Sitta autamani Urais 2015

Hollaaaaaaaaaaaaaaaaa, "Wazee hawatakiwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Tangu 70's mtu yuko kwenye uongozi wa serikali!!??????? Aibuuuuuuuuuuu.
 
Asante kwa kutujulisha kuwa huyu naye anautaka urais. Nikupe angalizo: Watanzania leo tunajua tunachokihitaji. sasa huivi tupo busy tukiwapima wale wanaonyesha nia ya kuutaka Urais. Itakapofika wakati, tunaomba mtupe nafasi ya kuamua nani anatufaa kuwa rais wetu na wala msituletee mizengwe baada ya kuamua
 

Duh!Jf kiboko mpaka sitta naye yupo humu?
 

Sijui kama uko sahihi kwa kusema Mheshimiwa 6 ndo anafaa au la lakini nitapisha na wewe katika haya:

a) Eti asiwe mtu wa kulipiza VISASI. Kisasi ndio dawa ya mwonevu!!! Ni katika kutolipizana visasi ndio tumetoa wezi wa muda mrefu ambao hata wakijulikana, tunawaomba wajiuzulu au tunawafukuza kazi badala ya kuwanyang'anya walivotuibiwa na kuwatupa magerezani wakalie na kusaga meno. Magereza yamejaa vibaka, wezi wa kuku na simu za tochi. Huko hakutakuwa kwa wezi wa EPA, Dowans, Richmond, Loliondo, Kiwira, nk kama hatutakuwa na visasi kwa makosa yao!!

b) Hakuna hiari isiyofuata na adhabu, katika sheria za nchi. Kukubali kosa na kurudisha ulichoiba hakuondoi kosa kuwa uliiba wala kuondoa adhabu yake. Kunapunguza kiasi cha adhabu. Kuwaomba warudishe kwa hiari yao na wasiporudisha unapotezea kwa "hakuna ushahidi waliiba", "hatuwajui ni akina nani" - HAIKUBALIKI!!!!!

Ninamtaka Rais ajae awe na visasi ili tuchukue hatua hata kwa mambo yaliyopita. John Demyanyuk amefungwa mwaka 2011 kwa makosa aliyofanya Auchwitz kabla ya mwaka 1945!!!! Tusipojenga utamaduni wa kuhukuma na kuadhibu makosa ya miaka ya nyuma, mwisho tutakuwa taifa lisilojifunza kutokana na makosa!!!
 
Sitta mie binafsi uwa simuelewi kila siku analalamika ufisadi ufisadi lakini hawataji hao mafisadi.
 
“Mimi ni mtaji wa urais”, hii ni kauli iliyowahi kutolewa na Mzee Samuel John Sitta mwanasiasa mashuhuri hapa nchini.Mazingira yaliyopelekea yeye kujinasibu kwa kauli hiyo ilikua ni kwamba kila chama cha siasa hapa nchini kilikuwa kinammezea mate awe mwanachama wake, ikiwani pamoja na Chama cha Kintelijensia CCJ.

Nikweli, habari za kuaminika nikwamba katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, Mzee Sitta alikuwa ktk mafungamano ya kugombea URAIS kwa tiketi ya CHADEMA akawatosa CHADEMA ktk dakika za majeruhi. Ndipo CHADEMA wakalazimika kumsimamisha Dr. Slaa.

Wanasiasa hawa huzaliwa, hukua, hufundwa na kukomaa kulitumikia taifa kutokana na sababu ama mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchambuzi na tathmini tunazowafanyia sisi wanaotuongoza.

Hoja yangu katika uzi huu ni kuhoji je baada ya Uchaguzi wa Wajumbe wa NEC ya CCM Mzee Sitta yuko na hadhi ileile ya kuwa MTAJI WA URAIS? NA KAMA JIBU NI NDIYO, KWA CHAMA GANI KAMA CCJ NA CHADEMA ALIPATA KUWALAGHAI?

Karibuni WanaJF katika mjadala, uchambuzi na tathmini juu mwanasiasa huyu na hatma yake ktk siasa za nji hii.
 
Sita mnafiki tu hana lolote. Utapulizaje dawa ya wadudu chumban wakat we mwenyewe upo humohumo?
 
Spent force! Uspika ulimshinda ata uweza urais ? Bora tuongozwe na mchuizi kuliko mtu mwenye wivu na visasi
Wivu wa uchoyo ni mbaya sana katika kuongoza nchi
Atataifisha kila kitu kama baba yake

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Dah mkuu hiyo heading imenishtua nilifikiri unasema sintah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…