Sitta ampinga Makinda kuhusu mabunge mawili

Obesity

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
111
Reaction score
46
SPIKA wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ametofautiana na mrithi wake, Anne Makinda kuhusu muundo wa Bunge katika Katiba Mpya, akisema nchi inahitaji Bunge moja tu.

Akitoa maoni yake Januari 15 mwaka huu, mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Spika Makinda alitaka kuwe na mabunge mawili; la kuchaguliwa na wananchi na lile la Seneti litakalotokana na wataalamu mbalimbali na viongozi wa zamani wenye uzoefu wa kuitumikia nchi.

"Tumetaka Bunge la Seneti lijumuishe viongozi waliolitumikia taifa ambao tunajua kwamba watakuwa na uzoefu wa kutosha katika masuala muhimu ya nchi. Tumetaka pia bunge hilo liwe na wataalamu wa mambo mbalimbali ili kuhakikisha tunakuwa na Serikali imara."

Alisema hatua hiyo itasaidia kwani Bunge la Seneti litaondoa mambo ya itikadi za vyama bungeni kama ilivyo sasa na kujali masilahi ya taifa. Lakini akizungumza muda mfupi baada ya kutoa maoni yake mbele ya Tume hiyo Dar es Salaam jana, Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema hakuna haja ya kuwa na mabunge mawili, kwani bado nchi haina uwezo wa kumudu gharama za uendeshaji wake.

"Kiukweli sioni kama kuna haja ya kuwa na mabunge mawili kwani uwezo wetu wa kuendesha mabunge hayo bado ni mdogo. Ninachopendekeza ni kwamba Katiba Mpya ieleze wazi kwamba bunge linatakiwa kuwa na idadi fulani ya wabunge."

Maadili ya viongozi

Sitta pia alizungumzia suala la maadili na kusema Tanzania inakabiliwa na tatizo la uadilifu wa viongozi na kupendekeza kuwa Katiba Mpya iwe na kipengele cha kuwabana wanaotaka kuwa viongozi kwa kuthibitisha maadili yao. Alisema Katiba Mpya inapaswa iwe na kifungu kitakachowalazimisha viongozi kuwa wawazi na waadilifu akisema amependekeza hayo kutokana na viongozi wengine kuonekana kutokuwa na maadili.

Alisema amependekeza kuwa kifungu hicho kitamke wazi kwamba mtu anapotaka kuomba nafasi ya uongozi akubali kuhojiwa hadharani ili kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na viongozi waadilifu. "Tusipokuwa na viongozi waadilifu taifa litaelekea sehemu mbaya kwani watu wanapeana nafasi za uongozi kwa kujuana kitu ambacho mwisho wake wanyonge wataendelea kuwa chini na kukosa haki zao," alisema.

Waziri Sitta alitoa mfano katika Ibara ya 39 ya Katiba ya sasa inayoeleza sifa mbalimbali ambazo anapaswa kuwa nazo kiongozi wa ngazi ya juu, lakini hakuna kifungu kinachoeleza masuala ya uadilifu. Alisema Katiba ijayo kuwe na kifungu kitakachosema kwamba sifa mojawapo ya kiongozi ni kuwa mwadilifu.

Mahakama ya Katiba

Waziri Sitta pia alipendekeza kuwa Katiba Mpya itambue uwepo wa Mahakama ya Katiba itakayokuwa inashughulikia kesi za uchaguzi. Alisema kuna malalamiko mengi ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na watu kwenda kinyume cha Katiba hivyo kusisitiza kuwa uwepo wa chombo hicho utasaidia kupunguza malalamiko ya ukiukwaji wa Katiba.

Pia alipendekeza kutambuliwa kwa mgombea binafsi katika Katiba Mpya ili kuongeza wigo wa demokrasia nchini... "Kuna watu wana uwezo wa kuongoza lakini hawako katika vyama, hawa wanapaswa kupata haki ya kuchaguliwa pia badala ya kuwalazimisha wawe kwanza wananchi wa chama cha siasa."

Kuhusu Muungano alisema hakuna haja ya kuwa na Serikali tatu kwani huko kutakuwa ni kuuvunja Muungano uliowekwa na waasisi wa taifa hili. Alisema anapendekeza Katiba Mpya iendeleze Muungano uliopo sasa kwani hakuna kitu chochote kinachouathiri.

