Sitta ameliona hili mapema

Zuwely salufu

Senior Member
Oct 7, 2012
105
20
Nimemsikiliza mh. Sitta na nimemwelewa kile alichokimaanisha, kama kweli tunahitaji katiba mpya tulitazame suala hili la kipengele cha serikali tatu itakuwaje kiitifaki? Kwanini tusiwe na rais mmoja wa muungano then znz na tanganyika ikawa na governers instead of rais?
 
Hivi nyinyi watu mbona Majina majina yamewakaa sana? Raisi ni jina tu hata tunaweza neno Spika wa Bunge tukalibadilisha ana kuita Raisi wa Bunge, au Mkuu wa Chuo tukamuita Raisi wa Chuo!

Cha muhimu SIO mtu anapewa jina gani, bali cha muhimu ni yule mtu ana MADARAKA gani, hilo ndio muhimu, hivyo hao Viongozi wa TZ Bara na Zanzibar wanaweza kuitwa vyovyote vile Raisi, Sultani, Watemi, n.k ila watakuwa na majukumu gani kwa mujibu wa Katiba ndio muhimu!

ulaji binafsi kwanza, utaifa baadae!
 
Nimemsikiliza mh. Sitta na nimemwelewa kile alichokimaanisha, kama kweli tunahitaji katiba mpya tulitazame suala hili la kipengele cha serikali tatu itakuwaje kiitifaki? Kwanini tusiwe na rais mmoja wa muungano then znz na tanganyika ikawa na governers instead of rais?
Haya mambo ya mchakato wa katiba kiukweli tusipokuwa makini wanyonge tutakiona cha moto.
 
anashangaa marais watatu nchi moja? je aliona wapi marais wawili nchi moja? mbona vyote hivyo vioja?
 
Hivi nyinyi watu mbona Majina majina yamewakaa sana? Raisi ni jina tu hata tunaweza neno Spika wa Bunge tukalibadilisha ana kuita Raisi wa Bunge, au Mkuu wa Chuo tukamuita Raisi wa Chuo!

Cha muhimu SIO mtu anapewa jina gani, bali cha muhimu ni yule mtu ana MADARAKA gani, hilo ndio muhimu, hivyo hao Viongozi wa TZ Bara na Zanzibar wanaweza kuitwa vyovyote vile Raisi, Sultani, Watemi, n.k ila watakuwa na majukumu gani kwa mujibu wa Katiba ndio muhimu!

Wewe mjanjaaa!unajua tatizo tulilo nalo watanzania ni kutotaka kwenda mbali na maamuzi yetu,hatujui tunataka nini kwa ajili ya nini na tutatimizaje utashi wetu.
Ni kweli kabisa katika muundo huo ni muhimu tujue kwa kina madaraka na mipaka ya hao maraisi vinginevyo itakuwa shida nene!asante kwa point yako murua!
 
Serikali mbili tu, Tanganyika na Zanzibar kama vile awali na mambo ya muungano wananchi wapime wenyewe au tukutane kwenye shirikisho la Africa Mashariki basi.
 
mimi mpaka hapa tulipofikia naona kabisa HASARA ZA MUUNGANO ZIMEKUA KUBWA KULIKO FAIDAZAKE
Nibora tuu kuachana hata bila kuogopa nasaha za nyerere @@@@@potelea mbali bwana.
 
Kinachodaiwa hapa si urais ni mamlaka za juu kuwa tatu kiitifaki itakuwaje ndio inayoleta shida ndio linakuja wazo la kupunguza baadhi ya mambo ambayo hayawezi kuleta mkanganyiko kiutendaji
 
kwani Sita ndio kaona hili mkuu? Kwani wewe hujaona serikali tatu sio issue? Yaani marais watatu kimtindo kisa muungano.
Tunahitaji kerikali mbili. Kwani tukikutana EAC hatutakuwa tumeungana? Kisa ni kura za wazanzibar kwenye uchaguzi mkuu tu.
 
Hivi nyinyi watu mbona Majina majina yamewakaa sana? Raisi ni jina tu hata tunaweza neno Spika wa Bunge tukalibadilisha ana kuita Raisi wa Bunge, au Mkuu wa Chuo tukamuita Raisi wa Chuo!

Cha muhimu SIO mtu anapewa jina gani, bali cha muhimu ni yule mtu ana MADARAKA gani, hilo ndio muhimu, hivyo hao Viongozi wa TZ Bara na Zanzibar wanaweza kuitwa vyovyote vile Raisi, Sultani, Watemi, n.k ila watakuwa na majukumu gani kwa mujibu wa Katiba ndio muhimu!

Kwahiyo kiongozi mkuu wa bara na visiwani aitwaje?
Mleta mada ameeeleza sababu ya kutoitwa rais
Wewe unasema rais ni jina tu haya mfano tukuimuita mpumbavu, kichaa, mtumwa na hayo si majina mtu!!!

Mimi nafikiri cheo cha Urais kiwe kimoja tu, huyu kiongozi mkuu wa Zanzibar na Tanganyika waitwe Waziri Mkuu na wachagulie na wananchi
 
kwani Sita ndio kaona hili mkuu? Kwani wewe hujaona serikali tatu sio issue? Yaani marais watatu kimtindo kisa muungano.
Tunahitaji kerikali mbili. Kwani tukikutana EAC hatutakuwa tumeungana? Kisa ni kura za wazanzibar kwenye uchaguzi mkuu tu.

haddidu za rejea walizopewa mojawapo ni uwepo wa muungano, kwa maslahi ya nani?? kwa faida gani?? Nyerere angekuwepo leo angeshauvunjilia mbali kwani unadidimiza kasi ya maendeleo kwa Znz na TZ bara..
 
Twende kwenye maoni ya hii rasimu na badaye bunge la katiba majibu yote yako wazi.
 
Kwahiyo kiongozi mkuu wa bara na visiwani aitwaje?
Mleta mada ameeeleza sababu ya kutoitwa rais
Wewe unasema rais ni jina tu haya mfano tukuimuita mpumbavu, kichaa, mtumwa na hayo si majina mtu!!!

Mimi nafikiri cheo cha Urais kiwe kimoja tu, huyu kiongozi mkuu wa Zanzibar na Tanganyika waitwe Waziri Mkuu na wachagulie na wananchi

Swala hapa sio JINA unaweza hata ukamuita mpumbavu kama ulivyosema, swala ni kwamba Katiba inampa madaraka gani huyu mtu mwenye hilo jina?
Hiyo ndio hoja ya kujadili na SIYO kiongozi wa TZ Bara au Zanzibar ataitwaje, tunaweza kupendekeza jina lolote lile tunaweza tukamuita Waziri Mkuu, Waziri kiongozi, Raisi, Makamu wa Raisi, Mfalme, Mtemi n.k ila huyu Mtu atakuwa na Madaraka gani au kazi yake itakuwa nini katika hiyo Katiba? Hilo ndilo la muhimu!

Majina hayasemi chochote Kanari Gadafi alikuwa hajiiti Raisi, lakini Madaraka yake yalikuwa tu kama Raisi mwingine yoyote!

Akili ndogo ikishindwa tambua jambo huliita baya.....inakuwa ngumu zaidi kwa akili ndogo pale akili KUBWA inaassume vitu fulani ni too obvioous na hivyo havihitaji kutolewa maelekezo.

ccm ni kutu ktk chuma.Wanaweza ua kwa fahari kwa vile hawajui wafanyalo.
 
Back
Top Bottom