Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Gazeti la Mwananchi limetuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Spika Mstaafu Mzee Sitta akiaahidi ya kuwa ataendeleza moto ule ule aliokuwa nao katika kutetea haki za wanyonge...............
Vile vile, gazeti la Nipashe limeripoti ya kuwa Mheshimiwa Sitta kaahidi ya kuwa ataendelea kuwa mkweli na unafiki kwake ni mwiko...............
Nionavyo huu ni ujumbe mzito kwa JK kama alifikiri Mzee wetu Sitta sasa amemziba mdomo kwa kumkata ngwala ya Uspika lakini Bungeni Mzee wetu Sitta atachachamaa kuhakikisha haki za wanyonge zinalindwa...............Hongera Mzee Sitta kwa huo ujasiri uliouonyesha kwetu......maana huko bungeni hatuna makimbilio mengi tukizingatia Chama cha mafisadi ndicho kimekamata hilo bunge na sijui tutaponea wapi..............na hivi sasa wanakazana kuanzisha hoja za udini ambazo hazipo ili tusahahu matabaka ya kimapato ambayo ndiyo chimbuko la migawanyiko kwetu.............
Mr. Sitta unauma na kupuliza lakini sioni haja kwake kuwa waziri alifikia rank kubwa kwa nini aombe chini kama alivyo Lowasa PM urudi kuwajibika current PM uroho huo wa madaraka
Kama nia yake ni heshima kutoka kwa wanyonge, basi abaki mbunge!
Nilisikia kua amekataa uwaziri?
Hatakua na nguvu sana maana kuna party caucas, kama walitaka kumvua uanachama akiwa spika nini kitawazuia sasa hivi hana cheo chochote? I think he need to be very careful now maana yuko exposed sana kwa sasa. By the way nini kinamzuia kuasi na kutimka ili apambane kwa uhuru na uwazi? Sitta make up your mind now, jump the ship or keep quite. If you jump the ship ur legacy will never fade whether alive or dead, now make a decision before its too late
Sitta kamwe hawezi kuwa mwiba kwa CCM wakati ni mmoja wao..........................inabidi atoke huko halafu kura irudiwe kule Urambo Mashariki na atarudi tu bungeni kwa tiketi ya Chadema na ikibidi awashawishi wabunge wengi wa CCM kuachia viti vyao ili kukiondoa CCM madarakani................................kwa mchango huo tutamkumbuka kuwa kweli alikuwa ni jemedari wa taifa hili.......................By the way nini kinamzuia kuasi na kutimka ili apambane kwa uhuru na uwazi? Sitta make up your mind now, jump the ship or keep quite. If you jump the ship ur legacy will never fade whether alive or dead, now make a decision before its too late
Huyu Sitta kwa watu wanaomfahamu ni mnafiki babu kubwa!! Kukubali kwake kuwa waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki, ndio mwisho wa heshima aliojijengea pale bungeni kama Sipika na pia inadhihilisha yale yaliyosemwa kuwa maamuzi yake mengi pale bungeni hayakuwa kwa sababu ya uamini wale[ principles] bali yalikuwa kuwathibiti wapinzani wake kisiasa; kama kweli angekuwa mtu mwenye msimamo asingekubali uwaziri aliopewa wakati yeye alikuwa kiongozi wa moja ya mihimili ya serikali ya jamhuri!!