"Ninavyoona ni vyema tukabaki na Serikali mbili kama kawaida. Hakuna haja ya kuwa na Serikali tatu kwani huko kutakuwa ni kutaka kuuvunja Muungano uliopo sasa," alisema.

source:Gazeti la mwananchi
 
Kwa hiyo suala la mabunge mawili hoja ni gharama tu sio? Nilidhani kuna zaidi ya hilo
 
Bi kiroboto kaona uwezekano wa kutokuwa na wabunge toka kwenye chama lao libovu anataka hao wa zamani ambao ni wengi toka kwenye chama chao wakajae huko nakuendekeza upumbavu kama huu wanaoendekeza ktk bunge la sasa
 
Sikubaliani na Sitta kwamba kubadilisha muundo wa muungano ni kuvunja MUUNGANO. Hii ni childsh argument.

Nakubaliana na Sitta kuwa mabunge mawili hayafai na ni gharama kubwa kwa nchi "masikini" kama Tanzania.
 
Mkapa alikuwa sahihi kutoa maoni yake kimya kimya
 
Mengine nakubaliana na 6 but hilo la Muungano kama si serikali 3 basi na Muungano ufe kifo cha kawaida. Muungano wa serikali mbili umechochea chuki na utengano wa kila upande kulalamika kwa kuchanganya mambo ya muungano na yasiyo ya muungano
 
Sikubaliani na Sitta kwamba kubadilisha muundo wa muungano ni kuvunja MUUNGANO. Hii ni childsh argument.

Nakubaliana na Sitta kuwa mabunge mawili hayafai na ni gharama kubwa kwa nchi "masikini" kama Tanzania.

Nakubaliana na Sitta kuwa kuwa kubadilisha muundo wa muungano ni kuvunja muungano kwasababu ametazama mbali..kutakapokuwa na serikali tatu muundo huo utaleta matabaka na kupelekea kuanzishwa kwa itikadi mpya za kisiasa...KWA HILO ALIONA MBALI
 
Huyu mzee Sitta ni kichwa, sema tu yupo kwenye chama mufilisi
 
Nakubaliana na mheshimiwa Sita 100%. Mabunge mawili ni kuongeza gharama zisizo za lazima wakati nchi ikikabiliwa na upungufu mkubwa katika upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo maji safi na salama kwa watu wake.
 
Nimeona issue ya UADILIFU, kumbei bado anamkomaa na yule hasimu wake mkubwa
 
Tuesday, January 22, 2013

SPIKA wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta ametofautiana na mrithi wake, Anne Makinda kuhusu muundo wa Bunge katika Katiba Mpya, akisema nchi inahitaji Bunge moja tu.

Akitoa maoni yake Januari 15 mwaka huu, mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Spika Makinda alitaka kuwe na mabunge mawili; la kuchaguliwa na wananchi na lile la Seneti litakalotokana na wataalamu mbalimbali na viongozi wa zamani wenye uzoefu wa kuitumikia nchi.

"Tumetaka Bunge la Seneti lijumuishe viongozi waliolitumikia taifa ambao tunajua kwamba watakuwa na uzoefu wa kutosha katika masuala muhimu ya nchi. Tumetaka pia bunge hilo liwe na wataalamu wa mambo mbalimbali ili kuhakikisha tunakuwa na Serikali imara."

Alisema hatua hiyo itasaidia kwani Bunge la Seneti litaondoa mambo ya itikadi za vyama bungeni kama ilivyo sasa na kujali masilahi ya taifa.

Lakini akizungumza muda mfupi baada ya kutoa maoni yake mbele ya Tume hiyo Dar es Salaam jana, Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema hakuna haja ya kuwa na mabunge mawili, kwani bado nchi haina uwezo wa kumudu gharama za uendeshaji wake.

"Kiukweli sioni kama kuna haja ya kuwa na mabunge mawili kwani uwezo wetu wa kuendesha mabunge hayo bado ni mdogo. Ninachopendekeza ni kwamba Katiba Mpya ieleze wazi kwamba bunge linatakiwa kuwa na idadi fulani ya wabunge."

