na mbinu za Edward Lowassa kuendesha siasa, nini ukweli wake?

Lissu: Nafikiri kuja kwa Edward Lowassa katika siasa za upinzani Tanzania tumeongeza nguvu sana. Ukizungumzia habari za uchaguzi tu, umpende au umchukie, umtukane au umshangilie, huyu mtu ana kura milioni sita kati ya kura milioni 15 zilizopigwa 2015. Kuna watu milioni sita ambao wanasema huyu mtu anafaa kuwa Rais.

Ukichanganya kura za wagombea urais wote tangu mwaka 1995 tulipofanya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, hazifikii kura za Lowassa za 2015. Hivyo ni historic figure. Kiongozi wa kihistoria kwa namna huyu pamoja na uzee wake, siyo mzima sana, na hakuwa mzima kabisa wakati wa uchaguzi, siyo Lowassa wa hiyo miaka ya Kikwete, lakini pamoja na hayo na matusi yote ambayo tumemtukana na sisi tuna sehemu hapo, bado ana nguvu kiasi hicho.

Kwa hiyo huko tunakokwenda kwa influence yake (ushawishi wake), kwa nguvu zake, lakini hatumwachii peke yake, maana Lowassa ni Chadema na Chadema ni Lowassa. Nadhani tunaenda vizuri.

Swali: Ukitanzama huko nyuma kwa jinsi mlivyokuwa mnamsema, mnamtukana, haiwasumbui?

Lissu: Hata kidogo. Nimesema mara nyingi everywhere (kila mahali), mimi ndiye niliyeandika orodha ya mafisadi. Na kama ulikuwapo Mwembeyanga wakati huo tuliisoma mimi na Dk (Willibrod) Slaa, je tuliyoyasema wakati huo mwaka 2007 yalikuwa uongo?

Ukisema yalikuwa uongo, maana yake Richmond haikuwapo. Richmond ilikuwapo. Na tulisema kwenye orodha ya mafisadi, kwamba Lowassa kama Waziri Mkuu alishiriki kwenye Richmond, hakushiriki? Alishiriki. Yalikuwa ni maamuzi ya Serikali ambayo yeye alikuwa Waziri Mkuu.

Kamati ya Mwakyembe ilithibitisha kwamba Lowassa alishiriki, kwamba alibebeshwa mzigo peke yake. Alikuwa Waziri Mkuu lakini hakuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, aliyekuwa kiongozi wa baraza ni Kikwete.

Kamati ya Mwakyembe ilisemaje kuhusu Lowassa, ilisema awajibishwe kwa sababu ya kushindwa kuwasimamia waliokuwa chini yake. Iliwataja watu ambao walifanya makosa na ikapendekeza waachishwe kazi na washtakiwe ni (waliokuwa mawaziri) Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, Mwenyekiti wa Bodi Tanesco, Balozi Fulgence Kazaura, Mkurugenzi wa Nishati, Bashiri Mrindoko, Katibu mkuu, Arthur Mwakapugi na mtu mwingine mmoja.

Dk Mwakyembe na kamati yake walikuwa very clear (wazi) juu ya Lowassa. Uwajibikaji wake ni wa kisiasa. Na sisi kwenye orodha ya mafisadi tulisema alishiriki kwenye Richmond kama msimamizi wao. Na hatukumsema peke yake, tulimsema (Benjamin) Mkapa, (Jakaya) Kikwete, (Nimrod) Mkono, (Andrew) Chenge, Karamagi, Daudi Balali ilikuwa list ya watu 11, were we wrong? Na aliwajibika, alifukuzwa kazi. Hao wengi waliopendekezwa wafukuzwe kazi na washtakiwe walichukuliwa hatua zaidi? Edward Lowassa peke yake kwa sababu alikuwa kiongozi wao.

Swali: Katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020 unaionaje nafasi ya upinzani?

Lissu: Rais Magufuli atajenga upinzani mkubwa sana. Magufuli ni fursa kubwa kwa upinzani. Fikiria alivyokuwa fursa kubwa wiki iliyopita Arusha (kwenye uchaguzi wa TLS. Wanasheria wa Tanzania wamelala kwa miaka zaidi ya 20, lala kabisa. Haya masuala ya nchi hawakuwa na habari nayo kabisa. Si wanasheria walioanzisha NCCR mwaka 1986, si wanasheria walioanzisha mjadala wa vyama vingi mwaka 1983, siyo wanasheria akina (Masumbuko) Lamwai wa miaka ya 1980, (Mabere) Marando, (Ringo) Tenga na (Dk Sengondo) Mvungi. Tulipopata vyama vingi tu, wanasheria wa Tanzania walikwenda kulala. Magufuli amewaamsha usingizini.

