Sitta ajitoa mhanga kumaliza ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta ajitoa mhanga kumaliza ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 30, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,494
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Arusha;
  Tarehe: 29th September 2009

  Habari Leo

  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, ametangaza rasmi kuwa amejitoa mhanga kupambana na ufisadi ili nchi isiangamie.

  Sitta amesema, ufisadi nchini ni wa kiwango cha juu hivyo yeye na baadhi ya wabunge wameamua kujitoa mhanga kupambana nao, na hawafanyi mzaha.

  Amesema, ufisadi unatisha Tanzania, na kwamba, mafisadi wanaiangamiza nchi.

  “Nyinyi vijana mnakua wakati wa mikataba hii mibovu mimi naweza kuwa nimeshakufa kwa wakati huo, ndio maana baadhi ya watu wakiwemo baadhi ya wabunge wanachukia rushwa,” Sitta amewaeleza waandishi wa habari leo mjini Arusha.

  Rais huyo wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola amesema, gharama za ufisadi nchini zinaweza kuambukiza vizazi vijavyo.

  “Rushwa ni tatizo kubwa katika bara letu la Afrika, wala rushwa wanatumia utajiri wao kuingia kwenye siasa huku wakiwa na nguvu kubwa ya kiuchumi,” amesema Sitta.

  Ametoa mfano wa ufisadi huo nchini kuwa ni viongozi wa Serikali kusaini mikataba feki itakayoliingiza taifa kwenye gharama kubwa siku zijazo. Amesema,Tanzania itaonja machungu ya gharama hizo kupitia madeni.

  “Sasa tunatumia kama asilimia 35 ya bajeti kwa ajili ya kulipia madeni ya nje; lakini kuna uwezekano wa kufikia asilimia 50 kama tutaendelea kuingia mikataba feki na ikifikia hapo tumekwisha.

  “Ufisadi umefikia hatua ya juu ndio baadhi yetu hatufanyi utani na tumeamua kujitoa mhanga kupambana dhidi ya wahusika wa ufisadi huo.

  Kwa mujibu wa Sitta, mwaka jana Afrika ilipoteza takribani dola za marekani bilioni 20 kutokana na vitendo vya ufisadi. “Kiasi hiki ni kikubwa kwani ni zaidi ya msaada ambao bara hili linapata, hii ni hatari kubwa.

  Sitta amesema, mkutano huo wa CPA utalijadili suala hilo la ufisadi wakati watakapokuwa wanajadili moja ya mada zitakazowasilishwa.

  Amesema, rushwa ni chanzo cha migogoro mingi Afrika kwa kuwa watu wachache wana utajiri walioupata kwa njia ya rushwa, wananchi wengi ni masikini.

  Kwa mujibu wa Sitta, watu wamekuwa wanakasirishwa na ustawi huo kwa watu wachache na hivyo kuwa chanzo cha mapigano na migogoro isiyokwisha katika baadhi ya nchi.

  Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, kitendo cha watu wachache kumiliki uchumi na kuwa na nguvu kubwa ya kisiasa kunasababisha watu wengi wawe masikini.

  Katika mkutano huo baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni Serikali ya mseto, majukumu ya Bunge katika kutoa habari kwa jamii, na mabadiliko ya hali ya hewa.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  Mhhhh.yangu macho,,,,,,,,nasubiri nione calculation zake,hasa
  wakati wa uchaguzi,na mwanzo wa bunge lijalo.uchaguzi wa spika....
  Kujitolea mhanga ni pamoja na kukubali matokeo hata kama umeshindwa....
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,384
  Likes Received: 3,142
  Trophy Points: 280
  nataka nione kasi naviwango atakavyoingia navyo novemberbaaa yakutikiswa kuledooma.................
   
 4. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tumesoma habari za Samwel Six,masurufu yake na wanawake wake.Nchi yeyote yenye morals ,tayari angeisha ondoka
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Writing something so on JF threads does not make it so. Habari Hizo ulizosoma hazina uthibitisho wala source documents kama vile tulivyoona EPA, RICHMOND, MEREMETA n.k. Sitta ni mpiganaji hasa, you can say all what you want but without solid proof of his moral conducts still will be nothing but hatred for his actions to make Parliament less fearful on speaking the truth about wizi unaofanywa na mafisadi kupitia mikataba kwa mwamvuli wa uwaziri au serikali au whatever you make call.
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hongera Sitta kwa uamuzi huo kama unatoka rohoni.Tuko nyuma yako.