Maadili ya viongozi
Sitta pia alizungumzia suala la maadili na kusema Tanzania inakabiliwa na tatizo la uadilifu wa viongozi na kupendekeza kuwa Katiba Mpya iwe na kipengele cha kuwabana wanaotaka kuwa viongozi kwa kuthibitisha maadili yao.

Alisema Katiba Mpya inapaswa iwe na kifungu kitakachowalazimisha viongozi kuwa wawazi na waadilifu akisema amependekeza hayo kutokana na viongozi wengine kuonekana kutokuwa na maadili.

Alisema amependekeza kuwa kifungu hicho kitamke wazi kwamba mtu anapotaka kuomba nafasi ya uongozi akubali kuhojiwa hadharani ili kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na viongozi waadilifu.

"Tusipokuwa na viongozi waadilifu taifa litaelekea sehemu mbaya kwani watu wanapeana nafasi za uongozi kwa kujuana kitu ambacho mwisho wake wanyonge wataendelea kuwa chini na kukosa haki zao," alisema.

Waziri Sitta alitoa mfano katika Ibara ya 39 ya Katiba ya sasa inayoeleza sifa mbalimbali ambazo anapaswa kuwa nazo kiongozi wa ngazi ya juu, lakini hakuna kifungu kinachoeleza masuala ya uadilifu. Alisema Katiba ijayo kuwe na kifungu kitakachosema kwamba sifa mojawapo ya kiongozi ni kuwa mwadilifu.

Mahakama ya Katiba
Waziri Sitta pia alipendekeza kuwa Katiba Mpya itambue uwepo wa Mahakama ya Katiba itakayokuwa inashughulikia kesi za uchaguzi.

Alisema kuna malalamiko mengi ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na watu kwenda kinyume cha Katiba hivyo kusisitiza kuwa uwepo wa chombo hicho utasaidia kupunguza malalamiko ya ukiukwaji wa Katiba.

Pia alipendekeza kutambuliwa kwa mgombea binafsi katika Katiba Mpya ili kuongeza wigo wa demokrasia nchini... "Kuna watu wana uwezo wa kuongoza lakini hawako katika vyama, hawa wanapaswa kupata haki ya kuchaguliwa pia badala ya kuwalazimisha wawe kwanza wananchi wa chama cha siasa."

Kuhusu Muungano alisema hakuna haja ya kuwa na Serikali tatu kwani huko kutakuwa ni kuuvunja Muungano uliowekwa na waasisi wa taifa hili.
Alisema anapendekeza Katiba Mpya iendeleze Muungano uliopo sasa kwani hakuna kitu chochote kinachouathiri.

Mwananchi

Hivi majuzi spika wa sasa wa bunge akitoa mapendekezo kwenye tume ya mabadiliko ya katiba alisema kuwa inafaa tanzania iwe na mabunge mawili eti bunge elect na senet!!!! Hii kuiga iga inashida kweli!!!! Sasa spika wa zamani ndugu samweli sita kampinga kasema mabunge mawili ya nini ,,......hapa namuunga sita mkono...ndo maana sipati sababu ya sita kuvuliwa uspika!!!!
 
Hivi majuzi spika wa sasa wa bunge akitoa mapendekezo kwenye tume ya mabadiliko ya katiba alisema kuwa inafaa t eti bunge elect na senet!!!! Hii kuiga iga inashida kweli!!!! Sasa spika wa zamani ndugu samweli sita kampinga kasema mabunge mawili ya nini ,,......hapa namuunga sita mkono...ndo maana sipati sababu ya sita kuvuliwa uspika!!!!

Huu ni upuuzi!
 
Mie natamani hata hili moja lisiwepo asilimia 85 ya wabunge ni ovyo kabisa wanachukulia ubunge kama ulaji nakuvuna pesa...kazi mojawapo ya bunge nikutunga sheria fanya utafiti leo wabunge wanaohusika kutunga sheria kila panapokuwa na mswaada sana sana ni Godfrey Zambi,John Mnyika na Zitto wengine wapo wapo,tena asimia kubwa ya wanaotoka magamba ndo hamna kitu kabisa.
 
mwana sheria vis a vis karani wa hesabu, aliyepevuka vis a vis asiye pevuka, aliyebebwa kupata uspika vis a vis aliyetoswa
 
mabunge mawili ya kazi gani, ikiwa hili moja tu linatufilisi.!
 
Back
Top Bottom