Swali: Moja ya mambo yaliyoibeba Chadema ni kuwaamini vijana, nini mnafanya kuelekea 2020.

Jibu: Kuna mtu ameandika mtandaoni juzi, jinsi gani CCM ina utaratibu wa kuwalea vijana na jinsi Chadema tulivyojisahau, nimeandika hapo nikamwambia ‘that’s rubbish’ (hizo ni takataka). Vijana wa CCM ni akina Daudi Bashite, unataka kutuambia nayo ndiyo malezi mazuri ya vijana. Vijana wa CCM ni akina January Makamba, ni akina Nape Nnauye. Nape wa mwaka jana si Nape wa sasa hivi. Nape wa muswada wa vyombo vya habari, Nape wa bao la mkono, Nape aliyezima umeme bungeni, Bunge limekuwa giza (Bunge live).

Chadema ni chama cha vijana. Miaka ya 2004 hakikuwa chama cha vijana, ilibidi mwenyekiti (Mbowe) wakati huo ndiyo ameingia kuwa mwenyekiti, kuwatafuta mmoja mmoja. Halima (Mdee), Zitto (Kabwe), (John) Mnyika sasa wako Chadema. Hilo ndilo tatizo la CCM, hizi kura za Chadema milioni sita karibu asilimia 90 ni za vijana. Angalia bungeni, mimi sijafikisha miaka 50 lakini ni aina fulani ya mzee. Kwa hiyo vijana ni wa kwetu.

Swali: Pamoja na CCM kuwa ndiyo adui yenu mkubwa mbali na udhaifu wao, unaweza kutaja mambo yapi mazuri kwake?

Jibu: Kama nilivyosema CCM ni fursa kweli. Magufuli ni fursa kweli. Amesaidia kila mmoja anajua umuhimu wa upinzani Tanzania, hawa kina Nay wa Mitego, Mwana Cotide (huyu ni wa kwetu) na wengine wamejitokeza. Hawa watu si wa kwetu kwa maana kwamba hatujawatengeneza, lakini wanatoa lugha kama za kwetu. Wametengenezwa na mapambano yetu na Magufuli.

Amefundisha watu umuhimu wa utawala wa sheria, umuhimu wa uhuru wa kujielelza, umuhimu wa mfumo wa vyama vingi vya siasa, amefundisha umuhimu wa Bunge, tulichukuliwa Bunge live kama jambo la kawaida, lakini Magufuli amefundisha umuhimu wake.

Ni kiongozi wa msaada mkubwa sana. Nimeomba appointment (miadi) naye nikamsalimie mimi na baraza la uongozi la TLS, tumeomba appointment tukamsalimie tuzungumza habari za utawala wa sheria na habari za nchi. Marais si huwa wanakaribisha (kicheko). Tunakwenda kujitambulisha. Tunaomba tukutane tujadili masuala ya utawala wa sheria.

Swali: Kwa misukosuko mbalimbali ya kisiasa unayokumbana huna hofu juu ya maisha yako?

Lissu: Ni kweli watu wana hasira na mimi, lakini hawajawahi kunitishia maisha. Kabla sijawa mbaya kiasi hiki, miaka 20 iliyopita nilipokuwa mwanaharakati kwenye Chama cha Wanasheria wa Mazingira (LEAT) pale nilikutana na vitisho. Nilianzisha ugomvi na mfanyabiashara anaitwa Reginald Nolan, huyu aliuzia nchi vifaa vya kijeshi na katika kulipa deni lake, Serikali ya Mkapa ikampatia ekari 20,000 ajenge mabwawa ya kufuga kamba. Tulianza kupambana naye, hapo ndipo tulikuwa tunakuta bahasha za vitisho chini ya mlango katika ofisi zetu pale Kariakoo. Lakini hatukunyamaza. Tulimvuruga yule jamaa akakimbia na baada ya hapo sijawahi kutishwa.

Lakini najua watakuwa wanajiuliza, unamuanzaje yule jamaa, useme nyamaza tutakuua, useme nyamaza tutakufunga, unaanzaje? Lakini kwa siasa za namna yangu, kwa sababu kuna watu wanakuchukia kwelikweli, huwezi kuwa salama na usipotegemea kusumbuliwa utapata shock (mshtuko).