   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  kaza buti kama kweli umeamua na kudhamiria kwa dhati tuko nyuma yako
   
 8. K

  Koba JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Bla blah blah blah blah...huyu si ndio alikuwa anapigana na kina Dr Slaa waliokuwa wanasema nchi inaangamia na kumpa ushahidi wote bado akaukataa,leo mafisadi wenzake wanataka kumtoa kwenye ulaji anajidai yuko upande wa wananchi,huyu mtu sio serious anatuchezea akili tuu
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  hapa point taken
   
 10. w

  wasp JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza Mhe. Sitta anapaswa kumuomba msamaha Dr. Slaa kwa jinsi alivyo mpiga danadana kuhusu hoja yake binafsi juu ya mafisadi mpaka Dr. Slaa akaamua kuwithdraw hoja hiyo na kuipeleka mwembe Yanga Temeke.
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,173
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Umesoma wapi habari za sitta kuhusu masurufu yake na wanawake, kwenye magazeti ya Mafisadi? Acha ushabiki wa kijinga huku ukishuhudia nchi yako ikiangamia
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,173
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280

  Katika vita mmoja akiteleza kisha akarudi kwenye mstari hakuna kulaumiana bali ni kusonga mbele.

  Kamanda Sita songa mbele na wapiganaji wenzako
   
 13. E

  Engineer JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha tusubiri na kuona atajitoa mhanga vipi. Lakini kama ni Sitta yule yule wa CDA na pale TIC na madudu yake yote, sioni huo uadilifu utaanza lini?

  Akipewa nafasi ya kutetea wananchi au kutetea serikali, ataenda kutetea serikali.

  Labda ameenda kuungama kwa mungu na kutubu ujambazi mkubwa aliofanya huko nyuma.

  Lakini vijana wengi hapa ni wapumbavu tu na wanashabikia bila kusoma historia ya mhusika. Sawa wote tunataka ufisadi uishe lakini kama viongozi wetu wenyewe ni akina Sitta, hapo tusitegemee matokeo.
   
 14. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Whether wanamtoa kwenye Uspika au la, kama nia anayo ya kupigana na ufisadi anaweza kufanya hivyo hata nje ya uongozi. Sisi wazalendo tutamuunga mkono kama ambavyo anaungwa mkono hivi sasa.

  Wanaoleta kashfa za mambo binafsi ni watu waliofilisika hoja! Wanaume wangapi wana nyumba ndogo nyingi na isitoshe zipo dini na mila za Kiafrika zinazoruhusu wake wengi. Acheni mambo hayo. Ni kuonyesha umbumbumbu wenu katika kujenga hoja zenye mshiko!
   
 15. M

  Mchili JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Alikua hajaujua ukweli na hakuamini. Baada ya kujua ukweli amejiunga kwenye mapambano. Kaza buti mzee.
   
 16. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ninyi watu kitendo chenu cha kuamua kukaa nyuma ya Six sikiungi mkono hata kidogo. Mnataka kumfanyia nini nyuma yake? Sikubaliani nasema.
  Kama nia yenu ni kuumunga mkona kutokana na kauli yake basi kaeni mbele yake ua pembeni yake. Vinginevyo acheni michezo yenu ya kula njama za kukaa nyuma ya viongozi.
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kaka umeongea vyema sana..huyu baada ya kuukosa U PM ndo kawa na kiwewe anahangaika tu kujifanya anapinga ufisadi...personally i dont see him serious and if he has anything meaningful for this country.otherwise i regard him as an opportunist tu..amewanyanyasa sana wapiganaji wa kweli akina Dr.Slaa na Zitto..kama anakerwa na ufisadi CCM anasubiri nini kuhama chama au kujitoa kabisa kwenye siasa.Mi simuelewi Mh.6
   
 18. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha kutukana watu kwa kuwaita wapumbavu. Wewe ndiwe mpumbavu ambaye unajali zaidi majungu kuliko kujali mustakabali wa nchi yako. Whatever you presume Sitta did in CDA or TIC is irrelevant midhali umekaa kimyaaa hukusema na wala hujatueleza lolote wakati wote huo mpaka sasa ulipoona watu wanamuunga mkono kwa kuwa jasiri! Sisi bwana hatuna haja ya kujua Sitta alikuwa na wanawake wangapi ama huko CDA aliendeshajie ofisi. Kwanza inavyoelekea ni kwamba wewe ni mmoja wa majeruhi wa uongozi wake and you are bitter about it which is too bad. Acha tupige vita mafisadi wanaoiangamiza nchi yetu kama utanuna kwa kuwa Sitta naye ameonyesha ujasiri kaa kando you are not the only pebble in the sea!

  And by the way, hii ni vita ya Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yetu na sio ya Slaa ama Sitta peke yake.
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ndo manake ,na alipoipeleka mwembe yanga ndo moto ukawaka mpaka leo tunaona akina Mwakyembe nao eti wanapigana na ufisadi..this country bwana is very funny
   
Loading...