Lile zimwi la kutokukubalika kwa diwani wa kata ya Olorien kama Meya wa jiji la Arusha limeendelea kumwandama Diwani huyo leo baada ya kupata mapokezi hafifu kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt. Teresia jijini Arusha inayoongozwa na Mh. Samwel Sitta. Tofauti na wageni wengine waliokuwa wakishangiliwa kwa vigelegele na makofi wakati wa utambulisho, Mh. Gaudence Lyimo hakupata mapokezi hayo kutoka kwa waumini hao kama wenzake. Waumini walionyesha kupoa hadi alipotangazwa mgeni mwingine ndipo hali iliporudi kama awali.
Mbunge wa Arusha ameendelea kutomtambua "Meya" huyo kwa kumtambulisha kama diwani huku akimwomba Mh. Sitta kuongea na wakubwa wake ili wakamilishe haraka kuumaliza mgogoro uliopo kupitia kamati iliyoundwa na Pinda na Mbowe.
Ninachojiuliza ni kwamba, ni lini atapata hekima ya kujiuzulu hiyo nafasi ili apate tena heshima kwa jamii ya Arusha. Licha ya kampuni yake ya ujenzi kufanya miradi mingi ya kanisa hilo kabla ya mgogoro huo, waumini hao hawamdhamini tena kama awali. Poor him!