Yote haya yanayonipata sijawahi kushanagaa, sijawahi kukosa usingizi. Hata nikilala Central Police (kituo cha polisi) huwa napata usingizi na ninakoroma kwelikweli. Nikishapata mto wangu, naunganisha chupa tatu za maji nazifunga kwa shati nalala kama kawaida.

Lakini nikisema sikosi usingizi sina maana kuwa napafurahia, hapana. Kule si mahali pazuri hata kidogo. Ni pabaya kwelikweli. Si pazuri hasa kama huna kosa. Nasema kama huna kosa maana najua kesi zangu zote za uchochezi kuwa sina kosa lolote, sheria ileile ninayodaiwa kuivunja imenipa uhuru wa kuzungumza, kuikosoa Serikili na kumkosoa Rais.

Swali: Unapataje muda wa kufanya hayo yote?

Lissu: Muda upo mwingi sana. Hebu fikiria muda unaokaa kwenye kinywaji ukitoka kazini ukapita sehemu, ni mrefu sana tu. Kwa hiyo na mimi huwa napata muda wa kupata kinywaji, nakunywa Tusker, nafanya kazi za TLS na tumeshafanya mikutano kama mitatu hivi, nakaa na mama na watoto, nahudhuria kesi hata sasa nimetoka kwenye kesi ya Mbunge wa Kilombero Lijualikali, nadhani kesi anaweza kuachiwa, jimboni huko kuna shida kidogo. Sijaenda muda mrefu, mwaka mzima huu sijapata muda wa kwenda, na wale watu wa kule wanataka mtu uwepo. Lakini ukisema uende, unajikuta una kesi, ukitoka mnaandika ameruka dhamana.

Swali: Vipi kuhusu suala la Ben Saanane, mbona mmenyamaza, limeshaje?

Jibu: Ben Saanane alitekwa nyara. Ni kazi ya vyombo vya usalama. Kisa kuhoji mambo yanayogusa viongozi na alifanya hivyo mara kwa mara bila kuacha. Aliandika sana mtandaoni. Kwa hivyo Serikali na vyombo vyake wanao uwezo wa kumsaka kwa kutumia simu zake, kama alitoka nje ya nchi wao ndiyo wanadhibiti mipaka, kama alikufa akazikwa na manispaa waeleze ni watu wangapi na wapi walikufa wakazikwa na manispaa na makaburi yao yako wapi. Kimya ni kwa sababu wanajua wanafanya nini na yuko wapi.

Nilikutana na mtu wa vyombo vya usalama (hakumtaja), alisema alifuatilia suala la Saanane na kufahamu alikodakiwa Novemba 16, 2016 na kuwa akipewa amri na IGP au DCI anaweza kukamata watu. Haya ujumbe alionyesha kuwa anatishiwa ulikabidhiwa polisi lakini wameendelea kukaa kimya.




 
Perfect Question-Perfect Answers (Nb;for somehow).

Maarifa yamekomboa watu wengi duniani kuliko vita vyote vilivyowahi kupiganiwa katika Hostoria ulimwenguni.Upinzani wayatafute maarfa kwanza then mengine yafuate baadaye.Dola inamuogopa mwenye maarifa,haimpendi na siyo rafiki naye.Knowledge First.

Upinzani wa-react haraka sana na professionally,waki-react un-prefessionally imekula kwao.Hii seriKALI ni KALI kweli kweli,inapenda KUPIGA TU (PT) na hawataki uikosoe (Utadhani wao ni Malaika wasiokosea).

Suala la Kupotea kwa Ben Saanane kimiujiza Mh Lissu kalijibu kisiasa sana (Narrow answer) sijapata kuona.Ni lini waliita press conference na kuuambia umma juu ya Maendeleo ya alipo Ben?.Au ni lini tumewaona au hata kuwasikia wakilifuatilia hili suala kisheria?.

Kuhusu kutokuwa na hofu na Maisha yake Mh Lissu katunywesha Chai,Lissu kuna sehemu anawaya.Suala la September Mosi mwaka jana ilinipa picha ya kipekee juu ya Uoga wa wanasiasa wa upinzani kiujumla.Hawajaisoma LONG WALK TO FREEDOM ya Mandela japo wajifunze machache kupitia istilahi ya neno Harakati?.Hawajamsoma Bikko,Martin Luther King Jr,Malcom X nk?.

Mwanasheria kushika Bango Mbele ya Bunge kupinga ukandamizwaji umewahi kuona wapi?.Kama mwanasheria anashika bango (Means Sheria hazipo) ,Je sisi akina holoi poloi tukamate nini siku tukikandamizwa?.

Hizi ni hesabu,Inatakiwa turudi darasani.
 
Back
Top Bottom